Komeo Lachuma
JF-Expert Member
- Oct 31, 2014
- 7,926
- 17,030
Wapi huko boda boda anaweza ingiza 70,000 kwa siku? Nipeleke boda boda wangu 5 tu. Hizi ni stories tu asikudanganye mtu. Boda boda wamesambaa tanzania ni wengi sana kwa sasa.Nina rafiki yangu bodaboda kwa siku anaweza pata hata 70000+ akikomaa kazini ila ni mvivu. Laiti kama angekuwa ana malengo na anatamani kuyafikia ana uwezo hata wa kulaza laki kwa siku. Ni vile bado hana majukumu so siku akipata hela ya kula,ya bosi na mafuta anarelax mpaka akamatike ana shida anapiga kazi sana. So ni kawaida
Sent using Jamii Forums mobile app
Story za vijiweni hizo bro.Wapi huko boda boda anaweza ingiza 70,000 kwa siku? Nipeleke boda boda wangu 5 tu. Hizi ni stories tu asikudanganye mtu. Boda boda wamesambaa tanzania ni wengi sana kwa sasa.
Basi niliamua kutulia ndani ya difenda na kumuachia Mungu yeye ndiye akawe muamuzi wa lile jambo,kwa hatua niliyokuwa nimefikia sikuwa na msaada wowote zaidi ya kuamini ni Mungu peke yake ndiye anaweza kuniokoa na mkono wa serikali!.Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua nyumbani - 7.
Sikutaka kabisa marafiki zangu na watu wanaonifahamu pale stendi wahisi kitu,kiukweli japo nilikuwa mikononi mwa wale askari lakini nilijitahidi sana kuonyesha hali ya kawaida na tena tulipofika kwenye hiace ya kuelekea mjini ni mimi ndiye niliyefanya kazi ya kuwaombea lift nikijifanya niwanangu!
Sasa tulipofika pale mjini kukamata mchomoko wa kuelekea Sirari ilibidi askari mmoja atoe hela amlipie yule mwenzie na mimi kudandia bure,wasingeweza kupanda mchomoko bure kwasababu ilikuwa inachukua watu wachache!.
Basi tukaondoka na hatimaye tukafika pale stendi ya mchomoko Sirari,tulipofika pale wanangu walianza kunichangamkia na wengine kuniuliza nilienda wapi,sasa wale askari wakataka kunidhibiti lakini niliwaambia kiaina ya kwamba siwezi kukimbia na wasinidharirishe mbele ya wana,bahati nzuri jamaa walikuwa waelewa na wao wakawa wameniacha najifanya kujizungumzisha mbele ya washikaji kana kwamba sina kosa kumbe moyoni naujua ukweli!.
Baada ya mazungumzo pale stendi na wanangu,nilijikuta kitete chote kimetoweka na kisha nikaandamana na wale mapongo hadi nilipokuwa nimepanga!.Nashukuru Mungu hakuna mtu aliyeshitukia mchezo pale stendi.Basi baada ya kufika hapo nyumbani nilifunua kifuta miguu(zulia)pale mlangoni kisha nikatoa funguo nikafungua mlango!.Sasa ile nyumba sikuwa peke yangu,kulikuwa na wapangaji wengine ambao nao kuna wengine walikuwa kwenye shughuli zao na wengine hasa wanawake walikuwa nyumbani,sasa desturi ikawa ni ileile ya kwamba asifahamu mtu yeyote kwamba wale ni askari,nilipofungua mlango niliwakaribisha kwa sauti ya "Karibuni" ili asitokee mtu yeyote akajua kitu.
Baada ya kufika ndani askari mmoja akaniomba funguo akafunga mlango kisha wakanitaka tuanzie kufanya upekuzi chumbani.Upekuzi haukuchukua muda mrefu kwasababu sikuwa nimejaza mle ndani makorokoro,bali kulikuwa na kitanda pamoja na begi kubwa la nguo na vitu vidogo vya kawaida,sebuleni nako kulikuwa na makochi,TV na redio na picha za ukutani zilizopendezesha sebule.Hakukuwa na vyombo vingi kwasababu nilikuwaga sipiki hapo nyumbani bali nilikuwa nakula kwa mama ntilie,nilikuwa na mabeseni mawili pamoja ndoo mbili tatu nilizotumia kwa ajili ya kuwekea maji ya kuoga na kufulia.
Sasa pesa zangu zote nilikuwaga nazihifadhi kwenye mfuko wa suruali kisha naweka hiyo suruali kwenye begi pamoja na nguo nyingine,wale askari walipekua kila mahali bila kuona kitu chochote.Wakati huo nilikuwa nimebaki na zile fedha haramu kiasi cha shilingi elfu 40,pia nilikuwa nina hela halali kiasi cha shilingi laki moja na elfu themanini.
Askari "Nadhani unajua kilichotuleta hapa ni kitu gani,hebu kuwa mkweli pesa umeweka wapi?,au unataka tutumie nguvu?"
Aliendelea "Mpaka tumefika hapa umekuwa mstaarabu,angalia mambo yasije haribikia hapa"
Baada ya jamaa kuniambia vile na akionekana kumaanisha,nilichukua ile suruali iliyokuwa imetupwa chini kutokana na shaghala baghala ya upekuzi nikatoa zile hela nikamkabidhi jamaa!.
Askari "Haya sasa ndiyo mambo,endelea kutafuta najua bado zipo nyingine!"
Mimi "Hapana afande pesa niliyokuwa nayo ndiyo hiyo"
Askari "Kwanini unatupotezea muda?,siutoe pesa mdogo wangu tuondoke!,au unataka tutumie nguvu?"
Mimi "Kweli afande pesa yote niliyokuwa nayo ndiyo hiyo"
Jamaa waliendelea kutafuta kila mahali lakini hawakuona kitu,sasa kwakuwa niliwapa zile hela askari mmoja akawa amesema wanipige pingu kwakuwa tayari kidhibiti nilikuwa nacho.Niliwaangukia miguuni nikawasihi wasinipige pingu na sitowasumbua njiani!,yule askari aliyefunga mlango wakati tunaingia ndani kiukweli akawa akinionea huruma sana kama kijana mwenzie na akamwambia mwenzie asifanye hivyo kwakuwa wakati tunakuja sikuwasumbua,sasa yule mwenzie akawa ameendelea kuweka msisitizo kwamba nipigwe pingu!.
