Ngongo
Platinum Member
- Sep 20, 2008
- 20,654
- 35,887
Heshima sana wanajamvi,
Kila mwanajamvi alijua msimamo wangu sina haja ya kuendeleza ligi uchaguzi umekwisha Lissu na Heche ni washindi.
Nawapongeza Lissu na Team yake ya kampeni kwa kazi kubwa sana.
Nilitaka uongozi wa Mbowe uendele lakini wenye chama waliona ni vyema wakabadilisha uongozi pengine kule kukaa sana kulichangia au hoja za washindani wake ziliwafanya wajumbe waone umuhimu wa kubadilisha uongozi.
Baada ya matokeo ya uchaguzi nilisikitika lakini ghafla najikuta nafurahi tena kwanini nafurahi ?.
Wakati mwingine unaweza kumlaumu mtu kwa mambo yote mabaya bila sababu au hoja za msingi.
Najua mwamba alilaumiwa sana kwa matokeo ya chaguzi zilizopita 2019,2020 na 2024 kwamba ni kiongozi legelege anashirikiana na CCM kuhujumu CDM na nk.
Wengi wetu tuliamini Uchaguzi wa 2019 & 2020 ilikuwa mipango michafu na dhulma ya MWENDAZAKE. Sote tuliamini KUTEKANA &KUTOANA UHAI ilikuwa mipango michafu ya MWENDAZAKE na pengine Mbowe na VIONGOZI wenzake waliamini zile siasa chafu zimekwisha.
Lema & LISSU waliokimbilia ughaibu walirejea nyumbani maana yake walijua nyumbani kumenoga siasa za kutishana,kuuana,kupotezana ZIMEKWISHA.
Uchaguzi wa 2024 umebainisha wazi siasa za wizi wa kura,kuvuruga uchaguzi na mambo mengi machafu hazikuwa siasa za MWENDAZAKE pekee yake bali zilikuwa siasa za mfumo mzima wa watawala. Kupotea kwa viongozi na wanachama wa CDM ni jibu tosha kwamba bado nchi ipo kule kule katika zama za giza.
Bahati mbaya MBOWE kabeba msalaba wote wa uovu wa watawala.Hili lilikuwa wazi kabisa katika kampeni za TEAM LISSU. Kuna wakati walionyesha wazi kabisa hata kupotezwa baadhi ya wanachama MBOWE alihusika au alijua mfano Mzee AlLY Kibao (siasa chafu)
Kwakuwa uchaguzi umekwisha na TEAM LISSU kuibuka washindi ni matarajio yetu kwamba mwelekeo mpya wa chama utaonekana katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika miezi michache kutokea sasa.
Lakini suala kubwa zaidi ni zile propaganda kwamba CDM ni chama cha WACHAGGA zitakuwa zimekwisha kabisa.
NO REFORM NO ELECTION.
Ngongo kwasasa Idodomya.