Nilitembea na ndugu yake.....

Da Pretty

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2010
Posts
3,059
Reaction score
1,152
Habari,
Hivi karibuni nimeingia kwenye uhusiano mpya na kijana ambaye ninahisi ananipenda kweli.
Tunakaribia mwezi wa pili katika uhusiano sasa, ni mvumilivu na hana haraka na mwili wangu.
Ni rafiki mzuri na amenitambulisha kwa rafiki na ndugu zake wengi maana karibu kila weekend nakutana na watu wapya.
Kilichotokea jana kanitambulisha ndugu yake ambaye nilimbana sana kujua undugu wao akaniambia bibi zao ni ndugu. Huyo kijana tunafahamiana vizuri japo tulijifanya hatujuani ni kua alikua shemeji yangu kipindi cha nyuma nimewahi kuwa na uhusiano na kaka wa huyo kijana niliyetambulishwa.

Wapendwa, nashukuru sana kwa ushauri wenu ambao kwangu nasema ni mzuri.
Nimependa mawazo yote....
Tumetoka na kijana tukapiga story zetu nyiiiingi wala hakuniharakisha niseme nilichomuitia!

Wapendwa!!
Nimejikanyaga wee lakini hatimaye nimesema,
nimetua mzigo na hapa nina mawazo!!
Ni kweli kaniuliza maswali mengi na magumu na kikubwa
kataka kujua uhusiano wangu na huyo kijana hadi sasa upoje.
Nimejieleza na nimempa sababu za kujieleza lakini cha msingi NIMEWEKA WAZI.
HAJANIBU LOLOTE KUHUSIANA NA HILO JAPO MASWALI NIMEULIZWA SANA NA NAHISI KAMA VILE ANA KINYONGO!
Kanirudisha nyumbani ila sijajua anawaza nini,
nampenda sikutaka kumkosa ila kwa hili sitajuta kwa sababu nisingeweza kufuta historia.
Ni nafasi yake kuamua na ni bora achague kuliko ningemficha ajue baadae.

 
Sioni tatizo hapo. Unless umewahi kumwambia kuwa hujawahi kuwa na uhusiano kabla sitarajii mwenzako aamini yeye ni wa kwanza kwako. Ila itasaidia ukimwambia rafiki yako ukweli kabla hajaambiwa na mtu mwingine maana version ya story inaweza kupotoshwa.
 
The sooner the better, mwambie na hii itakuwa kipimo kikubwa cha mapenzi yake kwako! Uzuri mapenzi yenu bado ni machanga.

Swali la msingi bado unafeelings kwa X wako? In case akarudi na kukuomba msamaha utareact vipi, uwezekano wa kubump into each other ni mkubwa kwa kuwa they r kinda related!
 
X nilikutana nae na ameshaoa,sina feelings zozote kwake tangu nilipoamua kua sitamtafuta tena.
Kweli, naona bora kumwambia
 
hebu mueleze ukweli mapema ili hata akija kusikia asishangae,
kama kweli anakupenda hilo haliwezi kuwatenganisha dear.
vunja ukimya ajue mapema kutoka kwako na si kusikia make
kusikia huwa inauma zaid mpendwa
 
Katika hili suala huna kosa kabisa na kama kijana ni mwelewa atakupenda zaidi. Mweleze ukweli namwachie yeye achague kumeza au kutema. Huna la kupoteza ila utaweza ku-gain mengi sana kwa kumweleza wewe kabla ya yeye kuupata ukweli kupitia wambeya.

Hebu fanya haraka sana kabla jua halijafika utosini umwambie una suala nyeti sana na kama hataweza kuonana na wewe leo utapata matatizo makubwa. Mweleze pia unavyojisikia vibaya kwa sababu hukutegemea kitu kama hicho na kwa hiyo mwombe yeye aamue la kufanya. Mweleze pia kwamba uko tayari kuupokea uamuzi wowote.

