Nilishindwa kumsaidia mlevi nikidhani ni jambazi

MtotoKautaka

JF-Expert Member
Joined
Jul 16, 2018
Posts
373
Reaction score
895
Nilikuwa bado mgeni Wiliya flani mwaka 2022 mkoa x huko kaskazini.

Nilipanga mitaa flani pembeni mwa mji, kumetulia karibu na kijito flani cha mchongo kilikuwa kinatiririsha maji na pembeni wagagaa na upwa walikuwa wanatafuta wali nyama kwa kujishughuliaha na kilimo cha mbogamboga.

Baada ya kuzoea zoea nikaanza kuwa naenda viwanja narudi late home.

Sikuwa namuda mzuri wa kufahamiana na majirani kwasababu ya ubize hivyo nilibahatika kufahamiana na majirani wachache sana.

Siku moja natoka viwanja mida ya saa5 usiku boda kanishusha main road nikaanza kuishika chocho ya magetoni.

Kama mita 50 kutoka main road nakutana na mlevi anayumba yumba huku analia, kummulika nikaona katapakaa damu hasa upande wa nyuma mgongonj kwa chini.

Jamaa akaanza kuniomba nimsaidie nikamuliza shida nini hasemi anasema tu nisaidie napo anasema kwa tabu.

Akajikaza akafunua shirt alokuwa ameivaa, alivofunua niliona jeraha kubwa kiasi Kwa muonekano alijeruhiwa kwa kisu kwasababu jeraha lilikuwa kubwa kuelekea ndani ni kama alichomwa kisu.

Damu ilikuwa nyingi sana, ananambia nimsaidie, usiku, simjui, sijui kimemkutq kipi mpka kachomwa kisu, vipi kama walomdhuru walikuwa wanaendelea kumfatilia nyuma wangenikuta naye pale ningedhurika namimi bila shaka, groves sina nashikaje dam bila groves what if tutaambukizana magonjwa.

Hizi sababu zilinifanya niishie kumvua shirt yake nikamfunga kwa umakini sana sehemu ya jeraha kuzunguka juu ya kiuno Ili kupunguza kasi ya kutoka kwa dam.

Nilimuliza kwake ni wapi, kanielekeza hakukuwa mbali sana na pale basi nikakimbia kuita watu pale kwake, ila kabla ya kuwaita nikawaza what if wakidhani mimi ndo niliyemdhuru na ukizingatia bado mgeni pale mtaani.

Sikujiuliza sana nikasema liwalo nitapambana, basi nikagonga akatoka mmama mmoja na chalii wa kiume nikamambia kuwa kuna mtu amelewa lakini anaonekana kajeruhiwa na amesema kwake ni hapa, wakasema atakuwa flani tushamkataza pombe kwasababu akilewa anaanza kupigana na anatongoza wake za watu.

Walionyesha kujivutavuta nikawambia jeraha ni kubwa anaweza kufa, wakasema ah atakoma si tushachoka. Nafikiri walikuwa wanajivuta kwasabab hawakujua uzito wa kilichomkuta ndugu yao.

Nasema hivi kwasababu ya reaction waliyoonyesha baada ya kufika na kumuona hali alokuwa nayo.

Tulipofika alipokuwa jamaa tulimkuta hawez kujigeuza anaongea kwa tabu sana, yule mama akaanza kuhamaki anamuita jina lake mixer mdogo wangu nikajua ni mdogo wake.

Alipiga simu Kwa dereva bajaj alikuwa anakaa jirani tu na pale kwao uzuri jamaa alikuwa active bas akaja tukampakiza njia moja hospital, nikawaza hawa hospital bilq kupitia polisi watapokelewa? Sikuhoji nikawaacha.

Mimi sikwenda nao hospital, kesho yake naskia jamaa kavuta kuna msiba mtaani kwetu basi tukazika yakaisha.

MyTake. Walevi leweni lakini muwe na mipaka, leweni kistaarabu.
 
Umesema mwanzo uliogopa kwa sababu hukuwa na gloves je baada ya kuwafata ndg zake gloves ulipata wapi?
Mara nyingine okoa tu mtu kadiri uwezavyo yatakayojiri ni matokeo ila umeokoa uhai wa mtu tiyari.

Siku ukifanya kazi machimboni ndo utaelewa haya mkuu. Niliwahi toa msaada na msaada ule kugeuka baraka sana.Mchimbaji alipigwa manusura afe natoka machimboni nakutaka katapakaa damu mwili wote na haongei hata ishara tu anatoa kwa shida.

Sikuwa na namna nyingine nikampiga picha kama nne hapo ni saa7 hivi na nilikuwa natoka machimboni kwenda mjini niko na pikipiki tu. nimekaa nawaza kama dk10 nikijua labda kuna mtu atapita jamaa anaendea kutoa ishara hata sielewi ana maanisha nini.

