Denis Lucas Shio
Member
- Aug 2, 2022
- 60
- 75
Habari wanajukwaa, kwa majina naitwa Yasini Yakubu ni muhitimu wa katika Shahada ya Uhasibu na Fedha mwaka 2016 katika moja kati ya Chuo Kikuu kilichopo Wilaya ya Moshi Mjini Mkoani Kilimanjaro na baada ya kuhitimu nilitumia miaka takribani mitano mpaka kufanikiwa kupata Ajira.
Baada ya kutunukiwa Shahada ya Uhasibu na Fedha nilianza kufuatilia matangazo ya nafasi za ajira mpya zilizokuwa zinatangazwa na niliaambia baadhi ya Ndugu, Jamaa na Marafiki wanitafutie ajira au kama wakisikia sehemu kuna nafasi za Ajira nimetangazwa zinazohusiana na kozi niliyosome basi wanipatie taarifa ili niweze kutuma maombi ya kutaka Ajira. Nilituma maombi ya Ajira katika Taasisi na Kampuni mbalimbali za Serikali na zisizo za Serikali kwa kipindi cha mwaka mmoja na nilifanikiwa kuitwa kwenye usahili wa Ajira mbalimbali lakini sikufanikiwa kuajiriwa.
Baada ya kuhangaika kutafuta Ajira kwa mwaka mzima bila mafanikio yoyote, sikikata tamaa niamua kuwasiliana na Rafiki yangu aliyekuwa anaishi Dar es Salaam na kumtaharifu kuwa ninataka kuja Dar es Salaam kutafuta Ajira lakini sina sehemu ya kufikia nitafikia kwake. Rafiki yangu alikubali ombi langu hivyo nikaawaaga Wazazi wangu na Kuwaaharifu kuwa nitaondoka kwenda Dar es Salaam kwa Rafiki yangu kutafuta Ajira. Wazazi Wangu walikubali na kunipa baraka zote nilijiandaa na kesho yake alfajiri na mapema nilipanda basi kuelekea Dar es Salaam kwa rafiki yangu.
Baada ya kufika Dar es Salaam niliangaika kutafuta Ajira na kuhudhuira Usahili wa ajira kwa Mienzi kadhaa bila mafanikio yoyote. Rafiki yangu alinishauri nitafute biashara ya kujishikiza angalu hata niweze kujiingizia kipato kidogo huku nikiendelea kutafuta Ajira. Nilikubali ushauri wa rafiki yangu lakini nikamwambia kuwa sina mtaji wa kuanzisha hata hiyo biashara ndogo, Rafiki yangu aliniambia haina shida alinipatia mtaji na alinishauri niafanye biashara ya kuuza maji pamoja na soda kwenye moja kati ya vituo vya daladala.
Nilianza biashara na kwa bahati nzuri biashara ilikuwa inaenda vizuri licha ya kipato nilichokuwa naingiza katika biashara kilikuwa ni kidogo lakini kilinisaidia kutatua baadhi matatizo madogomadogo madogomadogo huku nikiendelea kutafuta Ajira. Wazazi Wangu waliposikia kuwa ninauza maji na soda katika kituo cha daladala walifadhaika kwa kuwa mtoto wao walionisomesha kwa gharama kubwa lakini mwisho wa siku nimeishia kuuza maji pamoja na soda kwenye kituo cha daladala na wakati mwingine walinipigia simu na kunitaka niachane na kazi hiyo nitafute kazi nyingine.
Niliendelea na biashara yangu kwa kipind cha mwaka mmoja na nusu ingawa haikuniletea faida kubwa lakini ilinisaidia kujichanga na watu mbalimbali na baadae nilikutana na tajiri mmoja akaniuliza kama nina leseni ya kuendesha gari anipatie kazi ya udereva wa teksi. Kwa bahati nzuri nilikuwa ninaweza kuendesha gari na kwa bahati mbaya nilikuwa sina leseni ya udereva. Lakini nilimuomba anipatie muda nifuatilie leseni ya udereva. Yule tajiri alikubali na kunipatia mawasiliano yake akaniambia nikipata leseni nimtafute. Nilianza harakati za kutafuta leseni na baada ya wiki kadhaa kupita nilifanikiwa kupata leseni ya kuendesha gari na kumatafuta yule tajiri aliyeniambia nimtafute nikishafanikiwa kupata anipatie kazi ya udereva teksi na aliinita akanipa mkataba wa kazi na kuusoma kisha tukasainishana na kukabithiwa gari ambayo nitakuwa nafanyia kazi. Nilianza Kazi ya Udereva teksi huku nikiwa naendelea kutafuatilia matangazo ya Ajira mpya zilizokuwa zinatangazwa na kutuma maombi ya kutaka Ajira katika makampuni mbalimbali ya watu binafsi pamoja na serikalini.
