Watu mlio karibu na rais Samia msijisahau sana na wala msione mmepata na hivyo kuamua kupuuza uundwaji wa katiba mpya.
Tunataka katiba itakayompunguzia rais mamlaka na itakayoweka mipaka ya uongozi wake. Lkn cha muhimu zaidi rais awajibishwe pale atakapobainika kakosea.
Katiba hii ni mbovu, inampa rais mamlaka yote halafu hawajibiki kwa lolote. Tuliona jinsi JPM alivyoitumia hii katiba kunyanyasa viongozi wastaafu, viongozi wenzake ndani ya chama, wapinzani, viongozi wa dini na hata viongozi wa chama chake.
JPM hakuishia hapo, alibinya waziwazi haki za watumishi wa umma, wafanyabiashara na wakulima. Alikuwa akisema amesema hakuna wa kudhibiti maagizo na amri zake. Nchi haiendeshwi namna hii.
Nafahamu waliopo mamlakani hivi sasa wanaona wamepata na huwaambii kitu. Katiba hii mbovu wanayoona inawabeba hivi sasa itawatesa siku zijazo. Nape, mzee Makamba, Kinana, Kikwete na January Makamba bado wana kumbukumbu juu ya mateso waliioyapata awamu ya 5.
Leo kwako kesho kwa mwenzio (kanuni ya Karma).