Niliyoyasema kuhusu Yanga SC yetu mlidhani ' natania ' na hatimaye sasa ' Kimenuka ' rasmi huko na kuna ' Mgogoro ' mkubwa sana

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Nakumbuka hapa hapa niliwahi Kuwaasa Wanachama Wenzangu wa Yanga SC kuwa kama kuna Mwaka ambao tumechagua Viongozi ' Wabovu ' na ambao niliwaambieni kabisa kuwa Mmoja wao ambaye ni Mwenyekiti Wetu ni ' Kibaraka ' wa Timu bora kwa sasa Afrika Mashariki kama si Afrika ya Simba SC basi ni huu Watu mkadhani An Eagle nilikuwa ' natania ' wakati kumbe ni kweli Mimi ni Ndege Tai ambaye naona kule ambako wengi Wenu hamuwezi Kuona.

Sasa yametimia ambapo kuanzia Jana kuna ' Mtafaruku ' mkubwa ulitokea Klabuni huku Wanachama wa Yanga SC yetu wakiwa hawamtaki Mwenyekiti wetu kwakuwa ni mwana Simba SC hasa. Ni jana hiyo hiyo kuna Mwanachama Mmoja maarufu na Komandoo wa Klabu ya Yanga alisambaza taarifa yake Mitandaoni na bahati nzuri hata Efm Kipindi cha Michezo cha Usiku waliruka nayo ambapo alitoa Shutuma Kali na Nzito kuihusu Yanga SC yangu / yetu na huku akielekeza Makombora yake kwa Mwenyekiti wetu.

Baadhi ya Shutuma zake ni zifuatazo:

1. Mwenyekiti anatumiwa na Mahasimu wetu Simba SC kutuumiza Yanga SC
2. Mwenyekiti hapatani na Makamu Mwenyekiti wake hasa katika suala zima la Kumpata Katibu Mkuu wa Yanga SC
3. Mwenyekiti amechelewesha Posho na Mishahara ya baadhi ya Wachezaji
4. Mwenyekiti analaumiwa kwa Kuwapendelea mno Wachezaji wageni na akiwadharau wazawa / wenyeji
5. Mwenyekiti hapatani na baadhi ya Wajumbe na kwamba Mwezi December mwaka huu Wajumbe Wanne wanajiuzuru
6. Mwenyekiti hataki Kocha Zahera afukuzwe wakati wana Yanga SC wote hadi Mimi An Eagle tumeshamchoka
7. Mwenyekiti hatulii / hakai Ofisini na Yeye kila mara ni Kusafiri tu huku akiponda raha na Pesa zetu wana Yanga SC

Mwishoni akasema kuwa kuna Mpango / Mkakati ambao Mwenyekiti wetu anahusika nao moja kwa moja ambao ni Kuifanya Yanga SC ipoteze Michezo ama Minne au Sita ili Kuchwa na Simba SC kwa Alama ( Points ) 18 kisha alipwe chake na azidi Kula zake Maisha huku akijiandaa Kugombea Ubunge mwakani katika Mkoa anaokubalika ulio jirani na Dar es Salaam kama nia yake ilivyo.

Kwa mliokuwepo Klabuni jana nadhani mliona jinsi Wanachama / Mashabiki Wenzetu wa Yanga SC wasiopenda Ujinga na Upumbavu walivyokuwa ' wamefura / wamekasirika ' kiasi cha Kuanza Kutukana Matusi ya Nguoni na yote wakiyaelekeza kwa Mwenyekiti na Kocha wetu ' Mbovu ' na asiyejua ' Kuvaa ' Mwinyi Zahera na kama isingekuwa juhudi zangu Mimi An Eagle ( Mwana Yanga SC Kindakindaki kabisa ) Kuwatuliza huku nikisaidiana na baadhi ya Watu wa ndani kabisa tunaoijua Yanga SC yetu huenda lile Jengo letu jana lingechomwa Moto au hata dhahama Kubwa kutokea.

