Niliwahi kumuona kama rafiki ila yeye alinitumia kama rasilimali, kakwama anataka msaada, Nimsaidie ?

Tatizo lako kuu ni moja

Akili yako inafanya kazi kurudi nyuma, tenga muda uisikilize nafsi yako inataka nini sio kutusumbua hapa wakati tahadhari zote unaziona
 
Ulimwengu unahitaji watu jasiri kwenye kufanya maamuzi ya kiume.
 
Ulimsaidia ili awe rafiki yako zaidi au ulimsaidia ili na yeye atoboe??

Kama lengo ni hilo la pili basi limefanikiwa kama ni hilo la kwanza basi ungemwambia. Na rafiki akikosea mwambie, ajue kakosea.

La sivyo atakua anakuchukulia poapoa sana.
Soma post yote hadi mwisho uielewe utapata majibu ya swali lako
 
We ni daraja kwake anasahau njia zingine utaenda lakini utarudi tena ktk lile daraja sasa ye alivyovuka hana time nalo, we kuwa normal msaidie tu ila tambua hamna rafiki wa kweli apo.
 
Ulishawahi msaidia mtu na asikwambie Asante,, hata Asante nimeiyona hiyo hela.....

Ushawahi ??

Akikurudia next time unafanyaje ??

Unajua kushukuru, ama kusema Asante ni kuonyesha utii na kukubali Kuna mtu amesimama nyuma yako ukapata ada, chakula, bills za hospital, au chochote ulihitaji mtu awe daraja uvuke salama,,

Huyo Hana moyo wa kushukuru trust me,,

Ndiyo maana nyumbani tulikua n a kukuta mfumo wa ukipata chakula, chai Asante mama, ama Asante dada.... Ndo maana ukiwa ugeninii wengine wanashindwa kuishi kutwa kusingizia sipendwii
 
How are you confused sasa?? Seriously! Kama umefurahishwa na matendo yake basi msaidie kwa mara nyingine tena otherwise jibu unalifahamu
 
Waswahili husema kuwa
"Kuwa makini unapomsaidia mtu usibebe matatzo yake"
Kwahy hyo jamaa hana utu ndani yake muache ale janga alilolichuma kwa mikono yake mwenyew
 
Wewe ni mwema kwa kuwa ndivyo ulivyo, siyo kwa sababu watu ni wema. Msaidie. Ndio nature yako, Mungu atakulipa. Wema ama uovu ni akiba. Jiwekee iliyo njema.
Naungana na wewe,usiache kuwa mwema sababu ya watu wabaya
 
since hakuna utapoharibikiwa au kupata madhara ya aina yoyote, we msaidie tu halafu endelea na zako. Wema hauozi
 
Sikiliza moyo wako unakwambia nini. Ingawa kuna msemo wa asiyeshukuru kwa kidogo hawezi thamini kikubwa huyi sio mwana kabisaaaa
 
Dunia imekufundisha halafu hutaki kufundishika nguruwe wewe,wewe msaidie ile jua kuna consequences,siku ukiwa na shida wewe sahau kusaidiwa na huyo bata mzinga
 
Wewe umefanyika baraka. Usiipoteze hiyo baraka msaidie kama ipo ndani ya uwezo wako. Utalipwa na Allah kwa mlango mwingine, hata kama sio wewe basi inaweza ikawa hata uzao wako
 
😜😜😜😃😃😂😤😤 Za mbayuwayu changanya na zako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…