Nilitegemea Upigaji faulo wa Aziz K uwe somo kwa makocha, makipa na wachambuzi

bryan2

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2016
Posts
3,323
Reaction score
4,679
Ndio ni Azik K kati ya mafundi wanaoimbwa sana nchini mwetu kutokana uchezaji wake na kubwa zaidi aina yake ya upigaji wa Faulo.

Idadi ya makipa walioteswa na Aziz K ni wengi kwa kifupi kuna.

Aisha Manula-Simba
Ahmada-Azam
Nahimana-Namungo
Shekimweri-Mtibwa
Majock majock-Zalan
Kipa wa Club de Tunis-Tunisia
Farouk Shikalo-Mtibwa na bado kuna wengine watazidi kuteswa

Nlitegemea upigaji wa Mapigo huru wa Aziz K kuwa case study kwa makocha hasa wa makipa, wachambuzi wa mpira pamoja na makipa wenyewe either kwa kuzielezea kitaalamu na pia kuwafundisha makipa wao jinsi ya kudili nazo.

Makocha kama Juma Kaseja, Juma Pondamali...nk wana uzoefu mkubwa wa kucheza kama makipa na ukocha wenyewe watu kama hawa nlitegemea waeleze kitaalamu nini siri ya upigaji ule.

Ila Ajabu tumewaachia hawa wachambuzi uchwara wa kibongo badala ya kuja na majibu wamekalia propaganda na kusema makipa wanaachia makusudi bila kuja na suluhisho, wakumbuke wakitaja makipa hata kipa wa timu yao pendwa Manula keshakutana na kiama hicho.

Tunakumbuka Upigaji wa free kick wa David Beckham alivyokua anawatesa makipa ila sikuwahi kusikia kauli za kubeza kutoka kwa watu wenye kujua mpira nzuri zaidi makocha waliwaeleza makipa wao kuongeza umakini zaidi.

Kibongo Sidhani hata kama kuna kocha wa makipa yeyote kawahi kurudia kuangalia upigaji wa Free kick wa Aziz K na kuwafundisha makipa wao jinsi ya kupambana nazo

Ubaya nao wamebaki kwenye propaganda za wachambuzi fyeki wa kibongo.

Vile vitu Aziz anaanzia kuvifanya mazoezini kuna siri moja ningeandika hapa ila sio kocha nawaachia hiyo H/work makocha na wachambuzi wa Kibongo.

Mkichukulia poa free kick zile makipa wenu watateswa sana.
 
Hakika ujinga wa uzeen lazma utakufa nao tu pole sana
 
Ile ya mtibwa hapana.Mke wangu tu angedaka.Ya manula angemuua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…