Nilivyoenda kuwinda na wazee

Kunguru wa Manzese

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2016
Posts
12,729
Reaction score
18,119
Zamani kidogo tulienda kuwinda na wazee wa makamo wanne. Kwakuwa mimi nilikuwa mdogo nikaambiwa kazi yangu ni kumpiga kabali/roba mnyama wakishatamka neno "TAYARI". Kisha wao watasogea na kumchuna. Basi mnyama wa kwanza alikuwa digidigi baada ya kunasa kwenye mtego nilimpiga six one nine wakaja kumchuna..


Mnyama wa pili nakumbuka alikuwa pofu nilimchapa roba kali sana akafia pale pale,wakaja kunilaumu wakisema "tutakulaje kibudu?" Basi tukaenda hadi mnyama wa 3,nilimrukia vibaya sana [emoji22] kama kawa akala roba ya mbao,nasubiri wazee nashangaa wametimua mbio sana...
 
Duuu!!!! Mnyama gani huyo???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…