Nilivyonunua chainizi zenye harufu ya dawa

Mrs Gudman

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2015
Posts
613
Reaction score
1,297
Nitoe short story tu katika muendelezo wa kuelimisha jamii juu ya kilimo hai(organic farming).

Mimi Kwangu nimepanda mboga mboga katika mifuko hivyo mara nyingi huwa sinunui mboga sokoni, sasa juzi ilitokea nimefululiza kuchuma ikabidi ninunue tu mboga kwa siku hiyo.

Mbogamboga ambazo huwa napenda kununua ni majani ya maboga, mchicha laini,au tembele kutokana na kuwa hazina magonjwa mengi hivyo hata kunyunyiziwa dawa ni rare sana.

Mahali naponunuaga nikakuta mboga zote hakuna zipo tu chainizi so ikabidi tu nijikaze nikazinunua kwa sababu sikuwa na option.

Kiukweli mboga zile zilikuwa zinanuka dawa mpaka zimefika mezani, yani ni kama vile zilinyunyuziwa dawa two to three days ago then zikavunwa na kuletwa sokoni.

Nilikula mboga ile ka vijiko viwili nikaamua kuiacha na ikabidi tu imwagwe mana harufu ya sumu Ilikuwa kali kupitiliza.

#Ni mara nyingi sana wakulima wamekuwa wakinyunyiza dawa katika mboga matunda na mazao mengine bila kuzingatia hatua ya mazao hayo(i. e nyanya zimeiva kabisa anaona ugonjwa ananyunyiza dawa badala ya kuvuna).

Au ng'ombe anachomwa sindano asubuhi jioni anakamuliwa wakati dawa inaelekeza maziwa yatumike baada ya siku 5 au saba

#Kwa namna hii kutokomeza magonjwa yatokanayo na chemical kwa binadamu ni kazi sana.

#Kuna haja ya serikali na wadau wa sekta za kilimo, mifugo na uvuvi kutoa elimu juu ya matumizi sahihi ya hizi chemical.

#Lakini kubwa zaidi kuna haja ya sisi kurudi kwenye kilimo HAI, Kuzalisha bila matumizi ya chemical na mbolea za viwandani kwa maslahi( ya afya zetu, udongo na mazingira) ambazo kwa kiwango kikubwa zinachangia kuibuka kwa magonjwa mengi kwa binadamu na wanyama.

#ORGANICAGRICULTUREAMBASSADOR

AgriGanic Tz
P. O. Box 2021,
Dodoma Tz

E. Mail: Pnairah@gmail.com[/email
 
Nini Madhara ya hizo sumu mwilini?
Kufeli kwa figokibofu, cancer ni baadhi tu ya magonjwa yanayoweza kusababishwa na chemical hizi nafikiri.

Mtaalamu wa afya ya binadamu anaweza kutusaidia zaidi kuliko mimi.
Asante sana karibu.
 
Mwisho wa siku maradhi yote hayo hupelekea kifo.

Tusiogope kufa hatutaishi milele mkuu.
 
Siyo kwamba tunaogopa kufa la hasha ila kwa kawaida maradhi yana economic consequences nyingi, badala ya kusomesha watoto utakuwa busy kujitibu, badala ya kujenga unajitibu mwisho wa siku unakaribisha u maskini kwenye jamii wakati hakuna gharama kubwa kula organic
 
Nitoe short story tu katika muendelezo wa kuelimisha jamii juu ya kilimo hai(organic farming).

Mimi Kwangu nimepanda mboga mboga katika mifuko hivyo mara nyingi huwa sinunui mboga sokoni, sasa juzi ilitokea nimefululiza kuchuma ikabidi ninunue tu mboga kwa siku hiyo.

Mbogamboga ambazo huwa napenda kununua ni majani ya maboga, mchicha laini,au tembele kutokana na kuwa hazina magonjwa mengi hivyo hata kunyunyiziwa dawa ni rare sana.

Mahali naponunuaga nikakuta mboga zote hakuna zipo tu chainizi so ikabidi tu nijikaze nikazinunua kwa sababu sikuwa na option.

