Nilinusurika kwenye ajali hii

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001
Ilikuwa ni siku ya jumapili ya tarehe saba mwezi wa pili, mida ya saa nne usiku tulikuwa tukitokea pande za tegeta kuelekea maeneo ya mwenge.
Tukiwa tumefika maeneo jirani na mbezi jogoo kuna gari ilikuwa inaovateki na ilikuwa ikija spidi kali sana, kama 140 kwa saa. Tulisimama kwa kuwa hatukuwa na cha kufanya zaidi ya kumuomba mungu.
Gari dogo feroza yenye rangi ya blue ilitugonga kisha yenyewe kupinduka.
Kwenye gari yetu tulikuwa watu watatu, mimi na jamaa zangu wawili. Wote tulitoka tukiwa wazima wa afya njema.
Ila abiria waliokuwa kwenye gari iliyotugonga waliumia vibaya sana, hakukuwa na tukio lolote la kifo.
Mungu wetu ni mkubwa sana, mwenye upendo na rehema tele.










HIII ATACHMENT NAYO INAJITOKEZA NIKITAKA KUTUMA PICHA ZA AJALI..
SIJUI TATIZO NI NINI??
 
Pole Mkuu, but the pics are invisible to me!
 
Nimejaribu kuzi upload,
zinakubali kuwa uploaded, lakini ukienda kwenye preview zinasema kuna database error..
Mods watusaidie.
 
pole uncle jamani but Mungu ni mwema sana,usiache kulisifu jina lake daima
 
Pole na umshukuru Mungu kwa kukuepusha na ajali ile.
 
Nimejaribu kuzi upload,
zinakubali kuwa uploaded, lakini ukienda kwenye preview zinasema kuna database error..
Mods watusaidie.
Kuuliza si ujinga Wasiliana na Robot(Invisible) au Max warekebishe tuone Ziraili alivyotaka kuchukua roho yako. Hata hivyo ashukuriwe aliye juu ulisalimika.
 
pole Mkuu, japo ilikuwa ni usiku lakini upo makini sana kwenye defensive driving
 
Pole sana bwana shemeji.
Mbona umechelewa kututumia picha?
Mods wafanye mambo tuone ilivyokuwa
 
Pole sana kaka! Nahisi wanaweza kuwa vijana wa kihindi maana wanapenda sana kuendesha spidi wakielekea Bagamoyo. Hatahivyo nashauri next time u should take more action than just stopping. Kwa pale Jogoo ungeweza kupunguza mwendo huku ukiingia pembeni uache mwanya kwa hao wehu kipita probably wote mngekuwa wazima bila jeraha hata kidogo.

NB: Don't argue with a fool coz people might not notice the difference
 

Kwenye bold hapo lol lakini am not arguing!
 
Kuuliza si ujinga Wasiliana na Robot(Invisible) au Max warekebishe tuone Ziraili alivyotaka kuchukua roho yako. Hata hivyo ashukuriwe aliye juu ulisalimika.

watu mnachekesha ..
Pole Bujibuji mungu ni mwema sana hata kukuweka salama mpaka leo ..
 
Mie picha sizioni naona nyota nyota tu.
Pole mkuu laiti ungejifanya mbabe tungekuwa tunaongea mengine hapa.
 


BB, sioni picha!!!
Au ni mimi tu!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…