Kumshika nikagundua mguu mmojaa umevunjika nikapiga simu kwa wana chimboni napo mbali hadi wafike kama dk20. Nikambeba nikamkalisha kwenye pikipiki hadi kwenye dispenasary moja hivi wakta kumkataa nikawaambia jamani toeni msaada hata wa awali ukizingatia saivi usiku na haongei wakakataa kabisa nikampigia bro ambae kipindi hicho alikuwa diwani nikamweleza akasema wape simu na akasema atalibeba yeye nikawa nae hadi asbh muda hatujui ndg zake na bro akaja na gari tukambeba hadi hospital akapatiw matibabu by saa9 ndo akaanza kuongea.

anaongea neno moja analiaa balaa anasema mdogo wangu kama sio wewe ningekuwa nimekufa analiaa sana mara anasema wewe ni malaika analiaa hadi kuwataja ndg zake tukawapigia simu wakaja wakaendelea na majukumu mengine nami nikawa naenda kumcheki. alipigwa sana akidai alimdhurum mchimbaji mwenzie na walijua amekata moto wakamtupa karib na mfereji.

Jamaa alikuwa na kiwanja alinipa baada ya kupata nafuu maana mguu ulikuwa umevunjika mara2 alichelewa sana kupona mguu. Akanipa akaniambia usije kukiuza iwe kumbukumbu kuwa ulinisaidia. Ila shida mbaya sana niliuza
 
Hongera
 
Nilikuwa bado mgeni Wiliya flani mwaka 2022 mkoa x huko kaskazini.

Nilipanga mitaa flani pembeni mwa mji, kumetulia karibu na kijito flani cha mchongo kilikuwa kinatiririsha maji na pembeni wagagaa na upwa walikuwa wanatafuta wali nyama kwa kujishughuliaha na kilimo cha mbogamboga.

Baada ya kuzoea zoea nikaanza kuwa naenda viwanja narudi late home.

Sikuwa namuda mzuri wa kufahamiana na majirani kwasababu ya ubize hivyo nilibahatika kufahamiana na majirani wachache sana.

Siku moja natoka viwanja mida ya saa5 usiku boda kanishusha main road nikaanza kuishika chocho ya magetoni.

Kama mita 50 kutoka main road nakutana na mlevi anayumba yumba huku analia, kummulika nikaona katapakaa damu hasa upande wa nyuma mgongonj kwa chini.

Jamaa akaanza kuniomba nimsaidie nikamuliza shida nini hasemi anasema tu nisaidie napo anasema kwa tabu.

Akajikaza akafunua shirt alokuwa ameivaa, alivofunua niliona jeraha kubwa kiasi Kwa muonekano alijeruhiwa kwa kisu kwasababu jeraha lilikuwa kubwa kuelekea ndani ni kama alichomwa kisu.

Damu ilikuwa nyingi sana, ananambia nimsaidie, usiku, simjui, sijui kimemkutq kipi mpka kachomwa kisu, vipi kama walomdhuru walikuwa wanaendelea kumfatilia nyuma wangenikuta naye pale ningedhurika namimi bila shaka, groves sina nashikaje dam bila groves what if tutaambukizana magonjwa.

Hizi sababu zilinifanya niishie kumvua shirt yake nikamfunga kwa umakini sana sehemu ya jeraha kuzunguka juu ya kiuno Ili kupunguza kasi ya kutoka kwa dam.

Nilimuliza kwake ni wapi, kanielekeza hakukuwa mbali sana na pale basi nikakimbia kuita watu pale kwake, ila kabla ya kuwaita nikawaza what if wakidhani mimi ndo niliyemdhuru na ukizingatia bado mgeni pale mtaani.

Sikujiuliza sana nikasema liwalo nitapambana, basi nikagonga akatoka mmama mmoja na chalii wa kiume nikamambia kuwa kuna mtu amelewa lakini anaonekana kajeruhiwa na amesema kwake ni hapa, wakasema atakuwa flani tushamkataza pombe kwasababu akilewa anaanza kupigana na anatongoza wake za watu.

Walionyesha kujivutavuta nikawambia jeraha ni kubwa anaweza kufa, wakasema ah atakoma si tushachoka. Nafikiri walikuwa wanajivuta kwasabab hawakujua uzito wa kilichomkuta ndugu yao.

Nasema hivi kwasababu ya reaction waliyoonyesha baada ya kufika na kumuona hali alokuwa nayo.

Tulipofika alipokuwa jamaa tulimkuta hawez kujigeuza anaongea kwa tabu sana, yule mama akaanza kuhamaki anamuita jina lake mixer mdogo wangu nikajua ni mdogo wake.

Alipiga simu Kwa dereva bajaj alikuwa anakaa jirani tu na pale kwao uzuri jamaa alikuwa active bas akaja tukampakiza njia moja hospital, nikawaza hawa hospital bilq kupitia polisi watapokelewa? Sikuhoji nikawaacha.

Mimi sikwenda nao hospital, kesho yake naskia jamaa kavuta kuna msiba mtaani kwetu basi tukazika yakaisha.

MyTake. Walevi leweni lakini muwe na mipaka, leweni kistaarabu.
Kuzunguka kote kumbe unatafuta angle ya kutunanga ?

Mbona hata ungefungua uzi ukasema walevi muwe mnalewa kistaarabu alafu ukaacha bado tungesoma na tungekuelewa vizuri kuliko kuanza stori za kuogopesha namna hii
 
Back
Top Bottom