Kiukweli mboga zile zilikuwa zinanuka dawa mpaka zimefika mezani, yani ni kama vile zilinyunyuziwa dawa two to three days ago then zikavunwa na kuletwa sokoni.

Nilikula mboga ile ka vijiko viwili nikaamua kuiacha na ikabidi tu imwagwe mana harufu ya sumu Ilikuwa kali kupitiliza.

#Ni mara nyingi sana wakulima wamekuwa wakinyunyiza dawa katika mboga matunda na mazao mengine bila kuzingatia hatua ya mazao hayo(i. e nyanya zimeiva kabisa anaona ugonjwa ananyunyiza dawa badala ya kuvuna).

#Kuna haja ya serikali na wadau wa sekta za kilimo, mifugo na uvuvi kutoa elimu juu ya matumizi ya hizi chemical.

#Lakini kubwa zaidi kuna haja ya sisi kurudi kwenye kilimo HAI, Kuzalisha bila matumizi ya chemical na mbolea za viwandani kwa maslahi( ya afya zetu, udongo na mazingira) ambazo kwa kiwango kikubwa zinachangia kuibuka kwa magonjwa mengi kwa binadamu na wanyama.

#ORGANICAGRICULTUREAMBASSADOR

AgroGanic Tz
P. O. Box 2021,
Dodoma Tz

E. Mail: Pnairah@gmail.com
ikaweje
 
Siyo kwamba tunaogopa kufa la hasha ila kwa kawaida maradhi yana economic consequences nyingi, badala ya kusomesha watoto utakuwa busy kujitibu, badala ya kujenga unajitibu mwisho wa siku unakaribisha u maskini kwenye jamii wakati hakuna gharama kubwa kula organic
Unajua lini utakufa?
 
Kuna mboga lazima zipigwe sumu na huwa sizinunue sokoni na hata hivyo ni nadra kununua mboga maana nalima na zingine zinajiotea tu shambani .
Mbona zinazopulizia sana sumu .
1.chinizi ngumu na ile chainizi laini
2.mnafu
3 .kabechi
 
Binafsi zijakuelewa, tafadhali hariri ujumbe wako
 
Ungeeleza tu Nia yako kuhusu organic farming Na sio kuanza mbali hivo

Btw ni kwel kuna watu hufanya hivo lakini kiwango hadi unasikia Dawa bada ya kupika ndo nasikia Leo mkuu
 
Hahaha kumbe mnasoma?
Ni hivi ,kuna aina ya mboga piga ua lazima zishambuliwe na wadudu katika ukuaje wake.
Ndio nikazitaja
Chinisi laini na ile ngumu,figiri ,kabeji
 
Hata mm binafsi nakubali organic farming but hiyo ya dawa kusikika hadi mezani!!!!!!Mh hapana siamini maana ktk ukulima wangu wote sijawahi kuliona wala kuisikia kabisa.
 
Hahaha kumbe mnasoma?
Ni hivi ,kuna aina ya mboga piga ua lazima zishambuliwe na wadudu katika ukuaje wake.
Ndio nikazitaja
Chinisi laini na ile ngumu,figiri ,kabeji
Exactly hilo liko wazi
 
Ungeeleza tu Nia yako kuhusu organic farming Na sio kuanza mbali hivo

Btw ni kwel kuna watu hufanya hivo lakini kiwango hadi unasikia Dawa bada ya kupika ndo nasikia Leo mkuu
Si lazima niwe na njia moja ya kufikisha ujumbe, ujumbe huwafikia watu kwa njia mbalimbali

But ukitumia mifano ujumbe unafika na kueleweka zaidi

Mkuu usiwe too rigid pls
 
Hahaha kumbe mnasoma?
Ni hivi ,kuna aina ya mboga piga ua lazima zishambuliwe na wadudu katika ukuaje wake.
Ndio nikazitaja
Chinisi laini na ile ngumu,figiri ,kabeji
Dot to dot
 
Dot to dot
Haha yeh men ,ukienda sokoni usinunue au mboga Lima mwenyewe ,kama dar hata nikiingia kwa hotel siagizi kuwekewa mboga ya majani kwasababu dar wanamwagilia maji ya makaro maji machafu au wanatumia dawa sana.
 
Back
Top Bottom