Basi baada ya kuwasihi sana huku machozi yakinitoka,wakawa wamekubali na wakanitaka nisije kujaribu kuwakimbia.Sasa wakati tunatoka nikachukua ufunguo nikampelekea dada mmoja aliyekuwa mke wa mpangaji mwenzangu hapo nyumbani,nilimwambia akae na ule ufunguo kuna mahali naenda na nikirudi nitaukuta kwake!.
Tukaondoka na wale askari mpaka stendi tukapanda mchomoko kuelekea Tarime mjini,kwa namna tulivyokuwa tunatembea na wale askari wakiniuliza maswali kadhaa huku nikiendelea kuwajibu nilihakikisha kabisa hakuna mtu anayefahamu jambo lile,mimi sikutaka kabisa kujifanya mjuaji ili kujiepusha na aibu isiyokuwa ya lazima!.
Tulipofika pale Tarime mjini tukitokea Sirari,kuna askari mmoja niliona anaongea na simu na sikufahamu alichokuwa anaongea,sasa baada ya maongezi yale kwenye simu,alimwambia yule askari mwenzake kwamba ahakikishe nakaa chini,basi nilikaa chini huku yule askari mwingine akiondoka kusikojulikana!,wakati nimekaa chini yule askari alikuwa makini sana na mimi na hakutaka kabisa stori na maongezi!.Baada ya dakika 10 niliona difenda imefika lile eneo na kutakiwa kupanda.
Moyo wangu uliuma sana na nilikuwa nawaza napelekwa wapi wakati ilipaswa nirudishwe hadi buhemba nilikokuwa nimetokea!.Sikufahamu hatima ya Gabriel na mkewe iliendelea vipi nilipowaacha!,mimi nilijua huo msalaba tayari ndiyo nishaubeba!.Kilichokuwa kinaniumiza zaidi ni namna wazazi wangu wakija kufahamu ya kwamba mtoto wao nipo polisi au kufungwa gerezani,nilikuwa navuta picha ya Mzee wangu namna atakavyo ongea akisikia nimekamatwa,tena nilijua ndiyo atajihahakishia kabisa kwamba kunitimua pale nyumbani alikuwa sahihi kabisa!.
Basi niliamua kutulia ndani ya difenda na kumuachia Mungu yeye ndiye akawe muamuzi wa lile jambo,kwa hatua niliyokuwa nimefikia sikuwa na msaada wowote zaidi ya kuamini ni Mungu peke yake ndiye anaweza kuniokoa na mkono wa serikali!.
Kuna muda hata kama humjui Mungu na hujawai kukanyaga kabisa kanisani au msikitini,unapofikwa na jambo gumu kiutatuzi ndipo siku hiyo utatamani mahubiri na mihadhara isikike mahali ulipo ili uweze kuamini kuna Mungu na utajaribu kusali sala zote na utatumia lugha zote kumuomba hata kama unayemuomba uliamini hayupo.
Mpaka wakati huo baada ya kujiingiza kwenye upiga debe na vile vistarehe uchwara vya muda mfupi sikuwahi kabisa kukanyaga mlango wa kanisa lakini baada ya kupata hiyo changamoto ya muda mfupi nilikuwa nikimlilia Mungu kimoyo moyo aniokoe na kile kikombe kana kwamba nilikuwa muhudhuriaji mzuri wa ibada!.
Baada ya kupakiwa kwenye ile difenda nilipewa amri ya kukaa chini na kusogea mbele kabisa na miguu kuikalisha chini ikiwa imenyooka,ile difenda iliondoka yale maeneo kuelekea Nyamisangura ambako tulipofika pia huko kuna jamaa kama 6 walipakiwa kwenye ile difenda na kufanya jumla yetu wahalifu kuwa 7.Basi baada ya hapo ikaondoka kwa spidi kali huku askari wengine waliokuwa na bunduki wakidandia na kuondoka!.
Sasa tulipofikishwa pale central,baada ya kushuka tulitakiwa kuelekea ndani kwa kukimbia huku mikono tukiambiwa tuweke kichwani!,baada ya kufika ndani askari mmoja wapo wa wale niliokuwa nao akawa ameniambia nifuatane naye.Ndipo akafungua chumba kimoja ambacho baada ya kuingia ndani nikamkuta Gabriel na mkewe akiwa na yule askari niliyewaacha nae pale nyumbani kwake!.
Askari "Ooh umemleta bwana mdogo"
Aliendelea "Unapofika hapa kwetu bwana mdogo hakuna makaochi hivyo unatakiwa ukae chini!".
Basi baada ya hapo nikaona yule askari anatoa ile hela elfu 40 ambayo haikuwa halali anamkabidhi yule askari ambaye ilionekana alikuwa mkuu wa upepelezi!.Kilichonishangaza ni kutokuona ile laki moja na elfu themanini ambayo ilikuwa halali sikuona anakabidhiwa yule afande na ndipo nikagundua wale askari watakuwa waligawana ile hela!.
Basi baada ya mazungumzo ya muda mrefu hapo ndani huku tukiwa tunahojiwa na yule askari kuandika maelezo yetu,alipomaliza akawa amemwambia yule askari tunapaswa kuwekwa rumande!.Kiukweli nilijuta sana moyoni na sitakaa nisahau ile siku.Kabla ya kuingizwa rumande nilimuomba yule afande simu yangu ili niwasiliane na ndugu zangu wawe na taarifa,hakuwa na shida kabisa na alinipatia ile simu na akanitaka niongee nikiwa mle mle ndani ya kile chumba.
Basi baada ya kupewa ile simu,nilimpigia mwanangu mmoja tuliyekuwa tumeshibana sana aliyekuwa mpiga debe mwenzangu pale Sirari!.
Mimi "Nyamori mambo vipi?"
Nyamori "Mzee wa kuzugia mbona sikuoni kijiweni wewe!?"
