Niliwapa watu hela kwa makubaliano kuwa watanipa mazao lakini hawataki

Simplicity.

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2013
Posts
2,636
Reaction score
1,662
Wakuu habari zenu.

Mimi nipo mjini lakini huwa nafanya biashara ya kununua mazao mashambani/vijijni kwa kutumia wadau wangu, naweka stock halafu baadaye nayauza. Sasa mwaka huu kuna baadhi ya watu niliwapa hela mapema kabla hawajavuna mazao yao, kwa makubaliano kwamba wangenipa mazao baada ya kuvuna. Badala yake wamevuna wakauza mazao yao na hawajanipa magunia mpaka sasa.

Kwa sababu kuna ushahidi kwamba niliwapa hela ili baadaye wanipe mazao, nataka wanilipe kwa kulazimishwa na sheria hela sawa na bei ya gunia (x idadi ya magunia ninayodai) kwa sasa, au walipe magunia ninayowadai. Hivyo nataka kuwafungulia kesi lakini sitaki iwe ni ya madai, maana kesi za madai utampeleka mtu mahakamani, ataahidi kuwa atakulipa taratibu na kurudi mtaani kula bata. Naomba ushauri wa kisheria namna ya kuifanya hii kesi kuwa ni ya wizi wa kukusudia au ushauri mwingine wowote. Lengo ni watoe hela au magunia yangu na wasirudie tena kushobokea hela za watu huku wakijua hawatatoa mazao yao.

Natanguliza shukrani.
 
Huo unaitwa wizi wa kuaminiwa, nasikia...
 
Hakuna kesi ya wizi hapo.

Umesema mlikubaliana so hiyo ni kesi ya madai.

Kama hawajatekeleza upande wao kama mlivyokubaliana huko ni kuvunja mkataba na siyo wizi.

Washtaki kwenye kesi ya madai udai fidia au waheshimu mkataba, provided vigezo vyote vya sheria ya mikataba vilifuatwa wakati mnaingia kwenye mkataba.
 

Kesi ya madai na fidia katika haya mazingira ya biashara inaweza kuchukua sura ya ulipwaji wa kusuasua? Vinginevyo nitafute namna ya kuibatiza hii kesi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…