Nilisomesha mchumba

Tamu3

Member
Joined
Feb 17, 2023
Posts
28
Reaction score
18
Mezaliwa kijijini, kukulia huko pia,
Mazao yetu shambani, mengi tulijivunia,
Tukayajaza ghalani, akiba kijiwekea,
Tukawa wenye furaha, usiku tumevimbiwa.

Nilimaliza la saba, nikarudi kijijini,
Nikafaulu si haba, wa taifa mtihani,
Nikamuambia baba, nae akafurahini,
Usiku sikuulala, naiona sekondari.

Baadae wiki mbili, wazazi walipotea,
Walikufa kwa ajali, ya Mtumbwi huko Mafia,
Kwa sauti yangu kali, wazazi liwalilia,
Uyatima ukabisha, lipaswa kuupokea.

Mawazo ya sekondari, yakaanza kupotea,
Kwa hiyo nikaghairi, nilishindwa kulipia,
Ada ilikuwa shari, enzi zetu najutia,
Nikabaki kijijini, nikilima na kufuga.

Myaka michache kupita, kuoa nikatamani,
Binti mzuri Anita, akanikonga moyoni,
Kumwambia sikusita, yote nikamwelezeni,
Nashukuru likubali, ila kwa sharti moja.

Nimpeleke chuoni, ujuzi kaongezeni,
Nikakubali jamani, kaenda huko chuoni,
Kwa bidii lisomeni, uhasibu hiyo fani,
Ada nikamlipia, na mahitaji mengine.

Karibia kumaliza, akiwa bado chuoni,
Ujumbe akanijuza, hanitaki nimwacheni,
Hakika aliniliza, nikajawa na huzuni,
Akadai sina hadhi, nimuache ana wake.

Nilihisi ninaota, nikiwa usingizini,
Wiki tatu Zilipita, akaivunja laini,
Sikuweza kumpata, hapatikani hewani,
Ninajuta kusomesha, Anita ananiuma.

Niliuza kila kitu, mwenzangu ende chuoni,
Liuza hadi viatu, jawabu lake huzuni,
Sitomsamehe katu, Jambo alonifanyeni,
Wachumba sisomesheni, wengi hawana fadhila.

Denny Jeremias Kitumbika
Mtunzi wa mashairi na ngano za Kiafrika
Mufindi Tanzania 2/3/2022

 
Tajiri akili yake ipo kwenye kubana matumizi maskini yeye yupo kwenye kufanya matumizi. Halafu maskini anauliza kwanini sifanikiwi kimaisha au nimerogwa 🤣🤣

Inakuwaje umsomeshe mwanamke si mkeo tena hujazaa nae?.
 
Hilo ni shairi wakuu sio reality
 
Sijasoma hilo shairi ila ukipata producer na video director mzuri lazima diamond aite maji mma
 
Tajiri akili yake ipo kwenye kubana matumizi maskini yeye yupo kwenye kufanya matumizi. Halafu maskini anauliza kwanini sifanikiwi kimaisha au nimerogwa [emoji1787][emoji1787]

Inakuwaje umsomeshe mwanamke si mkeo tena hujazaa nae?.
Acha janjajanja soma hadi mwisho
 
Tajiri akili yake ipo kwenye kubana matumizi maskini yeye yupo kwenye kufanya matumizi. Halafu maskini anauliza kwanini sifanikiwi kimaisha au nimerogwa 🤣🤣

Inakuwaje umsomeshe mwanamke si mkeo tena hujazaa nae?.
tajiri anabanaje matumizi, huyo siyo tajiri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…