poisson
Senior Member
- Jul 17, 2016
- 130
- 42
Nilimpigia simu mwanamke mmoja niliyekuwa namdai fedha zangu, lakini hakupokea simu yangu.[emoji2]
Nilipiga mara 10 zaidi, akagoma kupokea. Nikitambua mumewe alikuwa safari, nikaamua kumtumia meseji hii:
"Halo dada, ninakupigia siyo kukukumbusha deni langu. Nilitaka tu kukwambia kwamba wasichana wawili walikuwa wakipigana kumgombea mumeo leo hapa mjini. Ulikuwa ugomvi mkubwa na yeye alikuwa akitazama tu, mpaka mmojawao alipofanikiwa kuchoropoka mumeo na msichana mwingine yule aliyebaki wakaondoka."
Baada ya dakika chache akanipigia lakini sikupokea. Aliendelea kupiga karibu mara 21 kisha akatuma meseji hii:
"Ugomvi umetokea wapi?
Wameelekea wapi?
Umewatambua hao wasichana? Tafadhali niambie, nimechanganyikiwa."
Nilisoma ujumbe wake nikaupuuza. Akapiga tena, karibu mara tano na sikupokea, kisha akatuma meseji nyingine:
"Ninazo pesa zako, tafadhali tunaweza kukutana, ili unieleze zaidi?"
Mimi nikamjibu, "Sawa, unaweza kunitumia pesa kwa simu ili nipite kituo cha mafuta niongeze wese, halafu nitakupitia na kukupeleka nyumbani kwa msichana kwa sababu najua aliko."
Dakika mbili baada, nikapokea ujumbe wa salio langu kwamba amenilipa pesa zangu zote.
Nimeizima simu na sasa nimejilaza kitandani nipate usingizi...
Sipendi ujinga. Januari ni mwezi Dume lazima ujiongeze