Cephas Saphiel
Member
- May 25, 2009
- 32
- 16
Habari zenu wanajukwaa. Naamini ni kwa rehema za Mungu kufika hapa hata pia kutupa akili na mtaji kidogo na kuwaza la kufanya. Nimenunua shamba Morogoro lisilopungua Hekari kumi ila naumiza kichwa ni nini nilime kiweze kunilipa. Niliwaza kulima mazao ya muda mrefu especially kokoa lakini nimeona wanunuzi ni monopoly sana na bei wanapanga coz mnunuzi mkubwa ni mohamed enterprisess na gharama hazinilipi nikijumlisha na usafiri mpaka kumfikishia. Haina maana sitaki kulima mazao ya muda mfupi, ninachotaka mimi ni kupata mwanga wa faida ya uhakika hata kwa baadae. Naombeni mawazo yenu ndugu zangu nilime nini coz ardhi inarutuba sana na barabara ipo nzuri. Please nisaidie kwa hilo. Ahsanteni sana.