Utashangaa njema itakavyokupiga mabusu na kukueleza kuwa hilo ni jambo rahisi sana. Hata mimi ukinieleza hivyo lazima nikutoea out na kukupa bonge la dinner (a big one and inclusive)!!

Ubarikiwe sana,

Babu DC.
 
X nilikutana nae na ameshaoa,sina feelings zozote kwake tangu nilipoamua kua sitamtafuta tena.
Kweli, naona bora kumwambia

Do the needful....Hebu nyanyua simu sasa hivi na kuomba appointment kabla ya lunch time kupita!
 
unajifanya mtoto eeeeeh??? yaningiliana nini??? khaaaa!!!
 
Kwani si ni vitu vya kutoka 2005? Mwambie tu au labda kama tangu mwanzo ulimuhakikishia kuwa hujawahi kuguswa mwili na mwanaume. Mwambie ukweli tu na wala sio kosa hilo mbona
 
ni vizuri kumwambia mahusiano yako ya nyuma na sababu iliyopelekea kutofautiana ila swala la huyo kijana kufahamu mtu uliyekuwa nae kabla wewe kaa kimya maana ushakosea kuonesha kuwa hamfahamiani na kama nae ana akili ameelewa, isipokuwa kama ule uhusiano wenu wa nyuma wewe ndio mwenye matatizo basi anaweza kumpa tahadhari ndugu yake.
 
Bidada tena ukimaliza hapo uwahi haraka kabla ya hatari, yule aliyejifanya hakujui sasa hivi anatembeza sumu hatari, yaani anaweza akawa amesha waambia watu hata wanne "namjua yule msichana" bora umwambie kabla hajaambiwa na mwingine, inaonekana kwenye kuelezea background yule ulimruka , narejea kwenye thread moja ilikuwepo hapa juzi kwamba kwa nini wanawake huwa wanapunguza idadi ya wanaume waliokuwa nao mahusiano,while wanaume wanaongeza? jibu tumelipata kwako
 
Nitaonana nae badae, sijamwambia nataka kumwambia nini ila nimemwambia nina jambo muhimu la kuongea nae.
Nahisi bado hajaambiwa chochote.
Nitawapa feedback na nashukuru kwa ushauri wenu
 
X nilikutana nae na ameshaoa,sina feelings zozote kwake tangu nilipoamua kua sitamtafuta tena.
Kweli, naona bora kumwambia

Halafu wewe DP usirudie kutumia maneno makali namna hiyo. Kichwa cha habari kina-mislead. Kinaonesha kama ulikuwa na uhusiano na mtu, na wakati huo huo ukanganya mapenzi na ndugu yake. Ila mada yenyewe inaongelea uhusiano halali uliokuwepo kabla ya kukutana na huyu kijana. Kwa hiyo ungesmea kuwa ulikuwa na uhusiano na ndugu wa BF wako wa sasa. Kuwa na uhusiano na mtu (hadi wa kimapenzi si kosa) ila kutembea na kufanya ngono na mtu mwingine wakati huo uko kwenye uhusiano (kutembea nje ya uhusiano wako au ndoa) ndo dhambi ambayo wanaume wengi huwawia vigumu kuisamehe. Issue yako ni very simple! Labda mwanaume awe mpuuzi!!
 
Nitaonana nae badae, sijamwambia nataka kumwambia nini ila nimemwambia nina jambo muhimu la kuongea nae.
Nahisi bado hajaambiwa chochote.
Nitawapa feedback na nashukuru kwa ushauri wenu

Hapo umetumia busara sana. Usi-pre empty issue (usimwambie mapema) na wala usipanic. Wewe mrushie kamba ajinyonge mwenyewe. Nakuhakikishia utashangaa majibu yake....

Tunasubiri feedback (mshindonyuma)
 
da pretty uko sawa tu na mimi, honey pot its yours, you can give it to any one.
Mweleze huyo kijana alijue hilo mapema.
Pia its sounds like umemzidi umri kidogo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…