Niliibiwa na Watanzania wenzangu?

Niliibiwa na Watanzania wenzangu?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2023
Posts
7,189
Reaction score
10,375
Mwishoni mwa mwaka Jana, nilienda nchini Kenya kupitia mpaka wa Sirari.

Kwa sababu nilifika "border" Usiku, niliamua kulala gesti ili niendelee na safari Asubuhi yake.

Nilimka vizuri, na nikatafuta wanakotoa huduma ya vyakula, nikaagiza supu ya kuku, ndizi mchesmsho na Pepsi.

Baada ya hapo, nilibadilisha hela ili kupata ya Kenya kabla ya kuvuka mpaka.

Kwa sababu nilikuwa na muda mrefu kidogo sijafika Tarime, niliamua kutembea tembea kabla ya kuvuka mpaka. Nilipotosheka, nilirejea tayari kuingia Kenya.

Lakini mita chache kabla ya kufika kwenye ofisi za Uhamiaji, mtu mmoja alinifuata na kunipigisha stori kidogo kabla ya kujitambulisha kuwa yeye anatoa huduma ya kubadilisha fedha, na kuniomba aniuzie fedha za Kenya.

Nilivutiwa na uwezo wake wa kujieleza, alionekana ana "skills" za "customer care".

Ingawa nilikuwa nimeshabadilisha fedha, niliamua kutunuku jitihada zake japo kwa kwa kiduchu. Nilikubali kubadilisha tena Tsh 100,000/= kupata Ksh.

Alinipeleka kwenye alichokiita ofisi yake, ambayo ilikuwa jirani na barabara.

Shangao la kwanza: akampigia mwenzake na kumjulisha kuwa kuna mtu anataka kubadilisha hela hivyo aje na "cash". Nikawa najiuliza, huyu ndiye mwenye ofisi au ni dalali?

Mshangao wa pili: aliyeambiwa aje na hela, hakuja peke yake. Alikuja na watu wengine kama watatu. Nilipoona hivyo, nilisogea karibu na mlangoni, muamala tukaufanyia hapo. Sikutaka "kuzama" ofisini kwao.

Mstuko wa kwanza: nilipohesabu hela ya Kenya niliyoinunua kwa Tsh 100,000/=, niligundua nilipunjwa pesa ya Kenya sawa na kama Tsh 6,000/=.

Nilipolieleza hilo, mfanya muamala akaomba azihesabu tena. Alifanya hivyo na akajiridhisha kuwa ni kweli alikuwa amenipunja, na kuongeza kiasi kilichokuwa kimepelea. Wakati wote hayo yakifanyika, nilikuwa nimemkodolea macho ili asinipunje tena.

Nilipokabidhiwa hela, nikaanza kuzihesabu kwa lengo la kuhakikisha kwa mara nyingine. Zilikuwa noti za sh Ksh 50, 100, 200, n.k. Muda nafanya uhakiki, nilikuwa nimesimama nje ya "ofisi" yao. Mmoja wao akanitahadharisha kuwa si vizuri kuzihesabu pesa hadharani maeneo hayo, kwa sababu kuna watu wasio wema. (Wakati inawezekana wao ndiyo hawakuwa wema)
Sikumtilia mashaka.

Hawakuridhika na hicho kiasi nilichobadilisha. Waliendelea kunishawishi ili nibadili hela nyingine nyingi zaidi ili nisiende kupungukiwa huko niendako. Ni mpaka pale nilupowaambia kuwa hiyo 100,000/= niliyobadili kwao ndiyo iliyokuwa hela pekee ya Tanzania niliyokuwa nimebakiwa nayo.

Jibu hilo liliwafanya waje na ushauri mwingine, safari hii, wakijifanya kunipa ushauri utakaonisaidia kufika haraka niendako. Sijui walinionaje?

Waliniambia wanitafutie bodaboda wa kuniptisha njia ya "short cut" ili nisipite kwenye ofisi za Uhamiaji! Hapo ndipo kengele ya tahadhari ilupoanza kugonga.

Kwa nini nipite njia ya panya wakati nina vibali vya kupita njia sahihi?

Hata bei ya bodaboda waliyonitajia ilikuwa ni ndogo sana, ukilinganisha na nauli ya magari ya abiria.

Nadhani, walifikiri mimi ni mgeni sana Kenya. Isingewezekana kwenda kwa bodaboda umbali wa zaidi ya "counties" mbili, tena kwa nauli waliyonitajia. Huenda, walikuwa na agenda yao ovu.