Sasa kwa pale Sirari jina maarufu nilifahamikaga kama mzee wa kuzugia,hii ilikuja baada ya kila sentensi nitakayoongea nilikuwa naweka neno kuzugia au kuzuga na hii kitu nimekuwa nayo hadi leo hii,nadhani ni mazoea tu!.Sasa jamaa baada ya kupokea simu yeye alianza utani wake bila kufahamu kilichokuwa kinaendelea!.
Mimi "Mwanangu nimepata msala!"
Nyamori "Msala gani tena mzee?"
Mimi "Nipo hapa polisi mwanangu,kama vipi mje kunicheki!"
Nyamori "Haina noma mwanangu ngoja niwashitue wana"
Basi baada ya yale mazungumzo nikawa nimekabidhi ile simu tena kwa yule afande.
Kabla ya kuingizwa lupango,tulitakiwa kukabidhi kila tulichokuwa nacho,mimi mpaka muda huo sikuwa na chochote zaidi ya saa ya mkononi na waleti ambayo haikuwa na kitu zaidi ya makaratasi na tiketi za gari!.Basi kwa mara ya kwanza mwanaume nikaingizwa lokapu ambako baada ya kuingia niliona ni heri ukalazwa chooni wiki nzima lakini si mule ndani!.
Muendelezo > Sehemu ya 8
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Hakika ummy Mwalimu una kazi ongezeni hodi za kulaza wendawazimu hapo mirembeKwanini uchangiwe wakati unaandika kutuburudisha? Acha njaa. Andika watu tunapokuwa free tunaburudika. Unasema wajifunze wajifunze nini? Huwa nyie jamaa mnaandika andika hivi mnaanza kudhani kuwa mnatia material na watu wanahitaji wafaulu. So mnaanza kutumia IDs zenu nyingine kujipasia mfunge. Hilo suala la kukuchangia tukuchangie we unalipa kupost hapa? Umepewa bure toa bure. Acha kutaka kutapeli watu.
Mkuu huyu jamaa ni kweli hii story ni yake Na wala c ya kutunga maana misukosuko aliyokutananayo hawezi kushindwa kuvumilia kejeri za humuJamaa ni form six leaver halafu ni bodaboda na ana umri mdogo tu, lakini ana akili na busara kuliku mbumbumbu nyingi sana hapa JF zinazojitia kuwa ni wasomi na wamekula chumvi
Ukicheki anavyosimulia na anavyojibu wanaomdhihaki utagundua hilo
Sio yule utopolo mpwayungu village
Naelewa ni nini unazungumza kaka .Jamaa inaonesha ndo wale watu ambao maisha yao yapo straight yani mtu kasomeshwa shule ya msingi nzuri ,secondary nzuri kafaulu vizuri alilishwa vizuri na wazee ametafutiwa kazi nzuri ila kuna watu wanaraha sana haya maisha kila kitu wamefanyiwa kmmk [emoji16].
Sasa ndo unawakuta wanabisha tu kila kitu wakiambiwa hawaijui dunia wao ni school - chuo - kazini asubuh hadi jioni
Mimi nishapewa Mil1.5 kuna dili ilitakiwa tukamilishe yani ile ilikua kama kishawish tu yani chambo unavutwa moyo uingie mzima mzima kwenye game na hayakuwa malipo yani iyo fanya maandalizi yako ujitengeneze kimazingira ya kazi baada ya wiki nikapewa tena kama laki 4
Nilichokifanya nilikimbia na ile pesa moyo wangu haukuwa tayari kufanya ule mchongo kwaiyo kupewa pesa kabla ya kazi kwa ishu haramu ni kawaida
Ila ndugu zangu aya maisha bora usakwe na polisi unaweza pona ukaishia nyuma ya nondo sio wahuni
Now nipo free nilisha clear tofauti zangu na wahuni[emoji16]
Na watu huwa hawapendi kutumia akili. Wakidanganywa wanafilimbwa tu kama walivyofanywa na Kalyinda. Eti boda boda analaza 70,000 kwa siku? Jamani hawa watu hawa sijui wanatuonaje?Story za vijiweni hizo bro.
Utawasikia wakisema ukiwa na Bajaj tatu unalaza laki.
Sasa wewe nunua hizo Bajaj tatu wapelekee.
Wataondoa vitu original kwenye hizo Bajaj na kufunga feki vya China, baada ya miezi mitatu Bajaj Ni nyumba ya kuku.
Wahuni sio watu mkuu.
Kama kuna sehemu watanzania huwa wanapoteza muda na kulishana matango pori ni kwenye vimigodi uchwara, yaani unakuta wanaamini eneo husika kuna madini huku wakiendelea kupambana kwa nguvu na kupoteza pesa lakini mwisho wa siku wanaambulia patupu,na ndivyo ilivyokuwa hapo Nyasana, kuna muda unawaangalia ndugu zetu watanzania wanavyohangaika hadi huruma kwakweli,Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua nyumbani - 14.
Baada ya kumsubiri Mtatiro hapo Nyasura kwa muda hatimaye nae akawa amekuja akiwa anaendesha baiskeli,kiukweli kama kawaida nilipokuwa nikionana na jamaa yangu huyo utani wa hapa na pale pia furaha kwa kiasi fulani ilichukua nafasi.
Mtatiro "Mwanangu unazidi kung'aa tu,naona Tarime imekukubali"
Mimi "Aah wapi mwanangu ni kuridhika tu!"
Mtatiro "Vipi lakini kina Monche na washikaji wengine wazima?"
Mimi "Mwanao Monche sijamcheki muda mrefu,siunajua tena mimi zangu muda mwingi huwa ni Sirari tu!"
Mimi "Nadhani atakuwepo!"
Mtatiro "Jamaa huwa nampigiaga simu hadi leo haipatikani"
Mimi "Uenda atakuwa alibadili simu"
(Monche alikuwa ni yule dereva wa ile Hiace ambayo Mtatiro alikuwa akifanyia kazi kabla hajaondoka kwenda Mwanza,hivyo walikuwa washikaji).
