mwezi uliopita, nilienda kufanya sherehe na rafiki zangu, nikarudi usiku kama wa saa sita ivi. sina gari (ugaibuni). mabasi nilikuwa natumia hivyo kabla sijafika home, ikabidi nitembee tu. katika umbali wa kilomita moja niliyotembea, nilikutana na machangudoa nane, mmoja mzungu blonde, saba ni waafrica (wanigeria), walivyovaa nilitamani kukimbia dunia, na wakiona unatokeza ndo wanasimama kuanza kujizungusha, kushusha zaidi kichupi na kufanya vimbwanga vya ajabu. bahati mbaya hawakujua kuwa mimi ni pastor, namshukuru Mungu nilimshinda shetani, nikamkanyaga shetani akalegea na kushindwa. kilomita moja niliona ni mbali kama kilomia mia moja kufika home...jamani hivi wanijeria wana matatizo gani, wamejaa huku ulaya kujiuza na kutuchafulia jina la waafrica? nyie madada mnaokuja huku ulaya, hakika ukivaa vibaya hata mchana, interpretation ambayo wazungu wanajua ni kwamba wewe ni changu sasa unasubiri giza liingie...Mungu ibariki africa.