Nilime nini kinilipe?

Joined
May 25, 2009
Posts
32
Reaction score
16
Habari zenu wanajukwaa. Naamini ni kwa rehema za Mungu kufika hapa hata pia kutupa akili na mtaji kidogo na kuwaza la kufanya. Nimenunua shamba Morogoro lisilopungua Hekari kumi ila naumiza kichwa ni nini nilime kiweze kunilipa. Niliwaza kulima mazao ya muda mrefu especially kokoa lakini nimeona wanunuzi ni monopoly sana na bei wanapanga coz mnunuzi mkubwa ni mohamed enterprisess na gharama hazinilipi nikijumlisha na usafiri mpaka kumfikishia. Haina maana sitaki kulima mazao ya muda mfupi, ninachotaka mimi ni kupata mwanga wa faida ya uhakika hata kwa baadae. Naombeni mawazo yenu ndugu zangu nilime nini coz ardhi inarutuba sana na barabara ipo nzuri. Please nisaidie kwa hilo. Ahsanteni sana.
 
lima mipapai inavumilia hali zote za jua na mvua.
 
lima vegetables zinalipa, kuna jamaa yangu alienda moro last year kuanza kilimo sasa anakuja dar amejaza lory mara mbili kwa wiki analeta mboga mboga

Kweli mkuu!!,mazao ya mbogamboga ndo habari ya mjini siku hizi.
 

Lima Matunda na Mbogamboga zina faida acha kabisa hautajuta.
 

Morogoro sehemu gani?kama dakawa ukilima Mahindi utapeta sana maana kuna ghala la chakula hapo serikali itayanunua.Ila pia mbaazi zinalipa na morogoro zinastawi,kwa sass mbaazi inauzwa Tshs.1300-1500/= kwa kilo moja.
Wadau wamependekeza mbogamboga hapa,nakubaliana nao maana kuna mtu nayemfaham analima na anauza fresh tu maeneo ya mvomero
 
Nashukuru sana wadau ila kamanda Swissme kaniacha hoi hapo kwenye bange, wadau suala la kulima mahindi lilikua ni la mwanzo ila mahindi hayana bei huwezi kupata faida nzuri kwa shamba la kiasi hiki. Kwa suala la kokoa bei si nzuri kwa sasa labda kwa baadae, ufuta ni wazo zurinpia na choroko hata maharage au viungo. Vipi kuhusu soko la viungo? Kuna mwenye idea kuhusu hili tafadhali? Niliwaza kulima matunda pia kama alivyoshauri mwanajukwaa hapo juu kuhusu mapapai. Niliwaza kuhusu ndimu au malimao hata embe au parachichi. Ninyi mnaonaje? Cha msingi ni soko kabla ya kuanza kulima. Naomba ushauri ndugu zangu. Shukran sana
 
Mbogamboga zinalipa ndio na soko nadhan lipo ila nadhan niifanye plan B kwa baadae kidogo ili nipate nguvu ya kuzilima kisasa zaidi kama kwa green house au drop irigation kwa mavuno mazuri.
 
Mkuu naomba unitumie namba yako tuwasiliane kuhusu mbaazi.au nicheki kwa 0655509828.tafadhali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…