Nilipokoswa koswa kuambukizwa UKIMWI nikiwa mdogo

Nilipokoswa koswa kuambukizwa UKIMWI nikiwa mdogo

mr vata

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2017
Posts
465
Reaction score
616
Katika maisha tunapitia visa vingi sana ambavyo vingine kama tukiwa makini vinatuachia funzo kubwa. Tuna mikasa mingi ambayo kama ukipata mtu wa kuisimulia kwa kuiweka kwenye kitabu au filamu basi vitu hivyo vitapata soko kubwa kutokana na mikasa iliyopo ndani yake.

Leo nataka niwasimulie kisa kimoja ambacho kwa mzazi yeyote makini ni lazima atakua/atazidisha umakini kwa mtoto wake baada ya kusoma kisa hiki. Kisa hiki si cha kufikirika bali kilinitokea mimi mwenyewe nikiwa katika umri wa kubalehe.

Kwa sehemu kubwa ya maisha yangu nimeishi kijijini mpaka pale nilipoamua kukimbilia huku jijini miaka ya hivi karibuni kwa sababu ambazo mpaka sasa sizikumbuki, ndio kusema hazikua za maana sana!

Kijiji nilichotoka sio kijijini saaana kama vile vijiji ambavyo mkisikia gari linakuja basi mnakimbilia ndani. Kwetu ni kijiji ambacho kina huduma zote za muhimu kama maji, zahanati, shule ya msingi/sekondari, barabara japo sio ya lami, umeme na kizuri zaidi reli ya tazara imepita na kuna stesheni pale kijijini.
Nyumbani kwetu kuna nyumba mbili, kuna kubwa kabisa na nyingine ndogo ya kizamani ina vyumba vinne na sebule ya wastani.

Katika nyumba kubwa alikua anaishi mzee na wapangaji kidogo, wakati mimi na mdogo wangu (wa kiume) tulikua tunaishi kwenye nyumba ndogo tukilala kwenye chumba kimoja na vyumba vingine pia vilikua na wapangaji.

Nidokeze tu ya kwamba mimi ni kijana niliyelelewa kwenye maadili mema. Baba mwalimu mama mwalimu, na mnajua walimu wa kizamani walivyokua wakali. Yale maisha waliokua wanaishi wanafunzi kwa muda ambao wapo shule sisi tulikua tunayaishi kila siku. Adabu juu[emoji1] [emoji1]
Kwa muktadha huo hapo juu utapata picha jinsi nilivyokua na tabia njema hali iliyopelekea watu wengi kunipenda hasa kina mama ambao mara nyingi walinituma nami sikusita kufanya kazi zao au kwenda mahali nilipotumwa.

Siku moja alikuja mgeni (mdada) wa mpangaji ambae alikua anakaa kwenye ile nyumba ndogo. Sasa kutokana na ufinyu wa nafasi ukizingatia yule mpangaji alikua na chumba kimoja ikabidi yule mgeni awe analala sebuleni ambako hata hivyo hapakua na viti zaidi ya ndoo za maji.

Mgeni huyu alikua ni mwanamke wa umri wa kati, kwa kukadiria kama miaka 25/28 hivi. Siku anakuja alikua amebeba mkoba mkubwa ambapo baadae tulikuja kuambiwa kuwa huko alikotoka amegombana na mumewe hivyo amekuja pale (kwa shangazi yake) kutuliza kichwa kidogo kabla hajatafuta uelekeo maalumu. Alikua ni mdada anaejipenda na siku ya kwanza kumuona alikua amesuka rasta, alivutia!

Mgeni huyu alinipenda sana. Alipenda kukaa karibu nami, akinituma nikirudi ni lazima anishukuru kwa kunipa pesa na kilichokua kinanifurahisha zaid ni tabia yake ya kupenda kuninunulia soda. Ukaribu ukazidi na wazazi (baba) hakuonekana kutilia shaka hali ya yule mwanamke kujiweka karibu sana na mimi. Kipindi hicho nilikua na miaka 15, ndio kusema nilishabalehe.

Siku moja huyu mgeni aliniambia nisile sana nyumbani kwani kuna chakula kizuri ataniletea, kweli ilipofika usiku akaja na chips akaniita ili tule wote. Sikuvunga! Tulikula baadae tukawa tunaongea tukiwa wawili nje kwenye mkeka, ndipo akanitamkia kuwa anajisikia kuwa na mwanaume na kama naweza ataweza kunipa siku ile.