Wana Yanga SC Wenzangu leo ' tugomeni ' kabisa tusiende Uwanjani ili ' tushinikize ' Mwenyekiti wetu ' ang'oke ' kwani kama akiendelea Kuwepo basi Mechi zetu zote Mbili na Simba SC ( tena hii ya sasa ambayo ipo vizuri kila Idara ) tunaweza Kufungwa Goli 7 kwa 0 kwa Kila mechi. Na Wachezaji kama akina Sidney, Molinga, Balinya, Sibomana na Bigirimana wala hawatufai kabisa kwani ni ' Wabovu ' na kama tutaona inafaa basi wana Yanga SC Wenzangu tusiwe tunaona Aibu kuwaomba Simba SC ' watuazime ' Wachezaji wao kama akina Mkude, Ajib, Ndemla, Muzamiru au Dilunga ili watusaidie nasi tuweze angalau Kushinda mechi zetu za Ligi kwani ni aibu kwa Timu yetu hadi leo imecheza Michezo Miwili tu tuna Alama ( Point ) Moja tu wakati wao Simba SC wameshacheza Michezo yao Minne na wana Alama ( Points ) zao 12 Kibindoni.

Wana Yanga SC Wenzangu msiponisikiliza Mimi An Eagle katika hili leo hii hii nahamia zangu rasmi Simba Sports Club.
 
Hizo ni porojo za Mikia Mbumbumbu,Yanga ipo imara sana. Bado tuna imani na Mwenyekiti na benchi lake lote la ufundi. Na kama huamini subiri saa kumi jioni ifike kipigo atakachokipata Coastal ndio itakuwa salamu kwenu nyie Waganga njaa.
 
Hivi wewe mkia una kazi nyingine kweli zaidi ya kuichunguza Yanga?. Nakuhakikishia nguvu hizo unazozitumia kwa Yanga uzihamishie kwenye maisha yako hakika ungekuwa umeshaacha kitambo hata kupoteza muda kucheza draft upenuni mwa majumba ya kihindi hapo kariakoo
 
Me ni mshabiki wa Simba lakini ulichoandika mtoa mada unaonekana ni mchabiki mwenzangu wa Simba na sijui unaandika hivyo kwa faida ipi?hiv yanga ikianguka wewe utapata faida gani?me nataka yanga ifungwe na Simba ikiwa vizuri sio tofauti na hapo.
 
Itasikitisha sana, endapo hizi taarifa zitakua na ukweli...


Cc: mahondaw

Ziamini kwa 99.9999% Ndugu kwani Mimi ni mwana Yanga SC hasa na hata Wana JamiiForums wote wanalijua hilo. Na ili uone kuwa Jangwani Kwetu ' Kumechafuka ' hata Matokeo ya leo dhidi yetu na Coastal Union tayari ninayo. Je, unataka nikupe hapa hapa? Una Moyo wa Kuhimili Uchungu? Mimi kama leo Yanga SC haitoshinda nahamia rasmi Simba Sports Club ambako naona sasa ' Kumenoga ' na kuna raha mno tu. Nakuuliza tena unataka nikupe Matokeo ya leo ili nawe ujiandae Kuandaa ' Bakora ' zako ili Jioni ' tukamfurumishe ' pale Klabuni Mwenyekiti wetu na atuachie Timu yetu?
 

Kuna mambo yanasikitisha sana...

Cc: mahondaw
 
The devil 😈 at work.

Fuatilia ya Swedi Nkwabi ujue undani wake. Ya Yanga tuachie wenye timu yetu.

Naona Mikia mmeanzisha kitengo cha kuichafua Yanga humu JF. It's a wrong platform ya kufanya uhuni huo.

Simba Sports Club morogoro. Maveterans na wapenzi wasimba ktk kikosi.
 
Kuna clip imezagaa mitandaoni ikimwonyesha kocha wetu kipenzi,akiifagilia SiMba ipo JUU,kauli hii imenikatisha tamaa,leo sitakwenda shamba la Bibi(uwanja waUhuru)
 
Kuna clip imezagaa mitandaoni ikimwonyesha kocha wetu kipenzi,akiifagilia SiMba ipo JUU,kauli hii imenikatisha tamaa,leo sitakwenda shamba la Bibi(uwanja waUhuru)
Acha uongo,tafuta uisikilize kwa kirefu,niyamsimu uliopita kuelekea mechi ya simba na Yanga, acha kukurupuka
 
Kadi yako namba ngapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…