Nilivyobebeshwa vitu hatari na magendo bila kujijua

Nilivyobebeshwa vitu hatari na magendo bila kujijua

Cheef Baroka

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2019
Posts
491
Reaction score
1,010
Leo naomba ku share nanyi matukio nilowahi kupitia yakubebeshwa vitu vya hatari pasi na kuelewa.

1: Mwaka 2002 Nikiwa darasa la 2 Mama yangu mzazi alifariki dunia. Nikaombewa ruhusa na kwenda kumzika (nilkuwa nikiishi na baba Mwanza). Baada ya Mazishi nilipata homa kali ambayo hospital za pale kigoma mjin ikiwemo Maweni wakasema hawaoni kitu hivyo mzee akanipeleka hospital ilioko Manyovu ambapo ni mpakani wa Burundi na Tz inaitwa NYAMASOVU( wenyeji mtanikosoa kama nakosea.)

Nakumbuka mzee alinivisha nguo za shule na begi lisilo na kitu ili ku escape nauli. Nikatibiwa pale na doctor wa kizungu baada ya muda wa siku 3 nikawa fresh hivyo nikaruhusiwa. Baada yakutoka nje ya hospital nikakutana na yule Doctor akiwa na wenzeke wa tatu alikuwa ananipenda sana na walikuwa wanaelewana na mzee mana mzee alikuwa akijua kizungu, basi wakasema wanaelekea burundi ila maeneo ya karibu na mpakani.

Me sijawahi kufika Buja ko nikatamani sana ikabidi watubebe mana mzee alikuwa na passport tukavuka. Kufika kule tukakutana na rafik wa mzee wa miaka mingi alikuwa akifanya biashara akitoa mzigo dubai anapeleka burundi na rwanda, walifurahi kukutana pia mzee akanitambulisha kama mwanae.

Jamaa likawa benet sana na mimi mara linipe maparachichi mara lininunulie juice badae likanipeleka cafe kula huku baba akiwa na wale wazungu basi kufika kule likawa limeniagizia chakula likanivua mkoba eti likague daftari zangu nikaliambia hakuna daftar likasema ngoja nikuwekee zawadi humu nikawa linapakia parachichi kume likaniwekea bastora mbili pasi kujua.

Baada ya kula likaubeba ule mfuko lenyewe hadi kwenye gari letu likaninunulia shuka moja (branket) eti kuna baridi hivyo kufanya lile begi kujaa sana na kuwa nzito ajabu huku tukijua ni zawadi tu za yule jamaa. Basi tukarudi na tulipofika mpakan askari hawajatusumbua mana tupo na gari la ile taasisi na wale wazungu madactari ambao wanafahamika sana pale mpakani mana wanapita sana.

Baat yakuvuka lijamaa likampigia sim mzee kumuuliza kama kavuka salama mzee akajibu ndio, na tukawa tumeachana na wale wazungu tukaenda panda gari pale Mnanila (nakumbuka tulikosa gari za abilia tukapanda magari ya mizigo ya udongo wanauita pemba ) likaishia sehem moja panaitwa Mwandiga. Muda wote huo me nimebeblea lile begi nzito ajabu afu lilikuwa kubwa (siunajua wazee wa zamani walikuwa wakitununulia vitu vinavyotushinda umri ili tukue navyo) niliteseka nalo sana but sijamwambia mzee kwa kumuogopa. Tukapanda daladala mpaka mwanga then home. Nilipofika home nikafika natupe lile begi nje nikaendakulala mana nilichoka sana.

Nalala kama dkk3 kanakuja kadogo kangu kakike na lile begi kakiwa kameshatoa zile zawadi za yule jamaa zimebaki bastora mbili na tuvyuma flan ivi ambapo tulihisi ni risasi. Zile bunduki zilipangwa kwa ustad mkubwa kwa kuzisamamisha na kuzificha ambapo ukikagua begi harakaharaka huwezikuona . Basi dogo ananionesha mara likaja kundi la watu walokuwepo (wengine wamekuja kuniona wengine walikuja kuhani msiba) wakitaka kujua nini ameona yule dada angu mdogo hadi akakimbia na lile begi akipiga kelele kuja kwangu.

Me nikiwa sijui chakufanya kadogo kakaficha lile begi kakashika lingine kakihofia habari zisifike kwa mzee tukachapwa. Basi wale wananzengo wakafoka sana kwamba dogo kawashtua bila kitu cha msingi. Sasa kimbembe kikaja kumpa taarifa mzee mana tuna muogopa sasa tunamwambiaje?. Ikibidi tumwambie mama mkubwa amwambie mzee tulichoona kwenye begi duh! Acha mamkubwa awashe moto kwamba baba alitaka kuniuwa mana haewezikani anibebeshe mabunduki bila kujua mzee akawa anashangaa huku mamkubwa akiendelea kumwaga maneno kwamba ndomana mzee kavungia eti Maweni hawakuona ugonjwa ili anipeleke burundi akanibebeshe mabunduki.

Mzee alipaniki sana akanipeleka pembeni kunihoji vizuri akagundua ukweli na akanilaum kwann niliskia begi nzito na sijamwambia?. Basi kabda yakufanya chochote yule jamaa kumbe alikuwa anafatilia mzigo wake akaja home wakaitana pembeni sikujua nini walionge na nini kiliendelea.

Hiyo ni stori yangu ya kwanza. Kwa kupunguza urefu kisa cha pili nakishusha kwenye comments. Kama nawewe unacho chako share na sisi tafadhali
 
Mm nilipakia abiria kumbe abiria alibeba kimkoba chenye bangi misokoto kama buku hv..kufika mbele beria ya polisi...wanataka kusachi gari...nikawauliza kuna shida yeyote..wakasema hakuna shida ni ukaguzi wa kawaida...wakaanza tafuta wakafungua buti wakaanza kagua mabegi...hamadi kibegi hichi hapa kimejaa misokoto...wakatuweka chini ya ulinzi...kumbe kile kituo alichopandia baharia ni kituo maarufu cha waasafirisha ngada..so jamaa alipopanda ...makachero wakawatonya polisi kituo cha mbele...hiyo kesi ilinipotezea muda na pesa ambazo huwezi amini...ndo nimejifunza kutowapa watu lifti hovyo
 
Mm nilipakia abiria kumbe abiria alibeba kimkoba chenye bangi misokoto kama buku hv..kufika mbele beria ya polisi...wanataka kusachi gari...nikawauliza kuna shida yeyote..wakasema hakuna shida ni ukaguzi wa kawaida...wakaanza tafuta wakafungua buti wakaanza kagua mabegi...hamadi kibegi hichi hapa kimejaa misokoto...wakatuweka chini ya ulinzi...kumbe kile kituo alichopandia baharia ni kituo maarufu cha waasafirisha ngada..so jamaa alipopanda ...makachero wakawatonya polisi kituo cha mbele...hiyo kesi ilinipotezea muda na pesa ambazo huwezi amini...ndo nimejifunza kutowapa watu lifti hovyo
Pole sana kaka.
 
Jamaa aliucheza mchezo vizuri sana.. ila mngedakwa pale border msala ungekuwa kwa mzee wako na sidhani kama angeeleweka kirahisi.
 
Back
Top Bottom