Wakati tunaondoka hapo Nyasura kuelekea huko walipokuwa kina Mtatiro,tuliamua kutembea ili kuendelea kupiga stori maana ilikuwa ni muda umepita sijaonana na jamaa,ile baiskeli japo ilikuwa na Carier(sehemu ya kukalia)lakini tuliona ni vema tutembee huku mastori yakiendelea.
Tukiwa njiani niliamua kumwambia ukweli Mtatiro mambo yaliyokuwa yamenitokea kwasababu ukizangatia ni yeye ndiye aliyekuwa ameniunganisha na Gabriel.
Mtatiro "Jamaa sijaongea nae muda sana"
Aliendelea "Kwahiyo mlichomokaje?"
Mimi "We acha mwanangu!"
Mimi "Kuna jamaa anaitwa Eric ndiye aliyetuchomoa"
Mtatiro "Aah Eric nammanya mwanangu"
Aliendelea "Yule jamaa ndiye mwenye ile michongo na hata Gabriel ni mpambe tu!"
Mimi "Jamaa watakuwa wamemdaka maana baada ya kutoka Migori nilimtafuta lakini hapatikani!"
Mtatiro "Zile mishe zina njuruku(pesa) lakini ni hatari sana mwanangu,kila muda unakuwa macho kodo kama popo!"
Mimi "Mwanangu ninao mzigo kwenye begi!"
Mtatiro "Acha utani wewe!"
Mimi "Kwanini nikutanie!"
Mtatiro "Hebu tuone mwanangu!"
Nilishusha kile kibegi toka mgongoni nikawa nimempatia Mtatiro akawa amefungua na kutazama zile pesa ili ahakikishe nilichokuwa nakisema kama kina ukweli!.
Mimi "Hizo nilikimbia nazo kuingia Kenya ndo zimebaki!"
Mtatiro "Mwanangu hizi mbona zitatoka,we subiri uone!"
Basi baada ya mwendo mrefu huku tukiendelea kupiga mastori,Mtatiro akanitaka nipande kwenye baiskeli ili apige pedo(aendeshe) kwasababu bado kulikuwa kuna umbali tulipokuwa tukienda!
Baada ya muda tukawa tumefika hapo Kijijini ambako aliniambia kulikuwa na mgodi umetema,kiukweli palikuwa ni kijijini ambako hakukuwa pabaya sana maana karibia huduma zile muhimu zilipatikana hapo!.
Tulifika kwenye mji mmoja ambao ulikuwa na nyumba mbili za nyasi, Mtatiro akawa ameingiza baiskeli ndani akanitaka niweke lile begi ndani, akafunga ule mlango na kufuli akawa ameniambia tuelekee hapo kwenye hicho kimgodi!
Baada ya kufika pale mgodini tulikuta raia wanapambana kuchimba mashimo, kuna wengine walikuwa wamechimba mashimo marefu kiasi kwamba walikuwa hawaonekani, kuna ambao bado nilikuta waking'ang'ana kuchimba huku mashimo yakiwafika magotini!
Kiukweli kulikuwa na watu wengi sana huku kina mama wakiwa wanahangaika kubeba vifusi kwenye makarai na ndoo wakirundika mchanga kila mtu kwenye eneo aliloona kwake litakuwa salama kabisa.
Mtatiro alinipeleka mpaka kwenye shimo alimokuwa kaka yake na jamaa mmoja wakiendelea kuchimba,ile kazi ya uchimbaji haikuwa ya kitoto maana kulikuwa na vikokoto mshenzi kama vyote.
Sasa kwakuwa nilikuwa hapo ili kujaribu bahati yangu kwa upande huo wa madini,baada ya kumpa Hi brother ake Mtatiro nilikamata ndoo nikawa nasogeza ule mchanga pembezoni ya lile shimo!.Ile kazi tuliifanya hadi mida ya saa 3 usiku ndipo yule brother akasema tuondoke tukapumzike halafu kesho yake tungedamka mapema kuendelea!
Kiukweli familia ya kina Mtatiro haikuwaga na mambo mengi, nilichokuja kugundua ilikuwa ni familia yenye upendo sana,sema ndiyo hivyo tu hawakujaliwa kuwa na pesa!
Ukweli ni kwamba,jamii yangu ya kikurya ni jamii ambayo huwa ina upendo na kuwajali watu wengine pia,ukiachilia tu yale madhaifu madogo madogo kama wanadamu wengine lakini wakurya ni kabila bora sana miongoni mwa makabila bora kwenye hii nchi!,yale madhaifu madogo madogo ya kupiga mwanamke, kukeketa na kuchinjana ovyo yalikuwaga ni kwasababu ya ukosefu wa elimu tu, sikuhizi hayo mambo kwa Tarime yamepungua na kama siyo kuisha kabisa baada ya watu kuelimika!
Tarime ni njema sana na atakaye na aende akajionee!.(Nilikuwa nachomekea tu ndugu zangu).
Tulipofika hapo nyumbani kwakuwa tulikuwa wanaume tupu,tulikoka moto tukaanza kupika ugali ambao tulikula na dagaa zilizokuwa zimepikwa mchana!
Namshukuru Mungu kulipokucha asubuhi Mtatiro alinipatia nguo zake ambazo zilikuwa zimechoka ili nivae twende tukapige kazi!.Kiukweli nilipofika hapo mgodini hiyo asubuhi tulikuta nyomi la watu kila mtu akiwa anapambana kwa upande wake!.Kama kawaida na sisi tukaanza kazi iliyotupeleka hapo,nikiwa nimekaa nasubiri udongo ili niupeleke maeneo husika,simu yangu ilianza kuita,ile nimeitoa mfukoni na kutazama nikakuta ni Da'Sarah alikuwa akinipigia!
Da'Sarah "Mdogo wangu uko wapi?"
Mimi "Nisamehe Dada jana sikuwa na Vocha nikashindwa kukwambia niliteremkia hapa Bunda!"
Da'Sarah "Bunda tena umeenda kufanya nini!?"
Mimi "Hivi wale watoto wa mzee Marwa bado unawakumbuka?"
Da'Sarah "Marwa yupi?,yule jirani?"
