Barnabas Mashamba
JF-Expert Member
- Jul 4, 2020
- 797
- 2,233
Technical error.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ndiyo mkuuTunaendelea
Nje ya mada kidogo. Ni hivi, nilipokuwa darasa la tatu niliteuliwa kuwa Bwana Afya (kiranja wa afya, cheo cha kuhakikisha vyoo vipo safi na majivu yamewekwa kila siku asubuhi-kama hujui umuhimu wa majivu kwenye vyoo vya shimo, utakuwa wa 2000 au uliishi kishua maisha yako yote). Nilidumu katika nafasi hiyo hadi nilipofika darasa la tano, walipohitimu waliokuwa darasa la saba mwaka huo nikapewa cheo cha Mtunza Ofisi maana aliyekuwa na cheo hicho alihitimu.
Nilipofika darasa la sita, majukumu yaliongezeka, niliongezewa majukumu ya kuwa Mkutubi Msaidizi. Hiki cheo kilikuja baada ya Mzee Mkapa kushusha madarasa ya maana enzi hizo (kutoka madarasa ya tofali za udongo (maarufu kama biskuti), hadi madarasa yenye sakafu nzuri), na yalipokamilika madarasa hayo (yalikiwa chini ya mpango wa MMEM) vilishushwa vitabu visivyopungua mia tano shuleni kwetu na tuliambiwa ni kwa ajili ya maktaba ya shule. Kwa kuwa nilikuwa mtunza ofisi ndiyo hapo nikapewa tena kazi ya kuwa mkutubi msaidizi nikimsaidia mkutubi mkuu ambaye alikuwa mwalimu wa taaluma (ngoja kwanza nielezee majukumu yaliyokuwepo).
Majukumu ya mtunza ofisi.
Kuhakikisha kila siku asubuhi ofisi zimefunguliwa kabla ya saa 12:50. Hivyo niliwajibika kuwahi shuleni na kwenda kwa mwalimu wa taaluma kuchukua funguo. Baada ya hapo nafungua ofisi zote (ya mkuu na ya walimu), nahakikisha usafi wa ofisi zote umefanyika (alikuwepo binti kwa ajili ya kufagia lakini akichelewa lazima nIlipaswa kutafuta mwanafunzi mwingine ili afagie), na kuhakikisha meza za walimu hazina vumbi, madaftari yamepangwa (ya walimu na ya wanafunzi kama hayakusahihishwa na kurudishwa madarasani) vyema yaani kila kitu kipo vizuri.
Vilipoletwa vitabu vingi, kukawa na maktaba rasmi shuleni. Jukumu langu likawa kuhakikisha hakuna kitabu hata kimoja kinapotea, pia ndiye nikawa na jukumu la kuazimisha vitabu kwa wanafunzi na kuhakikisha wamerejesha katika siku niliyowapangia.
Wakuu, kusema ukweli, nilifaidika sana na maktaba hiyo. Na kwakuwa vitabu vyote vilikuwa chini yangu, nilisoma vitabu vingi mno mno. Vitabu vililetwa vya kila aina, vya stori za sungura na fisi, Watoto wa Mama Ntilie na Kiu ya haki (nilishangaa nilipofika form one na kukuta form three na form four wanasoma vitabu hivyo huku mimi nilishavisoma toka niko darasa la sita), kitabu cha MWALIMU MKUU WA WATU, n. k, nashukuru mpaka nakabidhi ofisi hakuna hata kitabu kilichopotea (vingi vilianza kupotea Kwa waliopewa majukumu hayo baada yangu). Hata nilipofika form one, nilirudi nikaazima kitabu cha Grammer in English (bonge moja la mjikitabu, lilinisaidia sana kukuza English yangu na hili likitabu lazima nilitafute madukani niwanunulilie wanangu). Kitabu hicho nilikiazima nikiwa form one mwezi wa kumi na mbili, mkutubi akaniambia nitumie mpaka nitakaporidhika ndipo nirudishe, sema alifariki nikiwa form two mwezi wa tano na hivyo nikalazimika kukirudisha. Narudia tena, lilikuwa bonge moja la kitabu, hadhi yake kile kitabu haikuwa kuwa kwenye maktaba ya shule ya msingi.
Turudi sasa kwenye mada yetu.
Tuliishia jamaa ameshafika rasmi kwenye kambi iliyokuwa ikijisomea kwa kuweka makazi yake kwa mwalimu mkuu msaidizi.
