Nilimsubiri Mwanamke Hotel hakutokea

Nilimsubiri Mwanamke Hotel hakutokea

Manyanza

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
16,464
Reaction score
35,629
Mwanamume mmoja aitwaye Leavan Namayi Lubanga Mkazi wa Kaunti ya Homa Bay Nchini Kenya, ameshitakiwa Mahakamani baada ya kushindwa kulipia bili ya Hoteli moja ya kifahari Jijini Nairobi alimokaa kwa siku 12 kuanzia December 30 2023 akimsubiri Mpenzi wake washerehekee mwaka mpya.

Imedaiwa kuwa Lubanga ameshitakiwa kwa kushindwa kulipa bili ya Ksh. 466,965 (Tsh. mil. 7,421,637) kitendo ambacho kimepelekea kukamatwa kwake January 11, 2024 katika Hoteli hiyo na kupelekwa kwenye Gereza la Industrial Area akisubiri kesi yake isikilizwe wiki mbili kutoka sasa.

Akiwa Mahakamani wakati alipopandishwa kwa mara ya kwanza, Lubanga amenukuliwa akimwambia Hakimu Mwandamizi Gilbert Shikwe kuwa Mwanamke wake ndiye chanzo cha yote yaliyotokea kwani aliahidi kulipa bili zote za hoteli atakapowasili lakini mwisho wa siku hakutokea kabisa.

Lubanga amenukuliwa akimwambia Hakimu maneno yafuatayo “Mheshimiwa nilidanganywa na Mwanamke nimsubiri katika Hotel ya Pan Pacific lakini hakutokea, nilimsubiri kwa siku 12, nimeshindwa kulipa bili ambayo inajumuisha mlo, malazi na pombe, yeye ndiye chanzo” #MillardAyoUPDATES
 
Back
Top Bottom