Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, nilikuwa nafanya hicho kitendo kuanzia mwaka juzi na mwaka jana, katika mazingira fulanifulani almanusra nifumaniwe na kufedheheka,
Namshukuru Mungu alininusuru, ningepata fedheha ya milenia kwasababu mwenye nzigo ni mtu wangu wa karibu sana ni zaidi ya ndugu, hata wakati wa kupeleka mahari ukweni nilikuwemo kwenye msafara.
Baada ya kunusurika nikatubu na kuapa kamwe sitorudia tena, lakini pamoja na kutubu kote nafsi yangu haina amani kabisa najihisi mwenye hatia kila nikikumbuka, kibaya zaidi jamaa ananiamini sana mpaka mambo yake ya ndani huwa ananiambia
Mimi ni mshauri wake mkuu,nawaza nilipe faini pasipo yeye kujua ili niwe na amani, Kuna pesa namdai 550,000 aliahidi kunilipa tarehe 30 mwezi huu lakini jana kaja kujieleza hakufanikiwa kupata nisubiri mpaka 30 mwezi ujao,
Sasa mimi nataka hiyo pesa asinilipe nijitoze faini mwenyewe au kwa lugha nyingine nichangie mahari, naomba ushauri wenu wanaJF nipeni mbinu wanaJF nifanyeje ili yeye abaki na pesa na mimi nibaki na utulivu wa nafsi.