Habari Za Mchana Wana Jamvi, Nina Shamba Langu La Hekari 2 Kule VIGWAZA, Nataka Nilime, Nilimuuliza Mtu Nini Kizuri Cha Kulima Kule Akaniambia Ardhi Yake Ni Nzuri Kwa Kwa Kulima Mihogo Na Mahindi, Sasa Nilikuwa Nahitaji Mawazo/Maoni Zaidi Kwa Wenye Uzoefu Na Ardhi Ya VIGWAZA Kama Inafaa Kwa Kilimo Kingine Zaidi Ya Mihogo Na Mahindi, Nawasilisha..
Jaribu pia kuangalia na msimu tuliopo. Sidhani kama ukipanda mahindi this time yataota hata kama hiyo ardhi ni nzuri kwa mahindi!!
Habari Za Mchana Wana Jamvi, Nina Shamba Langu La Hekari 2 Kule VIGWAZA, Nataka Nilime, Nilimuuliza Mtu Nini Kizuri Cha Kulima Kule Akaniambia Ardhi Yake Ni Nzuri Kwa Kwa Kulima Mihogo Na Mahindi, Sasa Nilikuwa Nahitaji Mawazo/Maoni Zaidi Kwa Wenye Uzoefu Na Ardhi Ya VIGWAZA Kama Inafaa Kwa Kilimo Kingine Zaidi Ya Mihogo Na Mahindi, Nawasilisha..
Vipi akimwagilia, si anauza mabichi kwa ajili ya kuchoma.
Mkuu,
Maji sio kigezo pekee cha kulima, hata majira ya mwaka nayo yana mchango mkubwa. Anaweza kuotesha mahindi kuanzia July na akamwagilia kila siku na yasiote sababu ya setting za jua, mvua, joto, baridi vya kipindi hiki visiwe rafiki.
Labda aangalie matikiti kama kuna vyanzo vya maji.
ni kweli mkuu, lakini maeneo aliyosema hakuna baridi ya kutishia uhai wa mahindi na kama ana uwezo wa kumwagilia kushindana na jua linavyochukua maji basi lazima avune. btw, wazo la tikiti maji huenda ni zuri zaidi kwa sababu zina soko zaidi, lakini ndiyo ajiandae kuzinywesha maji ya kutosha maana zina kiu hizo!