Nikashanga lakini sikukataa. Nikakubali bila kikwazo huku nikiomba muda uende watu walale. Nikajisemea moyoni "ngoja nami nionje"! Kwa sababu alikua analala sebuleni akaniambia nikalale mpaka muda nitakaohisi watu wengi wamelala basi nitoke kwa kunyata nimguse ili tutoke kwenda chooni (nje) akanipe.

Ajabu ikaanzia hapa! Ingawa nilikua nimepania sana kuonja lakini nikajikuta nimelala sana siku ile, lakini nilishtuka kukiwa bado na giza nje. Nikanyata mpaka sebuleni, ile namgusa tu nikasikia bibi (shangazi yake) ambaye alikua anapika na kuuza vitumbua hapo nyumbani nae anafungua mlango, nikazuga naenda uwani, na kuanzia muda huo pilika za bibi hazikuisha mpaka kunakucha. Kumbe ndio ilikua pona yangu.

Kesho yake narudi kutoka shule nakuta kikao, kumbe mume wake alikuja. Wakayaongea wakapata muafaka na wakaondoka wote usiku wa siku ile ile.

Baada ya muda kidogo zikaanza kusikika habari kuwa yule dada na mumewe ni waathirika, mwanzo ilikua kama tetesi tu lkn kumbe afya zao pia zilianza kutetereka na siku nilipomuona tena yule mwanamke nilishangaa. Hivi ninavyoongea wote yeye na mumewe tayari ni marehemu.

Ukiwa kama mzazi/mlezi, usiache kisa hiki kipite hivi hivi... Kama ulikua na tabia ya kuacha mwanao akizoeana sana na watu hasa waliomzidi umri basi shtuka sasa. Baadhi ya watu si wazuri kwa mwanao. Sio vizuri kumshuku kila mtu kwa mabaya lkn pia sio vizuri kumpa mtu uhuru mkubwa wa kuwa na mwanao. Kuna tabia za baadhi ya wazazi kuwachunga sana watoto wa kike na kuwaacha huru wale wa kiume. Tabia hii pia inaweza kutugharimu.
Tuwachunge watoto.
 
Hhaaaa ukimwi ni conspiracy theory

Hakuna ukimwi ila ni kutokana na unavyoamini ya kwamba kuna ukimwi
 
Ukimwi hauambukizi kirahisi hivyo kwa bao la fasta fasta,tungekuwa tumeisha wote,unadhani we hujawahi kugonga nwanamke muathirika?
 
Endelea kujidanganya kuwa Ukimwi ni Jambo la kufikirika siku ukiupata ndio utaelewa uhalisia,jamani wanajamvi Ukimwi upo na unaua.
 
Mimi pia ilibaki kidogo.

Miaka hiyo usiku mmoja nilienda kulala kwa bibi. Kwa bibi ni mjini na bibi alikua mtumishi serikalini custom uko moja ya mipaka ya nchini. Karibu na bibi kuna binti jiran pua na mdomo tulikua na mazoea. Usiku huo bibi yupo jikoni (jiko la nje) anapika binti akaja akakaribishwa vizuri ni kawaida tu, akaja ndani hadithi kadhaa hapo mchakato ukataka kuanza. Dah.! binti akaitwa kwao mie nalalamika tu moyoni na sikua nimewahi kuonja. Haikutokea ile fursa tena.

Kumbe nilipaswa kusema ahsante MUNGU, Yule binti alikua muathirika toka kuzaliwa, na hivi sasa ni marehemu miaka tisa.
 
Mwaka 2000 tulitembelewa na family friend akiwa na watoto wanne, wawili wa kwake na wawili wa dada zake. Wakati wazee wanapata bia sisi watoto tukawa tunacheza room kwetu. Home tulikuwa wavulana tu na yule mama mgeni alikuja na mabinti tu.

Tuligawana kila mtu na wa kwake mi nikampata first born wa yule mama. Ilibaki kidogo nimchakate na vile nilikuwa sina uzoefu nahisi ningeambukizwa ngoma. Yule mama alifariki mwaka huo na binti yake alifariki 2001. Binti mdogo yupo mpaka leo aliolewa na hana maambukizi.
 
Back
Top Bottom