Nilimuambia; achague kumrudia mke wake au tumfungulie kesi ya Ubakaji. Ukatili kama huu haukubaliki

Robert Heriel Mtibeli

Platinum Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
40,153
Reaction score
93,069
NILIMUAMBIA; ACHAGUE KUMRUDIA MKE WAKE AU TUMFUNGULIE KESI YA UBAKAJI. UKATILI KAMA HUU HAUKUBALIKI.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

WIki hii nilipokea simu ya binti mmoja mwenye miaka 23. Hivi alijitambulisha anawatoto wawili.
Akaniambia anasoma makala zangu ingawaje zimejaa ubabe na upendeleo kwa wanaume(mtazamo wake).

Hivyo alinipigia simu kama kunishtakia kwamba, wanaume mbona nao ni wanyama, katili, washenze, na kwa nini siwaandami kama ninavyowaandama wanawake.

Anasema, yeye alipewa mimba miaka saba iliyopita akiwa kidato cha Tatu. Hali iliyomlazimu aache shule.

Kisha yule kijana akatiwa nguvuni na wazazi wake. Kwa sababu yeye binti Baba yake ni Askari polisi. Kijana alivyokamatwa, hofu ya kufungwa miaka 30 jela kwa kosa la ubakaji lilikuwa tishio la kuharibu maisha yake.

Baba Polisi akiwa na dhamiri ya kumfunga kijana. Binti katika namna ya kumuokoa mchizi, akatishia kujiua. Mama wa binti kuona hivyo na shinikizo la wazazi upande wa kijana, wakaanza kumshinikiza Baba Polisi kwamba haya mambo yanazungumzika.

Kijana na wazazi wake wakaahidi kufanya taratibu za kumuoa huyo binti. Kisha atakapojifungua binti angeendelea na shule.

Baba Polisi hasira zake zikapoa. Basi makubaliano yalikuwa watoe posa, wahudumie mimba, kisha mtoto akizaliwa binti ataendelea na shule.

Kijana akaachiwa. Maisha yakaendelea.

Binti anasimulia, baada ya mimba kufikisha miezi nane, Baba yake alifariki.
Baada ya mazishi iliamriwa binti akaishi na huyo kijana.

Binti akaanza maisha mapya kwa huyo kijana akiwa amebakiza wiki chache ili ajifungue.

Akajifungua, miaka ikaenda. Kijana alianza kubadilika vibaya mno. Hasa baada ya wao kuhama pale nyumbani na kwenda kujitegemea.

Walianzia kupanga chumba kimoja, wakiwa na godoro tuu. Yeye, kijana mtoto.
Mungu sio Athumani, kijana mambo yake yakawa yanafunguka, wakanunua kiwanja maeneo ya Tegeta. Wakajenga chumba sebule na Choo. Ambayo ipo mpaka hivi leo.

Kijana mali zote wanazonunua anaandika jina lake, huku mashahidi wakiwa Mama na ndugu zake. Binti kuona hivyo akauliza mbona mimi sioni jina langu hapo. Ikawa nongwa.

Wakapata mtoto wa pili. Kijana akawa mkorofi. Anamfokea na kumtukukana binti. Kisa na mkasa kijana kazidisha umalaya wa wazi, hizo ni dharau sasa.

Sasa kijana na mama na ndugu zake wamedhamiria kumfukuza huyo binti. Hati vyote viko nyumbani kwa binti. Binti maisha yake yamekuwa ya kulia.
Ajabu wote ni Wakristo tena wa dhehebu moja.

Binti akaniuliza hiyo ni sawa?
Nikamwambia sio sawa.

Akaniambia anataka kuondoka. Amuache hapo nyumbani. Ili awe na amani.

Nikamuuliza Mama yake anasemaje. Akaniambia Mama amekosa chakusema ukizingatia bi mkubwa mwenyewe mambo yake yenyewe yanamshinda. Ana presha zaidi sana anamtia matatizoni.

Nikamuambia tunaweza kukutana? Akasema tukutane kufanya nini? Nikamwambia nataka nimsaidie. Akasema niche tuu. Binti alikuwa analia mwanzo mwisho akiwa anasimulia.

Siku inayofuata Tukakutana pale makumbusho stendi.
Nikamwomba namba ya simu ya mumewe. Akanipa. Tukaongea wee. Huku naye akielezea upande wake.

Nikamwambia naye tunaweza kukutana. Siku inayofuata tukakutana Mbezi Beach Kwa Zena. Tukiwa wote watatu.

Siku hiyo sikuwa na maelezo mengi. Nilimwambia kijana anamachaguo mawili tuu.
Abaki na mkewe walee watoto na amheshimu mkewe kama alivyokuwa mwanzo.

Au amuache tukamfungulie mashtaka ya ubakaji aliyoyafanya miaka saba iliyopita. Nilimwambia jinai haiozi.
Nilimwambia alifanya kosa la ubakaji na kusitisha masomo ya binti mdogo asiye na uwezo wa kufanya maamuzi.

Hivyo kama anataka kukukaa na nondo miaka 30 basi afikirie kumuacha huyo msichana. Nikamwambia wapo wanasheria kibao watakaosimamia hiyo kesi na hilo jambo litatokea.

Hivyo kama Binti alimstiri na kumlinda miaka ile. Naye ni wajibu na jukumu lake kumstiri na kumlinda wakati huu. Hataki basi ajiandae kwa maisha ya jela.

Haiwezekani kijana hana sababu za kueleweka. Unamnyanyasa binti wa watu kiasi kile. Nilimwambia ku-cheat hata sisi tunafanya hivyo lakini sio kidharau namna hiyo. Kwamba waziwazi. Unajibu jibu unavyotaka. Kisa binti hana lolote la kukufanya. Mama yake hana lolote kisa mzee alishafariki. Huo ni ushenzi.

Nilimhakikishia yeye akitaka kuona jela kukoje basi amvuruge huyo binti.

Vijana, kuweni na fadhila. Mkiokolewa msisahau mlipotoka.

Na mabinti msikubali. Hakuna tuzo ya kumwachia Mungu.
Kijana alikupa mimba ukiwa shule, ukamstahi, ukamlinda, leo anakuletea za kuleta usimfanye aisha kwa amani. Usiende kuloga wala nini.

Wanasheria wapo wamejaa kibao. Hawana kazi. Hizo ndio kazi zao.

Yule Kijana alianza kwa kupandisha Kibesi, lakini alipoona ninamaanisha alirudi chini.
Nikamkumbusha yeye ni Mkristo. Aache mambo ya kishenzi shenzi.

Tulimaliza salama. Ingawaje kibabe na kwa vitisho vingi.

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
 
Uko sawa, ila km jamaa ana pesa, anaweza pindisha case na akavuka salama sakata.

Ikishindikana hapo ni kilogo tuu, wala hakihitaji mambo mengi.
Woiiiih
 
Uko sawa, ila km jamaa ana pesa, anaweza pindisha case na akavuka salama sakata.

Ikishindikana hapo ni kilogo tuu, wala hakihitaji mambo mengi.
Woiiiih

Angekataa ingejulikana huko mahakamani. Kuhusu ulozi huko hawezi kufanya lolote
 
Ndoa za sasa nyingi za wakristo hua zina mshikeri sana kuliko wenzetu waislamu tatizo liko wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…