Niliingizwa kwenye Kampeni za kisiasa tangu nilipokuwa darasa la Tano

Niliingizwa kwenye Kampeni za kisiasa tangu nilipokuwa darasa la Tano

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2020
Posts
7,899
Reaction score
10,415
Habari za leo ndugu wana jamii forum,

Kiukweli nilianza harakati za siasa nikiwa kijana mdogo sana. Nakumbuka Mwaka 2005 nikiwa na umri wa miaka 13, kipindi hicho nipo darasa la tano ndipo nilipoingizwa rasmi katika harakati za kisiasa.

Mambo yalikuwa hivi, kaka yangu ambaye sito mtaja jina hapa kwasababu za kiusalama alichukua form ya kugombea ubunge jimbo ambalo sitalitaja pia. Kama unavyo jua kwenye kampeni hizi za kung'ang'ania kiti cha kugombea ubunge ndani ya chama lazima udili sana na wajumbe wa chama. Hivyo kaka yangu alianza kunituma kumnadi kwa wajumbe wa chama waliopo ndani ya tarafa yetu ili wapate kumchagua.

Hapo nilinunuliwa biaskeli moja hivi kubwa phonex la mchina kwaajili ya kuwatembelea wajumbe na kuwashawishi kwamaneno ili wamchague kaka yangu. Hivyo kila nikirudi toka shule ilikuwa ndio kazi yangu kuwatembelea wajumbe wa CCM ndani ya tarafa yangu. Nilipata kumnadi vilivyo kaka yangu, ndani ya mwezi mmoja wajumbe wote walikuwa wanamfahamu kaka yangu.

Familia yangu toka enzi na enzi ni wana CCM hivyo mimi na CCM ni damu damu. Basi watu ilibidi wanipatie jina la Mbunge, kila wakiniona tu walikua wananiita mbunge. Kwa hiyo tangia hapo nikawa na ndoto ya kuwa mbunge, niliapa kwamba lazima niingie bungeni.

Mama yangu ameshiriki kuwa kampein meneja wa mbunge fulani hivi jina kwenye mabano, lakini pia kwa ile kata yetu mimi na mama ndio tulikua wahamasishaji wa watu kumchagua Rais wetu Dr. Magufuli mwaka 2015. Kiukweli tulifanikiwa kwa asilimia 90 kumnadi na kuwashawishi wananchi. Kutokana na uzoefu wangu mkubwa kwenye siasa wananchi wa jimbo langu wamekuwa wakinitaka nigombee ubunge.

Hivyo mwaka huu nilitegemea kuchukua form lakini nimeshindwa kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wangu. Lakini nadhani mwaka 2025 mambo yatakua mazuri maana nitakuwa nimejipanga vilivyo.

Mwisho:
Tanzania ni yetu sote,
Tuache maneno maneno bali tugombee nafasi za ungozi ili kujipima kabla ya kulaumu.

Ni wenu katika ujenzi wa Taifa.
Meneja wa Makampuni
Bwana Mbunge Mtarajiwa.
 
Mgawa rushwa toka mdogo anataka kuwa mbunge
 
Back
Top Bottom