Mimi "Eeh"
Da'Sarah "Mi namkumbuka yule mwanajeshi tu Ryoba"
Mimi "Sasa yupo mdogo wao ambae ni rika langu na ni rafiki yangu anaitwa Mtatiro,nilipita kumsalimia kaka yake anaumwa,alinipigia simu jana nikiwa kwenye gari nakuja hivyo nikaona niteremke kuja kumjulia hali!"
Niliamua kumdanganya dada yangu sababu ya mimi kuteremka pale Bunda ni kwenda kumuona kaka yake Mtatiro ambaye alikuwa mgonjwa ili asiendelee kunifikiria vibaya!.
Da'Sarah "Kwahiyo unakuja lini Mwanza!"
Mimi "Najitahidi dada nitawahi"
Da'Sarah "Uwahi kuja maana niliongea na shemeji yako akaniambia kuna muhindi alikuwa anatafuta mtu wa kusimamia boti zake za uvuvi"
Aliendelea "Siyo tumpange mtu kumbe na wewe huko una mambo yako!"
Mimi "Sawa dada nakuja"
Shemeji yangu alikuwaga akifanya kazi za uvuvi na yeye pia alikuwaga na mitumbwi yake kadhaa kwa ajili ya shughuli yake hiyo.Baada ya yale mazungumzo kazi zikaendelea kama kawaida,sasa lile eneo lilikuwa maarufu sana kama Nyasana Mgodini,kiumweli ni eneo lililokuwa limechanganya sana lakini jambo la ajabu hakukuwa na madini wala nini, maana Mtatiro alikuwa ananiambia wao wapo pale ndani ya mwezi na hakuna walichoambulia zaidi ya kupoteza hela tu!.
Mtatiro "Mwanangu hapa napo ni hasara tu,kila siku mara utasikia kuna kimkanda kimepita hapa,watu wakichimba kwenye hicho kimkanda hawaambulii kitu!"
Mimi "Kwani mlianza kuchimba lini?"
Mtatiro "Mimi nimekuja mwezi uliopita,lakini kina braza hapa wana miezi miwili,ndani ya miezi yote hiyo hawajawi hata kupata punje ya dhahabu!"
Mimi "Duuu!,mbona ni hatari"
Mtatiro "Kuna jamaa wao ndiyo walidai kuna mkanda umepita chini kutokea Geita,sasa watu wote hawa unao waona wanapambana kuutafuta mkanda!"
Mimi "Hakuna watu waliopata dhahabu hata mara moja?"
Mtatiro "Watu wanadai wanapata pata kimtindo lakini ukijaribu kuuliza waonyeshe walizopata hata huonyeshwi"
Aliendelea "Nishamshauri braza tuachane na hii biashara kichaa lakini hasikii,yeye bado anaamini kuna madini"
Kama kuna sehemu watanzania huwa wanapoteza muda na kulishana matango pori ni kwenye vimigodi uchwara, yaani unakuta wanaamini eneo husika kuna madini huku wakiendelea kupambana kwa nguvu na kupoteza pesa lakini mwisho wa siku wanaambulia patupu,na ndivyo ilivyokuwa hapo Nyasana, kuna muda unawaangalia ndugu zetu watanzania wanavyohangaika hadi huruma kwakweli, lile eneo ilikuwa inasemekana dhahabu ililipuka tu na watu wakaanza kujaa kwa wingi na kuanza kuchimba, sasa sikujua kama kuna wataalamu waliwahi kupima uwingi wa dhahabu ulioko pale ama la!.(Sijui kama hadi leo huo mgodi unafanya kazi).
Kuna muda tulikuwa tunatoka na mtatiro tunaingia mtaani kule kijijini tunabadili zile hela,tulipoona chenji kijijini hapo imekuwa ngumu tulikuwa tunaelekea pale senta ya Nyasura kupambana na ubadilishaji wa kununua bidhaa halisi na kurudishiwa chenji halali!.Kiukweli ile hela ikabaki chache sana!.
Kuna siku tukiwa tumetoka na Mtatiro tukiwa maeneo ya Bunda mjini kwenye mishe mishe hizo,simu yangu ikapigwa ikiwa ni namba ngeni!.
Mimi "Halloo"
Yeye "Mambo Umughaka"
Mimi "Poa,nani!"
Yeye "Hebu acha utani,kwahiyo namba yangu ushafuta!"
Muendelezo > Sehemu ya 15
Kabisa.... Zilizopo hazitoshi. 🤣[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Hakika ummy Mwalimu una kazi ongezeni hodi za kulaza wendawazimu hapo mirembe
Halafu cha kushangaza, jamaa huwa hawana mawazo ya KUSHTUKA, na kurudi nyuma! Kila siku wanajua watapata kesho!Kama kuna sehemu watanzania huwa wanapoteza muda na kulishana matango pori ni kwenye vimigodi uchwara, yaani unakuta wanaamini eneo husika kuna madini huku wakiendelea kupambana kwa nguvu na kupoteza pesa lakini mwisho wa siku wanaambulia patupu,na ndivyo ilivyokuwa hapo Nyasana, kuna muda unawaangalia ndugu zetu watanzania wanavyohangaika hadi huruma kwakweli,
Nyie ndio wabishi kwa kuona bodaboda ni kazi ya chini wakati kuna watu wanalea familia, wamejenga sababu ya bodaboda. Kweli siku haziwezi kufanana lakini bodaboda ina hela sana kama mtu yupo serious na kazi yake. Kinachowaponza bodaboda na bajaji ni ulevi, bangi, umalaya na kamali ndio zinaishia hela zao na madeni juu. Sibishi mimi kazi yangu ilikuwa pembeni kijiwe cha bodaboda nilijifunza mengi sana kuwahusu.Na watu huwa hawapendi kutumia akili. Wakidanganywa wanafilimbwa tu kama walivyofanywa na Kalyinda. Eti boda boda analaza 70,000 kwa siku? Jamani hawa watu hawa sijui wanatuonaje?