Hata kwa usafiri wa gari, sikuweza kufika siku hiyo. Nililazimika kulala mji fulani na nikaendelea na safari kesho yake Asubuhi.

Nilichohisi ni kuwa walifikiri begi nilikuwa nalo lina "mali", hivyo, huenda walikuwa wanatengeneza amazingira ya kwenda kuniteka. Au, walitaka niingie Kenya kwa njia ya panya ili wakanikitanishe na Askari Polisi au Afisa Uhamiaji wa mchongo. Inawezekana hawakuwa watu wazuri.

Mara tu baada ya kuingia upande wa Kenya, nilihitaji kupata huduma fulani iliyohitaji kutumia hela. Ndipo nilipogundua
kuwa katika ile Tsh 100,000/= niliyoibadilisha mwishoni, shilingi elfu kama ishirini za Kitanzania zilikuwa zinamisi.

Sina uthibitisho, lakini mwenendo waliouonesha unanishawishi kuamini kuwa wao ndiyo walioniibia. Sijajua walitumia mbinu gani kwa sababu walipokuwa walionibadilishia, nilikuwa nikiwakodolea sana macho ili kuepuka kupunjwa, lakini bado nilipunjwa.

Japo ni hela kidogo lakini iliniuma sana. Ni bora kama ningekuwa nimempa alau mtu, lakini siyo kuibiwa "kizembe" vile. Ninachukiansana kuibiwa. Ninachukia mno kupunjwa.

Nipo tayari nimsaidie mtu (bure) sh 10,000/= lakini sikubali nipunjwe sh 100/=.

Nilienda Kenya salama, na nikarudi salama kwa kuzungukia Kampala, lakini hiyo Tsh 20,000/= bado ilikuwa ikiniuma.

Sina uhakika kama ni hao Watanzania wenzangu ndiyo walioniibia, lakini ushahidi wa kimazingira unanishuhudia kuwa huenda ni wao, na walitamani kuiba zaidi ya hiyo sh 20,000/=, sema tu hawakufanikiwa kupata hiyo fursa.

Inawezekana ni Watanzania wenzangu ndiyo walioniibia(ingawa sina uhakika kama ni Watanzania kweli. Pale ni mpakani, ni kawaida kwa watu wa mpakani kuchangamana na wa upande wa pili bila kubwaghudhiwa).

Kama si Watanzania wenzangu ndiyo walioniibia, hela yangu ilipoteaje?
 
Wazoefu wanajua kuna dada mmoja aliibiwa style hii hii unasema imepungua anakwambia lete nihakiki unaangalia kwa macho yako anaongezea iliyobaki ila chini ananyofoa zaidi ya aliyopunguza , wewe ukishaona ameongeza iliyopungua unakuwa huna wasi wasi haurudii kuhesabu , kumbe kachomoa
 
pendelea formality. achana na shortcuts. unaishi dunia ya ukimani ambako wamejaa kima hawajastaarabika
 
Sehemu kama zile badili pesa mahali panapoeleweka ,wengi wanakuchezea mazingaombwe ,,wengi sana wamelizwa boda na hao jamaa wanaofata watu ili kubadili pesa, unaweza wekewa pesa feki au zikapotea/kupungua kimazingaombwe
Nimejifunza mkuu🙏

Sitarudia kosa. Kilichoniponza ni huruma ya "kijinga" iliyochochewa na "ukarimu" wa hila.

Siku za nyuma, wakati kuna usafiri wa moja kwa moja kutokea Jijini Mwanza, nilikuwa nabadilishia kwenye basi kwa sababu walikuwa wakiutoa "rate" nzuri kuliko "burea de exchange". Sikuwahi kubadilishia mpakani. Ilikuwa ama benki, burea exchange au kwenye basi.

Siku hiyo sikutaka kubadilishia jijini Mwanza kwa sababu sikutaka kutembea na kiasi kikubwa cha "cash". Ndiyo maana niliamua kwenda kubadilishia Sirari.
 
Ni uzembe wako, usilaumu Watu.
Kwani hujui taratibu za kiusalama unazopasa kuzifuata wakati unapofanya safari za kimataifa? Kwa nini haukuzingatia taratibu za ununuzi wa fedha za kigeni??
Nakubali ni uzembe wangu, na wala silaumu, ila nilikasirishwa.

Na kingine, ni sehemu ya shule katika maisha. Nimejifunza.

"We learn through mistakes". Kutapeliwa sh 20,000/= kumenifungua macho ili hilo lisijirudie.
 
