Nilivyokutana na Mariam kipindi nimemaliza kidato cha 4 nikiwa sina hili wala lile

Nilivyokutana na Mariam kipindi nimemaliza kidato cha 4 nikiwa sina hili wala lile

Magical power

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2022
Posts
2,158
Reaction score
5,626
Kipindi nimemaliza kidato cha 4 nikiwa sina hili wala lile yani sina mchongo wowote ule, nilisoma mbali na kitaa chetu kwahiyo kupata hata masela wa kunipa dili ilikuwa ngumu.

Kuna siku nilikuwa sina hata shilingi 500 ya kwenda Banda umiza kuangalia mechi ya Manchester United dhidi ya Liverpool.

Nilikuwa na mawazo sana lakini ghafla kuna Binti alinishika bega na kuongea "hauna hela ya kwenda mpirani eeeh ",naombe twende basi, nilishangaa na kuuliza amejuaje basi yule Binti alisema alisikia najiongea mwenyewe tu akaamua kunipa msaada.

Basi sikuzuga. Soka ni kilevi niliongozana nae hadi banda umiza na alinilipia hela na tulicheki game ijapokuwa yeye alikuwa ni Chelsea, baada ya hapo aliniomba namba yangu ya simu ili tujuane zaidi.

Baada ya kunipa namba tuliingia kwenye mahusiano ya kimapenzi sikujua katokea wapi, lakini niliingia kwenye mapenzi nae, kwake ilikuwa furaha kuwa na mimi, lakini mimi nilimpenda kisa hela na vitu alivyokuwa akinipa.

Nilikaa naye kwenye mahusiano kwa miezi mitatu na kuna siku alinitoa Out kwenye hoteli yenye thamani kubwa sana ambayo sikuwaza kuingia katika maisha yangu.

Tulifika eneo la tukio nilipata good time nae lakini baada ya muda aliomba aende Chooni kidogo basi mimi msela nikabaki peke yangu.

Kipindi nimekaa alikuja jamaa fulani hivi na ilikuwa ni sura ngeni kwangu lakini alipofika aliniuliza" huyo mpenzi wako jina lake anaitwa Mariam Eeeh " nilishangaa alimjuaje mpenzi wangu?

Jamaa aliniambia huyu Mariam alikuwa ni jirani yake na alifariki miaka 20 iliyopita kisa mateso ya mapenzi na aliniambia nisiwe naye karibu kwa usalama wangu halafu akasepa.

Baada ya taarifa hiyo nilikimbia eneo lile kama Mwehu, breki ya kwanza ilikuwa chumbani kwangu nilifika na kujitupa nikiwa na uoga wa hatari lakini mara ghafla kwa maajabu nilimuona Mariam mbele yangu.

Sikujua amefikaje na aliniambia "ulichoambiwa kule Hotelini ni kweli kabisa mimi nilifariki miaka 20 iliyopita lakini nilirudi mara yapili ili nione kama naweza pata mapenzi yakweli, lakini kumbe Wanaume wote mpo sawa hata wewe ulinipenda kisa hela kama yule wa miaka 20 iliyopita aliyeniua kisa pesa za kwetu....."

Baada ya hapo Mariam alipotea kimiujiza na sikuwahi kumuona tena.

NAKUMBUKA SURA YAKE ALIKUWA MREMBO, NAKUMBUKA JINA LAKE ALIITWA MARIAM.

1736940143498.jpg
 
Kpindi nimemaliza kidato cha 4 nikiwa sina hili wala lile yani sina mchongo wowote uleView attachment 3202476 ,nilisoma mbali na kitaa chetu kwahiyo kupata hata masela wa kunipa dili ilikuwa ngumu .

Kuna siku nilikuwa sina hata shilingi 500 yakwenda Banda umiza kuangalia mechi ya Manchester United dhidi ya Liverpool.

Nilikuwa na mawazo sana lakini Ghafla kuna Binti alinishika bega na kuongea "hauna hela ya kwenda mpirani eeeh ",naombe twende basi ,nilishangaa na kuuliza amejuaje basi yule Binti alisema alisikia najiongea mwenyewe tu akaamua kunipa msaada ..

Basi sikuzuga ,Soka ni kilevi niliongozana nae hadi Banda umiza na alinilipia hela na tulicheki game ijapokuwa yeye alikuwa ni Chelsea ,baada ya hapo aliniomba namba yangu ya simu ili tujuane zaidi .

Baada ya kunipa namba ,tuliingia kwenye mahusiano ya kimapenzi sikujua katokea wapi ,lakini niliingia kwenye mapenzi nae , kwake ilikuwa furaha kuwa na mimi,lakini mimi nilimpenda kisa hela na vitu alivyokuwa akinipa.

Nilikaa naye kwenye mahusiano kwa miezi mitatu na kuna siku alinitoa Out kwenye hoteli yenye thamani kubwa sana ambayo sikuwaza kuingia katika maisha yangu .

Tulifika eneo la tukio nilipata good time nae lakini baada ya muda aliomba aende Chooni kidogo basi mimi msela nikabaki peke yangu.

Kipindi nimekaa alikuja jamaa fulani hivi na ilikuwa ni sura ngeni kwangu lakini alipofika aliniuliza" huyo mpenzi wako jina lake anaitwa Mariam Eeeh " nilishangaa alimjuaje mpenzi wangu?

Jamaa aliniambia huyu Mariam alikuwa ni jirani yake na alifariki miaka 20 iliyopita kisa mateso ya mapenzi na aliniambia nisiwe naye karibu kwa usalama wangu alafu akasepa .

Baada ya taarifa hiyo nilikimbia eneo lile kama Mwehu ,breki yakwanza ilikuwa chumbani kwangu nilifika na kujitupa nikiwa na uoga wa hatari lakini mara ghafla kwa maajabu nilimuona Mariam mbele yangu.

Sikujua amefikaje na aliniambia "ulichoambiwa kule Hotelini ni kweli kabisa mimi nilifariki miaka 20 iliyopita lakini nilirudi mara yapili ili nione kama naweza pata mapenzi yakweli ,lakini kumbe Wanaume wote mpo sawa hata wewe ulinipenda kisa hela kama yule wa miaka 20 iliyopita aliyeniua kisa pesa za kwetu ..

Baada ya hapo Mariam alipotea kimiujiza na sikuwahi kumuona tena .

NAKUMBUKA SURA YAKE ALIKUWA MREMBO ,NAKUMBUKA JINA LAKE ALIITWA MARIAM .
Thibitisha story yako Kama Ina ukweli ndugu maana tupo nje ya muda
 
Shida ya kunywa gongo mixer bangi ukiwa umejifungia geto huna hili wala lile na oppo yako unafatilia pilikapilika za mchaga na mnyaturu af uko upande wa mchaga then unapitiwa na usngz mzto.baadae unaamka una boost kisungura unachkua oppo yako unawasha data unaingia jf kuandka ulichoota daaah, mpaka kwenye kampeni itakuwa 1USD = 5000TSH so kila mtu atasala kikubwa ni muda tu.
 
Back
Top Bottom