Nilikufa huku najiona kwa dakika chache halafu nikawa hai

Rihana

JF-Expert Member
Joined
Apr 26, 2013
Posts
498
Reaction score
250
Ndugu wanabodi,

Juzi nilikuwa nimelala usiku ghafla nikashtuka na kufungua macho, nikawa na fahamu lakini mwili wote ukawa ume paralyse siwezi hata kuinua kiungo hata kimoja hali hiyo ilidumu kwa dakika chache nikajikuta napiga kelele ndipo mwili ukarudi hali ya kawaida. Kwa kifupi nilikufa kwa dakika chache hii ni condition gani? Matabibu nijuzeni
 

Hiyo inatokeag kama ukiwa haupo vizuri kiroho, ulipitiwa na upepo mbaya.
 
juzi leo umepona? 60% ya maneno wanayosema au wanayoandika waafrika huwa ni uongo
 
Fanya maombi ndugu yangu, usijali dini uliyonayo. Inawezekana mkuu wa giza alikupitia kwa mda. Maana usiku kuna mengi kama upo kwa Mungu basi kaa kwa Mungu kiukamilifu na kama upo Upande wa pili kaa huko kiukamilifu. Usiwe njia panda
 

Hahaha, funny jinsi watu wanavoamini mambo ya kichawi na majini humu ndani, watanzania bado tuna kazi sana naona.. hayo majini yakufate wewe umeyafanyia nini..

Hii hali inaitwa sleep paralysis, inatokea mara nyingi tu, mimi ilikua inanitokea karibia kila siku hadi nlivobadili style ya kulala, hamna uchawi wala mambo yoyote ya kiimani, hii iko kisayansi kabisa...

Mtu akilala kuna stage anazopitia, hili hua linajitokea sanasana katika stage ya REM, hii stage kuna chemicals zinakua produced kwenye mwili kuzuia mtu kureact wakati amelala, bila hizi chemical mtu angekua anaota anarusha mikono au anatingisha miguu, sasa ikitokea disturbance yoyote ya kufanya ubongo ukawa active katika stage hii ndo hali hii inatokea, baada ya muda kidogo chemical effect inaisha mtu unaamka kawaida.
 

mkuu wachawi wametoka wapi tena? umesoma vizuri post yangu?
 
mkuu wachawi wametoka wapi tena? umesoma vizuri post yangu?
wewe umesoma nilichojibu ukaelewa?? au hujaona watu wanapost wanasema ni mambo ya kiimani hapo juu, soma reply ya kwanza, ya pili, ya tatu.. afu soma vzr na paragraph yangu ya kwanza uone inamuongelea nani afu rudi uulize tena hilo swali lako
 
Sleeping Paralysis....


Waswahili huita Jinamizi....Ni kawaida...huwainachukua sekunde tamo mpka kumi lakini unaweza ona ni masaa
 
Fanya maombi ndugu yangu, usijali dini uliyonayo. Inawezekana mkuu wa giza alikupitia kwa mda. Maana usiku kuna mengi kama upo kwa Mungu basi kaa kwa Mungu kiukamilifu na kama upo Upande wa pili kaa huko kiukamilifu. Usiwe njia panda

Mkuu wa giza..???
 

Ahsante.....Maeleze haya kwa lay wa kawaida anaelewa...yamejitosheleza
 
Wacha uongo....

Jiongeze ufahamu wako.....Google kitu kinaitwa Sleeping Paralysis

Hakun kitu ambacho wanasayansi watakosa explaination ya kusema, by the way sijakulazmsha ukubali nilichosema……
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…