Mwishoni mwa mwaka Jana, nilienda nchini Kenya kupitia mpaka wa Sirari.

Kwa sababu nilifika "border" Usiku, niliamua kulala gesti ili niendelee na safari Asubuhi yake.

Nilimka vizuri, na nikatafuta wanakotoa huduma ya vyakula, nikaagiza supu ya kuku, ndizi mchesmsho na Pepsi.

Baada ya hapo, nilibadilisha hela ili kupata ya Kenya kabla ya kuvuka mpaka.

Kwa sababu nilikuwa na muda mrefu kidogo sijafika Tarime, niliamua kutembea tembea kabla ya kuvuka mpaka. Nilipotosheka, nilirejea tayari kuingia Kenya.

Lakini mita chache kabla ya kufika kwenye ofisi za Uhamiaji, mtu mmoja alinifuata na kunipigisha stori kidogo kabla ya kujitambulisha kuwa yeye anatoa huduma ya kubadilisha fedha, na kuniomba aniuzie fedha za Kenya.

Nilivutiwa na uwezo wake wa kujieleza, alionekana ana "skills" za "customer care".

Ingawa nilikuwa nimeshabadilisha fedha, niliamua kutunuku jitihada zake japo kwa kwa kiduchu. Nilikubali kubadilisha tena Tsh 100,000/= kupata Ksh.

Alinipeleka kwenye alichokiita ofisi yake, ambayo ilikuwa jirani na barabara.

Shangao la kwanza: akampigia mwenzake na kumjulisha kuwa kuna mtu anataka kubadilisha hela hivyo aje na "cash". Nikawa najiuliza, huyu ndiye mwenye ofisi au ni dalali?

Mshangao wa pili: aliyeambiwa aje na hela, hakuja peke yake. Alikuja na watu wengine kama watatu. Nilipoona hivyo, nilisogea karibu na mlangoni, muamala tukaufanyia hapo. Sikutaka "kuzama" ofisini kwao.

Mstuko wa kwanza: nilipohesabu hela ya Kenya niliyoinunua kwa Tsh 100,000/=, niligundua nilipunjwa pesa ya Kenya sawa na kama Tsh 6,000/=.

Nilipolieleza hilo, mfanya muamala akaomba azihesabu tena. Alifanya hivyo na akajiridhisha kuwa ni kweli alikuwa amenipunja, na kuongeza kiasi kilichokuwa kimepelea. Wakati wote hayo yakifanyika, nilikuwa nimemkodolea macho ili asinipunje tena.

Nilipokabidhiwa hela, nikaanza kuzihesabu kwa lengo la kuhakikisha kwa mara nyingine. Zilikuwa noti za sh Ksh 50, 100, 200, n.k. Muda nafanya uhakiki, nilikuwa nimesimama nje ya "ofisi" yao. Mmoja wao akanitahadharisha kuwa si vizuri kuzihesabu pesa hadharani maeneo hayo, kwa sababu kuna watu wasio wema. (Wakati inawezekana wao ndiyo hawakuwa wema)
Sikumtilia mashaka.

Hawakuridhika na hicho kiasi nilichobadilisha. Waliendelea kunishawishi ili nibadili hela nyingine nyingi zaidi ili nisiende kupungukiwa huko niendako. Ni mpaka pale nilupowaambia kuwa hiyo 100,000/= niliyobadili kwao ndiyo iliyokuwa hela pekee ya Tanzania niliyokuwa nimebakiwa nayo.

Jibu hilo liliwafanya waje na ushauri mwingine, safari hii, wakijifanya kunipa ushauri utakaonisaidia kufika haraka niendako. Sijui walinionaje?

Waliniambia wanitafutie bodaboda wa kuniptisha njia ya "short cut" ili nisipite kwenye ofisi za Uhamiaji! Hapo ndipo kengele ya tahadhari ilupoanza kugonga.

Kwa nini nipite njia ya panya wakati nina vibali vya kupita njia sahihi?

Hata bei ya bodaboda waliyonitajia ilikuwa ni ndogo sana, ukilinganisha na nauli ya magari ya abiria.

Nadhani, walifikiri mimi ni mgeni sana Kenya. Isingewezekana kwenda kwa bodaboda umbali wa zaidi ya "counties" mbili, tena kwa nauli waliyonitajia. Huenda, walikuwa na agenda yao ovu.

Hata kwa usafiri wa gari, sikuweza kufika siku hiyo. Nililazimika kulala mji fulani na nikaendelea na safari kesho yake Asubuhi.

