Nilivyoumbuka kwenye swimming pool

Sasa baada ya kukamuliwa tumbo na kutemeshwa maji ya swimming pool niliyoyanywa pasipo kupenda ndo akili ikanikaa sawa nakuanza kuona watu wote walionizunguka walivyokuwa wakinishangaa mimi badala ya kuyashangaa maji yaliyotaka kuniua!.
Unakumbuka ladha ya maji ilikuwaje Mkuu? tangu tafiti zishindwe kubaini swimming pool ikijazwa lita 40,000 asubuhi jioni inajikuta ina lita 45,000 bila kuingiziwa maji mengine niliacha mpaka itakapojulikana ongezeko linatoka wapi
 
Unakumbuka ladha ya maji ilikuwaje Mkuu? tangu utafiti zishindwe kubaini swimming pool ikijazwa lita 40,000 asubuhi jioni inajikuta ina lita 45,000 bila kuingiziwa maji mengine niliacha mpaka itakapojulikana ongezeko linatoka wapi
ati zinatoka wapi hujui kwenye viwiliwili vya watu...๐Ÿคฃ
 
Uwa siyadogelei maji sio beach sio swimming. Mi mrefu 6โ€™2โ€ ila sisogei na sitaki kuyazoea.
 
Ungemalizia.. Jumuiya ya mataifa mbalimbali๐Ÿ˜ƒ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜€๐Ÿคฃ

Ila shukuru nyara zako zimeonekana kwa wazungu๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜€๐Ÿคฃ
hapo ndo nikapewa na pensi yangu nikasitiri nyara ya taifa ambayo ilikuwa imeshaonekana na jumuhia mbalimbali!.
.
 
Ungemalizia.. Jumuiya ya mataifa mbalimbali๐Ÿ˜ƒ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜€๐Ÿคฃ

Ila shukuru nyara zako zimeonekana kwa wazungu๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜€๐Ÿคฃ

.
hiyo mbalimbali ndio mchanganyiko wa wazungu na watz wenzangu, hao wazungu walikuwa wachache tu..๐Ÿคฃ
 
Aiseee nimecheka sana mpaka machozi

Mimi ni fundi wa kuogelea ila kuna siku kidogo nife,nilimbeba mtu mgongon nikaamin naweza kuogelea nae,kilichotokea ni mimi kuwa chini ya maji natapatapa na niliembeba alikuwa hajui kuogelea basi alikuwa kanikaba haswa haswa bahat nzur nilifurukuta chini ya maji nikabahatisha kurudi kwenye kina kifupi yeye jamaa kaning'ang'ania kama luba
 
Wale tuliokulia karibu na maeneo yenye maji, basi maji yalikuwa ndiyo kimbilio letu kama sanctuary Fulani hivi, nimejifunza kuogelea nikiwa na miaka mitano. Michezo yetu mingi ni kwenye maji kama bata. Tulikuwa tunashindana kuogelea kwenye vina hadi unahisi moyo umekuwa na ubaridi au umeganda kwasababu ya maji.
 
Nimechemka sana aisee... Yaani nyara za serikali zilibaki nje kila mtu anaona
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