Nikifanya kazi ya udereva teksi kwa bidii kubwa mno lakini changamoto kubwa niliyokuwa nakumbana nayo ni kutokuifahamu vizuri ramani ya jiji la Dar es Salaam hivyo nilikuwa nikiwaomba wateja wangu wanielekeze vizuri njia kwa sababu mimi ni mgeni sizifahamu njia vizuri na muda mwingine nilisaidiwa na ramani za mtandao. Wazazi wangu waliposikia kuwa nimekuwa Dereva wa teksi walifadhaika kwa sababu wamenisomesha kwa gharama kubwa lakini mwisho wa siku nimeishia kuwa Dereva wa teksi na muda mwingine walinipigia simu kunitaka niachane na kazi hiyo nitafute kazi nyingine ya kufanya.
Sikukata tamaa na niliendelea na kazi ya udereva teksi kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu huku nikiendelea kutafuta Ajira nyingine bila ya mafanikio yoyote. Baadae niligundua kuwa kuna baadhi ya Wateja wangu wa teksi ni viongozi katika Taasisi na Kampuni mbalimbali za serikali na zisizo za Serikali. Hivyo nilichangamkia fursa nikawa natembea na Vyeti vyangu kwenye gari na nikanza kujenga karibu wa kuongea na Wateja Wangu na muda mwingine nikawa nawaambia kuwa mimi ni Muhitimu wa Chuo Kikuu katika Shahada ya Uhasibu na Fedha na ninatafuta Ajira na ninawapa vyeti vyangu pamoja na wasifu binafsi na kuwaomba kama kuna nafasi za kazi katika Kampuni au Taasisi wanazoziongoza wanipatie nafasi hiyo na kuwashawishi kuwa nipo tayari kufanya kazi katika mazingira ya aina yoyote.
Niliendelea kufanya hivyo kwa kipindi cha mienzi sita bila mafanikio yoyote lakini siku moja nilimpata mteja mmoja kama ilivyokuwa kawaida yangu nilianzisha maongezi na yule mteja na baadae nilimuonesha Vyeti vyangu na kumuelezea kuwa mimi ni muhitimu wa Shahada ya Uhasibu na Fedha na muda mrefu nimekuwa nikitafuta Ajira bila mafanikio, Hivyo basi kama kuna nafasi ya Ajira au ikitokea nafasi ya Ajira katika Kampuni anayofanyia kazi basi naomba anipe taharifa kwani nipo tayari kwa usahili na kufanya kazi katika mazingira ya aina yoyote. Yule Mteja alimaliza kupitia Vyeti vyangu akaniambia nisijali kwanza amevutiwa na utendaji wangu wa kazi maana nilikuwa makini katika kazi yangu ya udereva teksi na nina uwezo mzuri wa kuwasiliana na Wateja Wangu vizuri. Halafu akaniambia yeye ni Mkurugenzi wa Benki na kuna nafasi kazi mbalimbali katika Benki anayofanyia kazi zimetoka lakini sio za hapa Dar es Salaam ni Mkaoni Kilimanjaro na kuniambia kuwa kama nipo tayari nijaandae na Usahili wiki ijayo. Nikamwambia nipo tayari kufanya usahili na kufanya kazi katika mazingira ya aina yoyote. Hivyo basi alinipatia mawasiliano yake na kunitakia kila la Kheri.
Nilimshukuru Mungu, na nikamuomba anisimamie niweze kufaulu katika Usahili. Nilijiandaa na Usahili na kusafiri kwenye Mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya Usahili na siku ya Usahili ilipofika nilijitahidi kufanya vizuri na nifanikiwa kufaulu katika Usahili na hatimaye nilipewa mkataba wa Ajira na kuanza kazi mpya rasmi kama Mhasibu wa Benki. Nilimshukuru Mungu kwa mara nyingine na kumshukuru kila mmoja aliyekuwa nyuma yangu kwa kunishika mkono na namna yoyote ile. Vilevile Wazazi wangu sasa wanajivunia kuwa mtoto wao walionisomesha kwa gharama kubwa nimefanikiwa kupata Ajira.
Kwa kumalizia, Ninawashauri Wahitimu wa Vyuo waachane na mitazamo ya kuchagua kazi na badala yake watafute kazi au biashara yoyote ya kujishikiza ili wajiingizie kipato hata kama ni kidogo huku wakiendelea kutafuta Ajira Serikalini au kwenye Taasisi au Kampuni za Watu binafsi zinazohusiana na fani walizosomea, Pia siku zote katika maisha tukiwa kama Binadamu hatupaswi kukata tamaa, tuishi na Watu vizuri kwani hatuwezi jua ni nani ambaye kesho atakushika mkono kukuvusha kutoka hapa tulipo na kwenda hatua nyingine ya maisha yenye mafanikio zaidi.

Upvote
43