Nilitaka nifungue akaunti ya Albarakah CRDB lakini nikasita

Nilitaka nifungue akaunti ya Albarakah CRDB lakini nikasita

Webabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2010
Posts
8,870
Reaction score
14,258
Benki zinazozikubali huduma za kibenki kwa mfumo wa kiislamu zinaongezeka kila siku kutokana na faida zake za uhakika.

Moja ya benki iliyoamua kuanzisha huduma hizo kwa Tanzania ni benki ya CRDB chini ya jina la Albarakah.

Juzi moja nilipokwenda kupata huduma mmoja ya wafanyakazi wake akanipatia kipeperushi kwa njia ya kunishawishi kwa kujua kuwa mimi ni muislamu na mtumiaji wa benki hiyo kwa huduma nyenginezo,
Nilipokisoma kipeperushi chao nikaona kuna ujanja mwingi katika kuikubali kwao huduma hii ambayo inatoa hdumua za halali na kwa kufuata sharia.

Wamezunguka huku na huku lakini wameshindw kutaja akaunti hizo zitakuwa zikitoa mikopo na huduma zinazoambatana nazo kwa kufuata misingi ya uislamu.
Wamesema ni huduma halali.

Uhalali bila kusema ni kwa misingi ya kiislamu hauwi uhalali kwani hata wanywa pombe wanasema ni halali lakini si halali ya kweli kwa misingi hiyo.

Iwapo kwenye tangazo tu wamefanya ubabaishaji namna hiyo basi na kwenye hizo huduma zenyewe kutakuwa na udanganyifu sana.

Mikopo inaweza ikatolewa kwa wauza baa na ikaitwa ni mikopo halali.

Hao wataalamu wao wanaosimamia hizo huduma za kisharia yawezekana wametafuta Masheikh ubwabwa na hawakushughulika kutafuta wataalamu wa fani hizo na wakweli ambao wamejaa.
 
Amana bank ndiyo suluhisho
Yawezekana hivyo kwani hata ukipata kwenye matawi yao nje imeandikwa wazi ni Islamic benki.

Tatizo nimewahi kusikia kuna sehemu wanapwaya sana.

Wana uzembe sana kwenye masuala ya huduma za mtandao.
 
Back
Top Bottom