Pole KWA msiba bro.......nakuappreciate SANA unasimamia msimamo wako huyumbishwi na maneno ya watu barikiwa SANA japo yawezekana wengine tusiweze kukulipa lakini Tunaomba MUNGU akusimamie katika shughuli zako milango ya neema na baraka ikapate kufunguliwa katika kila hatua unayopitiaWakuu habari za leo?
Bila shaka nyie ni wazima kabisa ndugu zangu,poleni sana,Aisee nimetoka kidogo nje ya mji nipo mkoani tulileta Msiba,hivyo nisubirieni nikirudi nakuja kuendelea na kumalizia sehemu kidogo iliyobaki!.
Pia niwatoe hofu hakuna mtu yeyote aliyenitisha wala kuzuia eti nisisimulie,hilo wala lisiwape tabu!.
Vilevile nimejaribu kupitia comments za watu nimeona positive na negative opinions,hii ndiyo akili ya mwandamu siku zote,ukipenda tu usifiwe katika maisha basi wewe utakuwa na matatizo ya utindio wa ubongo!,mimi niendelee kuwaomba watu wanaotoa negative comments wala wasitukanwe na kukejeliwa!,acheni nao waji mwaye mwaye kwa kutumia uhuru vizuri wa kutoa maoni!.
Nilisema nia na lengo ni kufundisha watu,wengine haya ndiyo yalikuwa maisha yetu enzi hizo.
Narudia tena kuwaambia ya kwamba mimi kazi yangu ni bodaboda na napatikana bunju,yeyote anayetaka kuonana na mimi kuja kijiweni napo paki bodaboda yangu basi aje pm nimtumie namba anitafute nimuelekeze aje anione tupige stori,sasa mkiendelea kubisha ya kwamba mimi si bodaboda hiyo haisaidii kwasababu utakuwa ni mjinga tu unayetaka kubisha bila sababu ya msingi wakati mimi muhusika nipo bunju tu hapo ambapo unaweza kufika ili ubishi wako uishe!.Kama nilikuwa mpiga debe ni kitu gani kinizuie kuendesha bodaboda?,mimi sichagui kazi wakuu ili mradi iwe halali,sasa hivi sitaki kuiba cha mtu!.
Mimi kuandika vizuri ndiyo ikufanye uamini mimi si bodaboda?.Kupanga ni kuchagua.
Vumililieni narudi mjini kesho kutwa,nikifika naendelea ndugu zangu!.
Unakula samaki mtamu kumbe amevuliwa kwa njia za uchawi.Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua nyumbani - 16.
Shemeji yangu kiukweli alikuwa na pesa isiyokuwa ya kawaida,hakuwa tajiri sana kiasi ambacho kingemuingiza miongoni mwa matajiri wa pale Mwanza, lakini alikuwa na uwezo na utajiri wa size ya kati!,nyumba aliyokuwa anakaa yeye na mkewe(dada Sarah)ilikuwa ya kwake ambayo aliijenga kwa fedha yake mwenyewe,pia alikuwa akimiliki gari aina ya Nissan Patrol Nyeusi.
Pia alikuwa ni mtu fulani aliyekuwa na viprinsipo vyake ambavyo kama ulikuwa hujamuelewa ungeona kama ni mateso kuishi nae,pesa yake mpaka ifikie hatua umeila basi ilikupasa umenyeke sana na jasho likutoke ki kweli kweli!.Hivyo hata wakati ananipeleka pale mwaloni na kumwambia yule bwana kwamba ningekuwa miongoni mwa wavuvi,nilikuja kumuelewa baadae maana mwanzo nilidhani kama alikuwa akinishushia heshima na kunidharau!.
Kwakuwa tulifika hapo Ijinga mida ya saa 10 jioni,yeye bwana shemeji baada ya kuwapa maelekezo wale jamaa na kuwaachia alicho waachia,aliondoka akatuacha.Sasa nilipouliza jamaa ameenda wapi yule jamaa aliyenipokea akadai anaelekea kwenye miradi yake mingine ambayo hata sikuifahamu!.
Wakati nimefika hapo sikufahamu kumbe kuna eneo jamaa walikuwa wakiendelea na mapishi bhana,sasa jamaa niliyekabidhiwa kwake alinichukua akanitaka tusogee pembeni kidogo ambako kulikuwa na kibanda cha mabanzi na nyasi,nilipofika hapo nikakuta kundi la watu 7 wakiwa na miili iliyokuwa imejengeka vizuri kimisuli!,jamaa walikuwa wamevaa bukta tu huku vifua vikiwa wazi.Mimi pamoja na kakitambi kangu kalikokuwa kameanza kuchomoza kwa ajili ya beer na fedha haramu,nilijiona kwa wale jamaa siyo kitu kabisa kwa namna walivyokuwa wamejazia misuli!.Jamaa mmoja wapo kwenye wale watu nilisikia anamwambia yule jamaa niliyekuwa nae ya kwamba "Waukae angalia usije ukalala njaa!".Kumbe yule jamaa niliyekuwa nae hilo ndilo lilikuwa jina lake,sasa sikuelewa kama ndilo alilopewa na wazazi wake au lilikuwa jina tu alilopewa na wale jamaa!.
Waukae "Aisee kazi mpya hii!"
Jamaa 1 "Ooh karibu mwanangu,huku ndiko nyumbani kwetu!"
Jamaa 2 "Town tulishakusahau,makazi yetu ni pamoja na samaki mwanangu!"
Wakati huo walikuwa wamekaa wamezunguka sufuria kubwa lililokuwa limefunikwa kwenye sinia kichwa chini miguu juu!,kuna jamaa mmoja alinyanyuka akaelekea ndani kwenye kile kinyumba akatoka na samaki 3 wakubwa ambao walikuwa kambale,samaki wale walikuwa wa kuchoma!,kumbe wao walishindwa kula muda ule walikuwa wakipiga stori wakimsubiri huyo Waukae.Jumla yetu pale ikafanya tukawa watu 9.
