Niliwaambia kumfunga Algeria haiwezekani

Wamuite JECHA aje kufuta matokeo. Mapumbavu yanafikiri uweza kuiba kura kila mahali.

Nimefurahi sana!

Mpira ni akili sio nguvu wenzetu walishatusoma kabla ya mechi mi binafsi nilikua sina iman na timu hii...Nilijua tu ni Yale yale tu...
 
Kocha ametuumiza sana, ilibidi sab ya kukaba na si kushambulia koz ushambuliaji ulikuwa fiti. Ila kuna watu yaani usiongee juu ya kumkosoa ngasa alichokifanya akiwa na ndemla,

Tanzania hapa hatuna wachezaji bali tuna mfano wa wachezaji ndio uwezo wao ulipoishia
 
sio mimi kama mchungaji nimeshangilia tu, kwa mizani ya kimataifa, cc tumeshinda na wao wamepoteza points kwa kutanguliwa kuchapwa bao 2-0 na tz. algeria walikua na mfungaj bora wa ligi kuu ya uingereza,yule wa t.spurs,na wengi tu.

We jipe matumaini tu
 
sio mimi kama mchungaji nimeshangilia tu, kwa mizani ya kimataifa, cc tumeshinda na wao wamepoteza points kwa kutanguliwa kuchapwa bao 2-0 na tz. algeria walikua na mfungaj bora wa ligi kuu ya uingereza,yule wa t.spurs,na wengi tu.

Huyo wa totenham kaingia dk 70 mambo yakaharibika kabisa na brahim hakuwepo, baghdadi kaingia dk 88 kulikuwa na islam tu najiuliza hawa jamaa wakianza mara kwa mara moja tutaficha uso wetu wapi
 
Hamna we mwenyewe unajua sisi ni kichwa cha mwendawazimu

Wewe ndio kichwa cha mwendawazimu. Ukikubali kuitwa mwendawazimu, utakuwa kweli mwendawazimu. Siwezi kukubali kuitwa mwendawzimu wakati nina akili timamu na uwezo wa kujifunza na kufundishika kufika walipofika wengine. Hao waliofika mbali walizaliwa na uwezo wa kufundishika kama mimi.
 

..unalazimisha watu washangilie huzuni? au unataka mpaka mtu akose usingizi usiku kwa ajili ya zile nafasi za wazi walizopoteza pale uwanjani ndio uuite uzalendo?!
Mambo mengine wacheni watu wajiamulie tu,msitake kuleta ustaarabu wa kinafiki, kulazimisha watu washangilie huzuni, haitakaa itokee.
If you really want to change it, win your matches,plain & simple.! sio kukariri uzalendo, uzalendo.....wakati matokeo kila siku ya hovyo.
 
kaka wenzako wanacheza soka la kimataifa sisi tunacheza soka la kisiasa so waache watu washangilie wapendavyo mpaka siku tutakapo pata akili ya kutenganisha ivi vitu

Umemjibu vizuri sana
 
Na wakirudiana stars wanafungwa vizuri tu si rahisi kwa stars kumfunga Algeria

Wanarudiana vipi wakati magufuli amepiga marufuku safari za nje😕😕au watacheza mabalozi wetu😀😀
 
kaka wenzako wanacheza soka la kimataifa sisi tunacheza soka la kisiasa so waache watu washangilie wapendavyo mpaka siku tutakapo pata akili ya kutenganisha ivi vitu

Kucheza soka la kimataifa ndio nini? Hivi umefuatilia jinsi gani nchi zisizo na wachezaji ulaya zilivyogonga nchi zenye wachezaji wa kimataifa ulaya? Kwanza unajua maana ya soka la kimataifa? Tanzania na Algeria leo wamecheza soka la kimataifa. Nchi mbili tofauti zinapocheza mechi hilo soka/mechi inahesabika ni ya kimataifa. International game/ international soccer match na wachezaji pia wanakuwa wa kimataifa because they represent their country vs other country. Huwa siwaelewi mnaposema sijui wachezaji wa kimataifa blah blah mnamaanisha nini?
 
Huyo wa totenham kaingia dk 70 mambo yakaharibika kabisa na brahim hakuwepo, baghdadi kaingia dk 88 kulikuwa na islam tu najiuliza hawa jamaa wakianza mara kwa mara moja tutaficha uso wetu wapi

Ni balaa majembe yote waliweka benchi ndio bahati yetu hata hiyo sare tungeisikia tu
 

Teh teh teh mtafute mwinyi umwambie afute kauli
 

...punguza stori wewe na uzalendo wako; bentaleb anatoka (spurz) uje kumlinganisha na nani wa Tanzania, Yacine brahimi porto, (japo hakuwepo) umlinganishe na nani wa Tz..
Wacha kujidanganya na uzalendo wako, utakufa kwa presha bure, rilaxxx, Tz hatujafika levo za wenzetu, hata tukiwa wazalendo vipi, hatuwezi kushinda sababu ya uzalendo tu!
 
Nilikua siamini na nilichotarajia ni sare tu kwa kua tunataka sifa tu sio kushinda mchezo tumeshukuru kwa sare ila bao la samata linazidi kumsafishia njia ya kwenda kua top wa mabao wa lile ya ufaransa
Hongera samata
Kwa maelezo yako kama ni wewe uliyeweka ile post, maneno yako yalimaanisha Algeria aachiwe. Hajaachiwa mtu na laIma wakasimuliane kwao mziki walioupata!
 
Wamuite JECHA aje kufuta matokeo. Mapumbavu yanafikiri uweza kuiba kura kila mahali.

Nimefurahi sana!
Sasa ndo nini hii?
Akisoma Mustafa Ali, Nadir Haroub, Kelvin Yondani, Farid Mussa, Juma Hajj, Samatta, Ulimwengu, Maguri, Himid mao, Yahya, Kapombe, Ndemla, Ngassa, na wengine walio stars watajisikiaje??
Watanzania sisi wenyewe ndo wachawi wa sisi wenyewe!
Les Brown hakukosea aliposema; IF THERE IS NO ENEMIES WITHIN, ENEMIES OUTSIDE CAN DO YOU NO HARM.
Watanzania wengi wana enemies within!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…