Niliugua kifua kikuu(TB)





Ipi ni sababu sahihi?
 
Ipi ni sababu sahihi?
Sababu kuu iliyopelekea nikaacha dawa ni maeneo niliyokuwa nachukulia dawa nikahama mkuu Ze Heby.

Nilijiaminisha kuwa nimepona kwa sababu afya yangu ilirudi kama zamani

Kwa hiyo pindi nimehama sikutaka kuendelea na dawa japo nilijua kabisa kuwa ni kosa ndo maana nimeuliza.
 
Kwa kuongezea swali, uliacha kutumia dawa miaka 4 iliyopita, nn leo kimekufanya uhofie? Kuna dalili zozote za kuugua?
Sijahisi dalili zozote zile kuwa naweza kuugua tena TB mkuu Jozzy

Afya yangu ipo kama zamani tu kabla sijaugua huo ugonjwa.
 
Sijahisi dalili zozote zile kuwa naweza kuugua tena TB mkuu Jozzy

Afya yangu ipo kama zamani tu kabla sijaugua huo ugonjwa.
Basi kuna mawili, la kwanza pengine umepona kabisa, la pili wadudu wa TB (Mycobacterium tuberculosis) wamekuwa weaken na dawa ulinzi wa mwili ukawaweza na hivyo wakawa kwenye latent form, endapo immunity itashuka kwa sababu yoyote ile TB inaweza kuonekana. Ushauri wangu usiwe unakatisha dozi, kwa sababu ugonjwa unaweza kukurudia, pia unasababisha dawa hizi zizoeleke kwa wadudu (drug resistance - wadudu wa TB wana uwezo wa kupasiana genes zinazotoa ulinzi dhidi ya dawa fulani) kiasi kwamba miaka ya baadae hazitafaa kwa matibabu
 
Akhsante sana kwa ushauri wako mzuri mkuu Jozzy.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…