Tukauzunguka ule ugali na ndipo lile sufuria likafunuliwa,aisee sikuwahi kushuhudia ugali wenye ukubwa ule toka nizaliwe,hiyo ndiyo ilikuwa mara ya kwanza kuona ugali uliokuwa mkubwa kwa kiwango kile,wale samaki wakawekwa chini kwenye mfuko na kazi ya kuanza kufukuzana na matonge ikaanza rasmi!,mimi nilikula sana samaki kwakuwa nilikuwa nina hamu nao sana maana wakati nikiwa Sirari chakula changu kikubwa ilikuwa nyama na kichuri!.
Baada ya kushiba nilijisogeza kando nikawaacha jamaa wakiendeleza libeneke!.
Jamaa 1 "Mwanangu mbona unakimbia"
Mimi "Mwanangu niko fiti!"
Jamaa 2 "Huyu hana njaa muda bado!"
Ile kauli ya yule jamaa wa pili sikuielewa kwa wakati ule lakini kwa baadae ilikuwa na maana kubwa sana kwangu!.Niliondoka zangu nikaelekea ziwani kwenda kunawa mikono!..
Walipomaliza kula ugali ambao haukubaki hata punje,ndipo kila mtu alinyanyuka na kuendelea na mambo yake,mimi niliendelea kushangaa kwa kuwa ndiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza kufika ziwani kabisa na kusogelea maji ya ziwani,mara zote nimekuwa nikiliangalia lile Ziwa Victoria kwa mbali tu na sikuwahi kabisa kulisogelea kwa karibu hadi kuyagusa maji yake!.
Ilipofika mida ya saa 12 jioni niliona wale jamaa wakianza kubeba nyavu pamoja na makarabai na kupelekea kwenye ile mitumbwi,zoezi lile lilifanyika kwa haraka na ndipo wengine wakawa wanavaa masweta na nguo za kazi,kuna jamaa wengine wao walibaki kama walivyokuwa tu hapo awali!. Baada ya muda giza nalo likaanza kutanda,ndipo Waukae akawa ameniambia nivue suruali nibaki na bukta pamoja na tisheti kisha nizame kwenye mtumbwi!. Sasa kumbe ile mitumbwi mingine niliyoiona ilikuwa ya watu wengine,wale jamaa tuliokuwa tunakula nao pale,waliokuwa wafanyakazi wa shemeji walikuwa 4,hivyo ukiniweka mimi pamoja na Waukae tulikuwa jumla 6,wale wengine walikuwa wa mitumbwi mingine!.
Tuligawana watu watatu kwa kila mtumbwi na kisha ikawashwa tukaondoka!.Hakuna siku ambayo sitokuja kuisahau kama hiyo maana ndiyo ilikuwa siku yangu ya kwanza kupanda mtumbwi pia ilikuwa siku ya kwanza kusafiri ziwani,muda huo kiukweli ziwa lilikuwa limetulia sana na hakukuwa na mawimbi.Baada ya mwendo mrefu kuelekea katikati ya ziwa Victoria,nilikuwa nikigeuka nyuma naziona taa za pale kijijini mwaloni kwa mbali sana,pia kwa umbali ule ilifanya tukawa tunaona mianga ya taa kutoka vijiji vingine vilivyokuwa kando ya ziwa!.Baada ya kufika walipoona panafaa kushusha nyavu,zile boti zilizimwa injini,kulikuwa na utulivu wa hali ya juu sana wakati huo,mawazo yangu yalikuwa yanakwenda mbali zaidi na kujikuta nawaza endapo tukizama itakuwaje,lakini kwa upande wa wale jamaa wao hawakuwa na hofu kabisa!.
Zile nyavu zikaanza kushushwa taratibu kutoka kwenye ile boti yetu,nyavu zilipokwisha kushushwa zote,ndipo nilimuona Waukae anachukua kopo moja kubwa la Toss(ambalo lilikwisha sabuni) lilikuwa na maji ndani yake akalifungua kisha akawa anachota yale maji kwa mkono kisha anayatupa ziwani huku akinuia jambo fulani!,sasa kwakuwa nilikuwa mtu mzima niligundua ya kwamba ile ilikuwa ni dawa na alichokuwa kuwa anafanya ni kama vile walipewa masharti na mganga,lile jambo lilikuwa likifanyika siku zote ambazo nilikuwa hapo Mwaloni na ilikuwa ni lazima lifanyike!.Na hata ule mtumbwi mwingine pia lilifanyika jambo hilo!.
Baada ya hapo tulitulia humo ndani ya mitumbwi hadi mida ya saa 10 usiku,sasa mimi nilifahamu ya kwamba tukishatupa zile nyavu tungerudi mwaloni hadi kesho yake ndipo kazi ifanyike kumbe haikuwa hivyo!.Ilipofika mida saa 10 usiku ndipo tukaanza kuvuta zile nyavu!,nilichokuja kugundua ni kwamba,wale jamaa hawakujazia ile miili yao misuli kwasababu ya kunyanyua nondo(vyuma vya Gym)bali walijaza kwasababu ya kuvuta zile nyavu!,aisee asikwambie mtu,ingawa kulikuwa kuna baridi na hali ya hewa isiyokuwa ya joto lakini mimi nilichuruzika jasho kama nilikuwa nakimbizwa!.
Mahala popote ukiwa unawaona wavuvi nakuomba wapigie saluti,ile kazi haikuwa ya kitoto kama watu wazaniavyo!.
Basi baada ya kuvuta zile nyavu kwa muda,ndipo na samaki nao waliokuwa wamenaswa na zile nyavu wakaanza kujitikisa na kurukaruka!,kwa upande wangu niliendelea kushangaa sana kwasababu ilikuwa ni kitu kipya!.Hiyo siku tulipata samaki wengi sana na kitu ambacho niliendelea kukishangaa sana ni kitendo cha kumvua samaki aina ya Sangara mwenye ukubwa na kimo kama cha mtoto wa miaka 6.Niliuliza nikaambiwa huyo ni cha mtoto,kuna siku huvuliwa Sangara mwenye kimo cha mtu mzima ingawaje huwa ni mara chache lakini hutokeaga!.
Ilipofika mida ya saa 12 asubuhi baada ya kuifanya ile kazi kwa muda mrefu,mashine ziliwashwa na kurudi mwaloni huku tukiwa na rundo la samaki wakubwa na wadogo!.Tulipofika Mwaloni tulikuta kulikuwa na gari kubwa ambalo lilikuwa rasmi kwa ajili ya kubeba na kuhifadhi samaki!.Haukupita muda nikawa nimemuona na shemeji pia!.
