Mwamuzi wa Tanzania
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 15,486
- 45,256
Ni kama mwezi sasa au wiki kadhaa tangu benki kuu ya Tanzania itoe waraka wa kuwataka wakopeshaji wa mitandaoni wanaolalamikiwa kufuata taratibu ikiwa pamoja na kuacha lugha za matusi, kutokusumbua ndugu na jamaa wa mkopaji, kutokusambaza taarifa za mkopaji.
Mimi nilisema hakuna hata kimoja hawa watu watakifuata. Nilijibu waraka wao kwa njia ya maswali yafuatayo;
1. Je, ni BOT ndiyo iliwapa ruhusa kukopesha watu mikopo ya siku 4 mpaka 6 kwa riba ya 40%-50%.
2. Je, ni BOT ndiyo iliwapa ruhusa ya kukusanya namba za phone book ya mteja?
3. Je, ni BOT ndiyo iliwapa ruhusa ya kusumbua mteja na kumdhalilisha katika jamii huyo mkopaji akipitiliza hata siku moja?
Kama waliweza kufanya hayo yote na mengine ambayo ni kinyume cha kanuni na Sheria na hawajachukuliwa hatua je, watautii waraka wa BOT ambao ni toothless?
Umaskini ndio unawafanya Watanzania wawe shamba la bibi. Na viongozi wanapewa Senti na mabepari mchezo unaisha.
Mkopo kwenye fomu unaambiwa ni wiki 2 ukiclick tu kukubali wanaanza kwanza kukukata makato ya hovyo, pia siku ya 4 tu au ya 3 simu zinafuata usipolipa tu umekwisha. Utaundiwa group Whatsapp la kukutukana, kijiji chote kitajulishwa n.k
Soma Pia: BoT yakataza rasmi kampuni za mikopo mitandaoni kuchukua mawasiliano ya wateja ili kuwadhalilisha. Yatoa mwongozo mpya!
Serikali iwakomboe Wananchi. Wana hali ngumu sana. Jana nimepigiwa simu kuna mtu anadaiwa nikamuuliza Mimi kama ni mdhamini wake mbona sijajulishwa kabla hajakopeshwa akasema Mimi sio mdhamini. Sasa kwanini nipigiwe simu kama sio mdhamini jibu analonipa ni upumbavu mtupu.