Nilikubaliana na jamaa yangu kuwa hatutakuwa tunapeana taarifa ya alichokiona kwa njia ya mdomo, tutatumia karatasi ili kuepusha udadisi wa kwanini tumekuwa karibu sana baada ya yeye kuanza kulala kwenye kambi hiyo ya kujisomea.
Karatasi aliileta kwa njia ifuatayo.
Kwa kuwa mimi ndiye niliwajibika kufungua ofisi, na kwa kuwa nami kipindi hicho nilikuwa kwenye kambi ya pili ya kujisomea ambayo nilieleza iliweka makazi yake kwenye nyumba iliyobaki wazi baada ya mwalimu aliyekuwa akikaa humo kuhama, baada ya kukaa kambini, nilikuwa nakuwa mtu wa kwanza kufika shuleni (mara chache sana aliniwahi mgonga kengele).
Kambi ya kwa mama mdogo wa mjimilikisha dictionary (ya kwa mwalimu mkuu msaidizi) ilikuwa nyuma ya ofisi zote mbili (ofisi ya walimu na ofisi ya mkuu wa shule). Ukiwa unatoka kwenye hiyo kambi, unaweza kupita katikati ya madarasa (kulikuwa na uwazi uliotenganisha madarasa ambayo pia kuna ofisi ya walimu), na madarasa ambayo kuna ofisi ya (mwalimu mkuu). Na njia nyingine unapita nyuma ya ofisi ya mwalimu mkuu (hasa kwa wale waliokuwa wanasoma darasa la sita na la saba). Hivyo, tukakubaliana, nikifika nifungue madirisha ya ofisi ya mwalimu mkuu, kisha nielekee ofisi yenye maktaba (ilikuwa rahisi zaidi kumuona akitoka kambini kutokea kwenye ofisi hiyo), akifika usawa wa dirisha la mwalimu mkuu, alipaswa kudumbukiza karatasi ya maelezo ya alichokiona).
Ili tuende na muda vizuri (timing), maana hapo kuna mdada wa kufagia ofisi anaweza kuwahi kuingia kabla yangu ofisini kwa mwalimu mkuu baada ya karatasi kudondoshwa, ilipaswa jamaa afanye tukio lolote la kunijulisha kuwa naenda (tukio kama kukohoa, au kumuita mwanafunzi kwa sauti kubwa kumwambia aokote uchafu au afagie, maana kabla ya viranja waliokuwa darasa la saba kustaafu, naye alikuwa kiranja hivyo ukiranja mstaafu ilikuwa tiketi ya kufanya mchezo usishitukiwe).
Hapo ningesubiri dakika zisizozidi tano ningeenda ofisini kwa mwalimu mkuu na kuokota karatasi aliyodondosha na kusoma ujumbe alioandika.
Baada ya hapo, nilipaswa kumjibu kuwa nimeona maelezo yake na nini tufanye kuichukua (kama amekuta kweli dictionary ipo). Mimi nilipaswa kumwekea karatasi hiyo kwenye shimo la takataka (mitaa ya hilo shimo siyo ndani ya shimo). Shimo hilo lilikuwa njiani ukiwa unaelekea chooni, hivyo nilipaswa kurusha hiyo karatasi kama narusha uchafu (uzuri shimo lilikuwa linasafishwa kwa karatasi na uchafu wote kuchomwa asubuhi wakati wa usafi hivyo nyakati natupa karatasi hapakua na makaratasi mengi ya kumchanganya na pia karatasi hiyo nilipaswa kuirusha upande wa mashariki wa shimo hilo). Baada ya mimi kutoka chooni, angesubiri angalau dakika 10, akiona mtu anakwenda chooni, angeongozana naye na yeye angeenda kuchukua karatasi hiyo na kuisomea huko chooni na akimaliza aidumbukize chooni (na mimi nilipaswa kuidumbukiza chooni karatasi aliyoniletea wakati nikiwa nimeenda chooni).
Siku ya kwanza tokea jamaa yangu aanze kujisomea na kulala kwenye hiyo kambi, asubuhi yake alinidondoshea ujumbe kama tulivyokubaliana.
Tutaendelea kesho usiku saa mbili kamili juu ya alama na tutaona jamaa alileta ujumbe gani.
Kumbe UJASUSI ulianza kitaambo 😎Tunaendelea