Tuliwashusha wale samaki kwenye chombo kisha wakawa wanapimwa uzito,waliokuwa wakubwa wa size iliyotakiwa waliipakiwa kwenye ile gari,na waliobaki waliwekwa kwenye madumu kisha kuna land-rover lilikuja kuwachukua!.
Baada ya kuifanya ile kazi kwa muda wa mwezi mmoja nikaanza kuizoea,sasa kuna siku nikawa napiga mastori na Waukae ambaye tayari alishakuwa mtu wangu wa karibu sana!.Wao ilipofika mwisho wa Mwezi walikuwa wakilipwa kwa makubaliano walioyafahamu wao,lakini mimi sikulipwa chochote,sasa nikafahamu uenda shemeji atakuwa anampatia Dada pesa yangu anihifadhie,uenda alidhani angenipatia ningeitumia katika ulevi na uzinzi uliokuwa umekithiri pale kisiwani,kilichokuwa kinanisaidia ilikuwa ni ile hela yangu ambayo bado nilikuwa nayo.
Waukae "Unadhani bila vile utapata samaki!?"
Aliendelea "Utarudi na mitumbwi ikiwa inakukodolea macho!"
Mimi "Kwahiyo ni kila mtu mwenye mtumbwi anafanya?"
Waukae "Ni ujanja wako tu,wapo ambao wanamtegemea Mungu lakini huwa hawasaidii wanaishia kupata hasara na kuuza injini!"
Mimi "Kwani Injini inauzwaje!"
Waukae "Injini ipi sasa,maana kuna hiyo Yamaha na Honda!"
Mimi "Kwani zinatofautiana bei!?"
Waukae "Hiyo Yamaha ina bei yake na Honda pia ina bei yake"
Mimi "Nzuri ni ipi kaka?"
Waukae "Yamaha ina sipidi ila Honda ina nguvu na hata bei yake imesimama"
Ile mitumbwi ya shemeji yeye alikuwa amefunga injini za Honda,lakini mitumbwi karibia mingi ilikuwa na injini za Yamaha!.
Waukae "Yaani hapa bila dawa unadhani unatoboa!"
Aliendelea "Hivi Masangara ni shemeji yako kabisa eti!"
Mimi "Masangara ndiyo nani?"
Baada ya kuuliza Masangara ndiyo nani yule jamaa akaanza kucheka sana kana!.
Waukae "Sisi tunamjua kwa jina la Masangara"
Mimi "Ni shemeji yangu ila hilo jina sikuwahi kulifahamu"
Waukae "Huku watu wanamjua kwa jina hilo"
Waukae alikuwa ni msukuma bila hata kuuliza kwasababu ongea yake na rafudhi yake vilitosha kukuaminisha pasipo shaka!.
Baada tena ya kupiga kazi kwa mwezi mmoja uliofuata wenzangu wakalipwa hela nzuri tu lakini kwangu ikawa hola!.Sikuelewa sababu za shemeji kutokunilipa ilikuwa ni nini wakati nilikuwa nafanya kazi sawa na akina waukae!.
Niliamua kuweka vocha kwenye kiswanswadu changu na kumpigia Dada Sarah na kujifanya namsalimia ili nione uenda angeniambia shemeji huwa anamuachia hela yangu!,baada ya mazungumzo nikaona yuko kimya sikutaka kumuuliza maana niliona nikimuuliza na akajua kumbe mumewe anipatii chochote ingeleta shida katika mahusiano yao,ingeonekana nimekwenda pale kuwachonganisha, hivyo nikaamua kukaa kimya!.
Ndani ya mwezi huo nilipokuwa nimejifunza na kuielewa ile kazi na namna ilivyokuwa inapesa ndefu, niliamua kumpigia simu Mwanangu Mtatiro.
Muendelezo > Sehemu ya 17
Tunamshukuru umetutoa hofy mkuuWakuu habari za leo?
Bila shaka nyie ni wazima kabisa ndugu zangu,poleni sana,Aisee nimetoka kidogo nje ya mji nipo mkoani tulileta Msiba,hivyo nisubirieni nikirudi nakuja kuendelea na kumalizia sehemu kidogo iliyobaki!.
Pia niwatoe hofu hakuna mtu yeyote aliyenitisha wala kuzuia eti nisisimulie,hilo wala lisiwape tabu!.
Vilevile nimejaribu kupitia comments za watu nimeona positive na negative opinions,hii ndiyo akili ya mwandamu siku zote,ukipenda tu usifiwe katika maisha basi wewe utakuwa na matatizo ya utindio wa ubongo!,mimi niendelee kuwaomba watu wanaotoa negative comments wala wasitukanwe na kukejeliwa!,acheni nao waji mwaye mwaye kwa kutumia uhuru vizuri wa kutoa maoni!.
Nilisema nia na lengo ni kufundisha watu,wengine haya ndiyo yalikuwa maisha yetu enzi hizo.
Narudia tena kuwaambia ya kwamba mimi kazi yangu ni bodaboda na napatikana bunju,yeyote anayetaka kuonana na mimi kuja kijiweni napo paki bodaboda yangu basi aje pm nimtumie namba anitafute nimuelekeze aje anione tupige stori,sasa mkiendelea kubisha ya kwamba mimi si bodaboda hiyo haisaidii kwasababu utakuwa ni mjinga tu unayetaka kubisha bila sababu ya msingi wakati mimi muhusika nipo bunju tu hapo ambapo unaweza kufika ili ubishi wako uishe!.Kama nilikuwa mpiga debe ni kitu gani kinizuie kuendesha bodaboda?,mimi sichagui kazi wakuu ili mradi iwe halali,sasa hivi sitaki kuiba cha mtu!.
Mimi kuandika vizuri ndiyo ikufanye uamini mimi si bodaboda?.Kupanga ni kuchagua.
Vumililieni narudi mjini kesho kutwa,nikifika naendelea ndugu zangu!.