josephdeo
Member
- Nov 23, 2015
- 95
- 207
Sio mfuatiliaji wa tamthilia kabisa, sio kwa hapa nyumbani. Ila hii imenipa fundisho hili.
Sifahamu ni Nani mwingine ambaye atanufaika na haya lakini ninayo imani ya kuwa yupo hapa. Hivyo hiyo inanipa msukumo wa kuandika.
Ila ipo tamthilia moja ambayo inaitwa blackish ambayo imetayarishwa na Kenya Barris chini ya Abc. Katika filamu hiyo ingawa inafurahisha kuyatizama maisha ya Dre na familia yake. Ila nilipata fundisho moja nadhani hata kwako linaweza kuwa na msaada kama ilivyokuwa kwangu.
Katika maisha ya dre na mkewe kulikuwa na utaratibu wa kupeana zawadi kama wapenzi pale inapofika anniversary ya ndoa yao. Kila mmoja alitoa zawadi aliyoona inafaa kwa mwenzake.
Lakini wakati wote watu hawa hawakufahamu ya kuwa zile zawadi walizokuwa wakipeana. Hawakuwa wanazipenda licha ya kuwa kila aliyempa mwenzake aliamini ni sahihi. Mpaka siku walipoamua kuambia ukweli kuwa licha ya kuonekana wafurahia wakati wanazawadiana lakini hawakuwa wanazipenda.
Hii ikanifundisha Jambo hili ya kuwa tupunguze kujipa umaana kwenye maisha ya wengine. Kwa kudhani kuwa tunawafahamu au tunawajua. Inawezekana akawa anakudanganya juu ya kile unachoona ni sahihi juu yake. Hivyo tujifunze kubalance hulka zetu kwa wenzetu.
Pengine hayo unayodhani ni sahihi kwa yule unayemfanyia ni machukizo ila anakuonyesha tabasamu kama anafurahia ili kutokukukatisha tamaa juu ya juhudi uliyoionyesha. Moyo wa mtu ni kichaka kilicho hifadhi mengi na ni ngumu kuyafahamu bila yeye kuruhusu.
Jitahidi kukwepa kuumia pale unapofanya kitu na isionekane kina umaana kwa unayemfanyia. Kwani hapo unakuwa umetumia akili yako na si yake.