Nilivyoibiwa chaja ya simu Mwanza kizembe

Idrissou02

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2018
Posts
354
Reaction score
656
Juzi juzi tu niliwasili mkoani Mwanza usiku sana nikitokea mkoa fulani. Nikasema isiwe kesi ngojea nikapumzike kabla asubuhi sijakwenda uko nilipotaka kufika. Kweli nikapata guest moja karibu na stend ya mabasi ya Buzuruga, nikalala hapo mpaka asubuhi.

Asubuhi nilichelewa kuamka, nikaamshwa na sauti ya mlango ukigongwa hodi, ilikuwa takribani mida ya saa 2 asubuhi hivi. Nikajifunga taulo na kwenda kufungua mlango. Nikamkuta dogo mmoja ambae sidhani kama anazidi umri wa miaka 21.

Akaniambia anaomba aniazime chaja yangu ya simu aboost simu yake ili afanye mawasiliano na kwamba yupo chumba cha pembeni yangu hapo. Nikamwambia sawa ila nitaichukua si muda maana mi pia naondoka asubuhi hiihii.

Kweli bana nikamaliza mambo yangu yote ya kujiandaa, nikasema ss niko tiari kuondoka niende kumcheki dogo anipe chaja yangu.

Asalale! Nlimkuta sasa? Chumba cha jirani kulikua na mtu mwengine tofauti kabisa, nikasema labda kamaanisha chumba cha jirani kingine, nikagonga vyumba vyote ndani ya ile guest hakuna hata chumba kimoja alichofungua yule dogo

Dah nikaondoka kinyonge baada ya kutambua nishaingizwa mjini na msukuma.
 
Chaja ya Orion 🀣 🀣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…