Jaribu kuacha kabisa leo umemtukana bibiee kesho inaweza kutokea kwa mtu unayemuheshimu zaidi ukaaibika zaidi kilevi noma usipoweza kukontro
Aisee pole sana mkuu yani kitabia tunafanana na tunashare matukio na yote ni pombe,ila baada ya kuona naharibu imebidi niache pombe na vishawishi vyake,omba msamaha na mambo yatakuwa swaaf,ulevi noumaaah!
Ntakuaidia mkuu pls niamini.Ana umri gani vile?hahahahahah upo serious nikupe. . ? Ntashukuru kweli ukinisaidia kwa moyo mweupe. . .Ata ukitaka vocha za kumpigia ntatuma. . Ila ukifanya kinyume na hapo,ntasikitika sana!
dah mkuu, . .Umeacha kabisa? Dah kumbe kila kitu kinawezekana,. .Naja huko bro,pombe inataka kuharibu future ase
Unastahili kuachwa kwa sababu hii ni mara ya tatu kumtenda!!!!
Kwanza inaonekana matusi yapo akilini mwako na ukipata stimu ndiyo unaamua kumshikia maiki!!!!
Nashauri huyo demu ashikilie msimamo wake ili uanze upya uone kama utapata anayependa kutukanwa na kudhalilishwa kwa kigezo cha ndoa.
hapo inabidi uache tu kamanda wangu, manake huyo ukimkosa utakuja oa kitu cha ajabu kama cha huyo jirani yako hapo!
Yani niliacha taratib kwa kupunguza idadi huwezi amini saivi watu wanashangaa imekuwaje nimeweza,umalaya nimeacha na baby saivi tunaheshimiana mpaka raha
ni uongo kusema hukumaanisha,vitu ulivyomwambia ukiwa umelewa ni vile ambavyo hukosa ujasiri kuvisema ukiwa "sober",so labda ana mapungufu,come clean mwambie,bado una nafasi ya kurekebisha mambo pasipo kutegemea pombe
kijana unawaamini wakware wa humu jf? yaani mpaka uwape namba za simu za bibi yako? come on vaiko,this is a social forum,chunga privacy yako!hahahahahah upo serious nikupe. . ? Ntashukuru kweli ukinisaidia kwa moyo mweupe. . .Ata ukitaka vocha za kumpigia ntatuma. . Ila ukifanya kinyume na hapo,ntasikitika sana!
....Hustahili kuwa na binti kama huyo, inabidi upate chakaram mwenzio labda ndio utatia akili kichwani. Ukipata bahati ya kusamehewa kwa mara nyingi tena basi achana na kilevi kabisa na wala si kwa miaka miwili bali usiguse tena kilevi maishani mwako, kilevi kinakuharibia maisha yako...utabaki unajuta na kulia kilio cha mbwa.
thanks mkuu, . . Well said, . .Fikiria hivi "nina marafiki kumi wote walevi na ninatumia masaa kama manne tu kuwa nao kwa siku, nina mke ninaempenda sana na ninatumia zaidi ya masaa kumi kuwa naye kwa siku, kipi ni muhimu katika maisha yako" mi nafikiri kuacha pombe sio ngumu kihivyo kama kweli una nia ya dhati, usihofu kupoteza marafiki kwa sababu utaacha pombe, utapata wengine