Nilichohisi ni kuwa walifikiri begi nilikuwa nalo lina "mali", hivyo, huenda walikuwa wanatengeneza amazingira ya kwenda kuniteka. Au, walitaka niingie Kenya kwa njia ya panya ili wakanikitanishe na Askari Polisi au Afisa Uhamiaji wa mchongo. Inawezekana hawakuwa watu wazuri.

Mara tu baada ya kuingia upande wa Kenya, nilihitaji kupata huduma fulani iliyohitaji kutumia hela. Ndipo nilipogundua
kuwa katika ile Tsh 100,000/= niliyoibadilisha mwishoni, shilingi elfu kama ishirini za Kitanzania zilikuwa zinamisi.

Sina uthibitisho, lakini mwenendo waliouonesha unanishawishi kuamini kuwa wao ndiyo walioniibia. Sijajua walitumia mbinu gani kwa sababu walipokuwa walionibadilishia, nilikuwa nikiwakodolea sana macho ili kuepuka kupunjwa, lakini bado nilipunjwa.

Japo ni hela kidogo lakini iliniuma sana. Ni bora kama ningekuwa nimempa alau mtu, lakini siyo kuibiwa "kizembe" vile. Ninachukiansana kuibiwa. Ninachukia mno kupunjwa.

Nipo tayari nimsaidie mtu (bure) sh 10,000/= lakini sikubali nipunjwe sh 100/=.

Nilienda Kenya salama, na nikarudi salama kwa kuzungukia Kampala, lakini hiyo Tsh 20,000/= bado ilikuwa ikiniuma.

Sina uhakika kama ni hao Watanzania wenzangu ndiyo walioniibia, lakini ushahidi wa kimazingira unanishuhudia kuwa huenda ni wao, na walitamani kuiba zaidi ya hiyo sh 20,000/=, sema tu hawakufanikiwa kupata hiyo fursa.

Inawezekana ni Watanzania wenzangu ndiyo walioniibia(ingawa sina uhakika kama ni Watanzania kweli. Pale ni mpakani, ni kawaida kwa watu wa mpakani kuchangamana na wa upande wa pili bila kubwaghudhiwa).

Kama si Watanzania wenzangu ndiyo walioniibia, hela yangu ilipoteaje?
Pole sana. Hata mimi hakuna mtu nayemchukia kama mwizi. Ushauri: Katu, katu usipende mtu usiyemjua akuzoee hasa unapokuwa safarini. Mambo ya kuonea huruma watu tupa kule, na fanya mambo yako yote kwa kutumia official channels! Epuka sana watu wanaojifanya wako friendly kwako na usimwambie mtu yeyote kuhusu safari yako na ikibidi basi uwe na tahadhari sana.
 
Wazoefu wanajua kuna dada mmoja aliibiwa style hii hii unasema imepungua anakwambia lete nihakiki unaangalia kwa macho yako anaongezea iliyobaki ila chini ananyofoa zaidi ya aliyopunguza , wewe ukishaona ameongeza iliyopungua unakuwa huna wasi wasi haurudii kuhesabu , kumbe kachomoa
Kumbe!

Nafikiri ndicho walichonifanyia. Bora tu haikuwa hela nyingi. Wale walikuwa "full" matapeli.
 
Pole sana. Hata mimi hakuna mtu nayemchukia kama mwizi. Ushauri: Katu, katu usipende mtu usiyemjua akuzoee hasa unapokuwa safarini. Mambo ya kuonea huruma watu tupa kule, na fanya mambo yako yote kwa kutumia official channels! Epuka sana watu wanaojifanya wako friendly kwako na usimwambie mtu yeyote kuhusu safari yako na ikibidi basi uwe na tahadhari sana.
Uko sahihi mkuu!
 
Asee matapeli wamefanya hata watu wenye uhitaji wa msaada kukosa huo msaada kwa kuhisiwa ni matapeli. Yani huwa nakataa kabisa kuonesha ushirikiano na mtu simjui kwenye gari halafu anaanza kujiongelesha
 
Ni uzembe wako, usilaumu Watu. Kwani hujui taratibu za kiusalama unazopasa kuzifuata wakati unapofanya safari za kimataifa? Kwa nini haukuzingatia taratibu za ununuzi wa fedha za kigeni?
Kwenye hizi technique za wezi sidhani kusema uzembe kama haijakaa sawa , sidhani kama kuna mtu hajawahi kuibiwa kwa namna yeyote iwe kutapeliwa barabarani, nyumbani, hata kuvamiwa pia
 
Back
Top Bottom