Nilithubutu nikaweza

naliwe

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2013
Posts
410
Reaction score
987
Mwanzoni haikua rahisi, ile miezi miwili au mitatu sitaisahau kwenye maisha yangu kwani ilikua ni migumu sana

Biashara niliyoanza nayo haikua biashara sahihi kabisa mambo yakawa magumu sana tena sana

Watu wakanicheka,wakanidharau sana niliumia sana,lakini sikuvunjika moyo nikajipa imani kwamba iko siku tuu

Ile biashara nilidumu nayo kwa muda wa mwaka mzima bila kuleta mafanikio yoyote zaidi tu ya kuniongezea madeni mtaani,nilikonda sana wapo watu walionishooshea kidole kua nimeukwaa

Maisha ya mtaani yamenijenga nimejifunza mengi,nimeamini kwenye nia pana njia ,nakiri maisha yakuajiriwa yamenipotezea muda wangu mwingi sana zile nguvu nilizozitumia kwa mwajili wangu ningezitumia mapema kwenye sughuli zangu binafsi basi ningekua mbali sana

Mtaani kuna fursa nyingi sana ambazo ukiwa mwajiriwa uwezi kuziona kamwe,kweli nawaambia nimeziona fursa nyingi nimechangamkia moja sasa ivi nimeajiri watu zaidi ya 30

Vijana went angle nawashauri tafuteni pesa sio ajira, Tanzania ya magu sio mchezo,pesa ni chache mtaani lakini mianya ya kutafuta pesa ni mingi

Nawakilisha
 
Huo ndo ukweli mkuu, Furusa zipo,
 
Mkuu hapo umesema kweli lakini ungetusaidia zaidi kama ungetuambia unafanya nini hasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…