Nimeacha Kutumia Sukari kabisa na chumvi kidogo. Je, kuna madhara?

Nimeacha Kutumia Sukari kabisa na chumvi kidogo. Je, kuna madhara?

KimChi

Senior Member
Joined
Feb 14, 2018
Posts
122
Reaction score
161
Wadau habari,

Nimekuwa ni mpenzi sana wa kutumia sukari, chumvi na pilipili nyingi siku za nyuma, nina miaka 27 na siku ambazo nilitumia sukari kidogo ni zile tu ambazo nilikuwa shuleni boarding (std 1 had form 6) na chuo sikuwa nakunywa chai, chumvi na pilipili nimetumia nyingi kwa kipindi chote hicho, soda nilikunywa mara nyingi nilipokuwa chuo, bia na vinywaji vikali natumia mara chache na kidogo sana(kukiwa na party tu).

Kama mwezi umepita nimeacha kutumia sukari kabisa na chumvi nimepunguza hii ni baada ya kuamua kujipunguzia uwezekano wa kupata magonjwa yatokanayo na matumizi ya vitu hivyo kwa wingi huko utu uzimani. Swali ni je kuacha kabisa ni suluhisho au kuna madhara yoyote kiafya kwa kuacha kutumia kabisa hivi vitu.
 
Kuacha kutumia sukari hakuna madhara kiafya, badala yake utaipata kwenye matunda. Chumvi ni muhimu usiache kabisa kula kawaida kwenye mboga.
 
Tumia kila kitu kwa kihasi ,fanya mazoezi ,kunywa maji ya kutosha ,kula balance diet utaepuka hayo magonjwa!! Sukari ndio chanzo cha kwanza cha energy mwilini.
 
Tumia kila kitu kwa kihasi ,fanya mazoezi ,kunywa maji ya kutosha ,kula balance diet utaepuka hayo magonjwa!! Sukari ndio chanzo cha kwanza cha energy mwilini.
Nashukuru sana mdau
 
Back
Top Bottom