wastani kwa idadi
JF-Expert Member
- Jun 28, 2024
- 503
- 1,432
Naiandika hii ppost kwa sababu nimeona kuna uzi wa "nifenyeje wanangu wawe na akili darasani"
Kwanza kabisa niseme nyumbani kwetu hili lilikuwa ni tatizo kwa watoto wote labda kasoro kwa mdogo wangu tu ambae ni wa mwisho, wawili wa mwanzo walishakataa shule kiasi cha kutishiwa kuletewa polisi, badili shule sana, piga sana, ku resit mara 3, n.k. hadi wamehitimu chuo umepigwa mwingi sana.
Binafsi nilikuwa nasoma shule nzuri ya msingi tena english medium wanafunzi 28 tu darasani lakini tatizo lilikuwa ni kukosa umakini napofundishwa na kuhusu kujisomea sijawai kabisa nilianza form 5, yaani nilikuwa napenda sana kufanya mambo mengine kama kuchekesha darasa, kupiga stori, kucheza, n.k. ila sio kusoma.
Mimi binafsi na mdogo wangu walituwahi, tuliletewa mwalimu nyumbani sio kama zile tuisheni hazina utofauti na darasani mpo wengi, NO !! ni macho kwa macho attention kama yote ipo kwajili ya watu wachache tu, kwangu nilianza darasa la tatu, mdogo wangu aliwahi na nikiri alikuwa Genius nafasi zake ni top 3.
Shuleni sikuwa na umakini, ilikuwa sehemu ya michezo, stori, mizaha, n.k. lakini nikirudi nyumbani namsubiri mwalimu tunasoma masaa mawili hivi, ni hali iliyowaduwaza hata marafiki zangu tuliofanya mizaha kushangaa inakuwaje wao wapo mwishoni lakini mimi nipo nafsi ya 4 hadi 6
hapo darasa la tano kidogo nikapelekwa tuition tupo wanafunzi 10, mimi na wenzangu wanne tuliokuwa tunasoma darasa moja na hao ndio walikuwa wanashika top 3 mimi nipo nafasi ya 4 hadi 6, mdogo wangu na mwenzake wa darasa moja, mtoto wa mwalimu na mwenzake na mwengine alikuwa peke yake, kulikuwa na vyumba viwili ikifika zamu ya darasa flani tunaenda chumba cha mwalimu sisi tunakuwa wanne tu na mara nyingi sana alinikazania sababu nilikuwa na uwezo mdogo kuzidi wenzangu ilikuwa ngumu kupoteza focus sababu kachumba ni kadogo yani ni macho kwa macho, ikifika zamu ya wengine tunawapisha sisi tunaenda kufanya maswali chumba kingine.
Darasa la saba nilipasua fresh kabisa lakini wazazi hawakutaka kabisa kusikia shule za serikali na hapo, Nilipelekwa boarding, tatizo langu lilinisumbua sana nikaanza kushika nafasi za mwisho hata mwenzangu tuliesoma nae shule ya msingi niliyekuwa nampita alishangaa sana,
nikirudi nyumbani likizo napelekwa tuition hizi tunajazana watu kibao, wala haikusaidia chochote, form 4 nilipata division 3 ya kuchechemea sana, ila si haba niliweza kupata credit tatu.
Form 6 nilirudi day na nikawa naletewa mwalimu nyumbani, form 6 nikawa naenda sehemu tupo watatu tu, ukiongeza na kuanza kujisomea nilibutua division 2 safi tu, shuleni hapo two zilikuwa 3, one moja, three kama 50, four kama 10, zero 2.
Chuoni mwaka wa kwanza ulinirarua vibaya mno, nilifeli masomo mawili il niliya clear kwenye sup, mwaka wa pili ndio nilianza kwenda discussion ilisaidia sana, kifupi nilihitimu n gpa ya 3.9 si haba.
nikaunga na masters sababu ya umri mdogo nikaipiga fresh kabisa.
Kazi nikaipata, kazi nyingi zinawezwa kufanywa hata na darasa la nne wanaofoji byeti sio kama mziki wa kupata vyeti darasani