Nilipoteza mapenzi ya kweli kisa Familia

Nilipoteza mapenzi ya kweli kisa Familia

Kizoda

Senior Member
Joined
Mar 5, 2022
Posts
130
Reaction score
302
Maisha haya bwana magumu saana.

Nilikuwa na mwanamke wangu mzuri ambaye nilipendana naye saana. Huyo mwanamke alikuwa msaada mkubwa saana kwangu. Alikuwa ni mtu mwenye akili ya kufikiria mafanikio saana alikuwa hawezi kufanya kitu bila kunishirikisha.

Na kuna siku kabisa nilimwambia nina plan ya kuanzisha biashara ya nguo za watoto. Nilikuwa sina mtaji kabisa akanipa wazo la kununuwa watoto wa mbuzi wa 4 alafu tunawakuza wale watoto wa mbuzi mwaka kesho tunauza kila mbuzi laki moja au Chini ya laki moja kitu ambacho tulikuja kufanikiwa nikapata mtaji uo, Pamoja na mazuri hayo.

Familia yangu walikuwa wanamchukia huyo sister saana hawakutaka mimi niwe naye kabla yangu huyo mtoto wakike haliwai kuwa kwenye mausiano na wanaume tofauti na kibaya zaidi kila mausiano yake yalikuwa yanatambulika saana kijijini kwetu kisa hali yake ya kupenda usupar star tena wanaume mabishoo ndo alikuwa anatembea nao saana wakamchukulia ni malaya sasa habari hizo Familia yangu walizipata wakawa wanamuandama mtoto wakike eti hawamtaki asijekuniambukiza magonjwa. Nilijaribu kutetea mtoto wakike ilishindikana. Mwishowe tukaachana.

Sasa tulivyo achana naye sasa hivi aliolewa na mwanaume mwingine kizuri zaidi maisha yao yako Good saana wana biashara yao
Na kibaya zaidi ni mjamzito. Mimi huku mambo yangu yanazidi kuaribika na nilipata mwanamke ambaye ni chawivu yaani mwanamke ana wivu saana yaani kila siku ni ugomvi tu.

Saa zingine Familia zinatuaribia saana.
 
Nimesoma nikagundua yafuatayo:-

1• Wewe ni mwanaume unae fungamanisha maisha yako binafsi na familia yenu/watu wengine.
2• Hauna uwezo wa kufanya jambo kubwa pasipo kuiuliza ama kuishirikisha familia yako/watu.
3• Hauna uwezo wa kufanya maamuzi na kujisimamia kama baba wa familia.
4• Unapenda kusikiliza watu wengine/umbea.

Mwisho nikukumbushe kwamba hakuna mwanamke ambae anaweza akakubali ama kudumu kwenye ndoa ambayo mwanaume hwategemea watu wengine ama kwao kumfanyia maamuzi.

Alafu...... situlisha kubaliana hapa ndani kwamba wanaume tusioe..🤔
 
Dedication; wimbo wa tuonane paradiso...

Mwambie ana bahati sana ungekuwa ushamchosha kapauka kama ugoko wa mponda mawe
 
Wewe ni aina ya wanaume wa ovyo sana

Huna msimamo na maamuzi yako

Ungekuwa karibu ningekuzaba hata makofi

Sent from my Nokia 2.4 using JamiiForums mobile app
Bro nijaribu kutetea penzi nilishindwa tukaingia kwenye ugomvi mkubwa mimi na mwanamke na kilicho muondosha mwanamke alikibia eti Familia yangu wasijekutowa roho yake
 
Bro nijaribu kutetea penzi nilishindwa tukaingia kwenye ugomvi mkubwa mimi na mwanamke na kilicho muondosha mwanamke alikibia eti Familia yangu wasijekutowa roho yake
Huna msimamo kijana ungeonyesha msimamo tangu mwanzo hamna mwanafamilia angekubabaisha
 
Huenda familia yako walikushauri vema, wala usijutie sana!

Songa mbele !

Halafu usione kwa nje watu ukazani wana maisha mazuri huwezi jua kwa ndani wanapitia changamoto au matatizo gani!

Zungumza na huyo mkeo Mwambie akue a punguza wivu wa kijinga!
 
Katika vitu ambavyo huwa ninamsimamo navyo ni uchumi wangu, future yangu, afya na mahusiano yangu

Aisee ogopa sana kufanyiwa maamuzi
Kuna watu huwa wanajiona miungu watu wanajua kitakachotokea
 
Maisha haya bwana magumu saana

Nilikuwa na mwanamke wangu mzuri ambaye nilipendana naye saana
Huyo mwanamke alikuwa msaada mkubwa saana kwangu

Alikuwa ni mtu mwenye akili ya kufikiria mafanikio saana alikuwa hawezi kufanya kitu bila kunishirikisha

Na kuna siku kabisa nilimwambia nina plan ya kuanzisha biashara ya nguo za watoto
Nilikuwa sina mtaji kabisa akanipa wazo la kununuwa watoto wa mbuzi wa 4 alafu tunawakuza wale watoto wa mbuzi mwaka kesho tunauza kila mbuzi laki moja au Chini ya laki moja kitu ambacho tulikuja kufanikiwa nikapata mtaji uo
Pamoja na mazuri hayo

Familia yangu walikuwa wanamchukia huyo sister saana hawakutaka mimi niwe naye kabla yangu huyo mtoto wakike haliwai kuwa kwenye mausiano na wanaume tofauti na kibaya zaidi kila mausiano yake yalikuwa yanatambulika saana kijijini kwetu kisa hali yake ya kupenda usupar star tena wanaume mabishoo ndo alikuwa anatembea nao saana wakamchukulia ni malaya sasa habari hizo Familia yangu walizipata wakawa wanamuandama mtoto wakike eti hawamtaki asijekuniambukiza magonjwa
Nilijaribu kutetea mtoto wakike ilishindikana
Mwishowe tukaachana

Sasa tulivyo achana naye sasa hivi aliolewa na mwanaume mwingine kizuri zaidi maisha yao yako Good saana wana biashara yao
Na kibaya zaidi ni mjamzito
Mimi uku mambo yangu yanazidi kuaribika na nilipata mwanamke ambaye ni chawivu yaani mwanamke ana wivu saana yaani kila siku ni ugomvi tu
Saa zingine Familia zinatuaribia saana
[emoji3516]
MKUU,
KAMA KATIKA WALE WATOTO WA MBUZI MLIOKUWA MNAFUGA AMEBAKIA ANGALAU MMOJA,
NICHECK TUFANYE BIASHARA.
 
Mtafute Chausiku au Mwadawa hapo kijijini hao mabinti hua wametulia sana uoe muishi.
 
Back
Top Bottom