Nimeachana na hawara nachanganyikiwa

Kwakweli wanaume tunakazi kubwa sanaa wewe kila nashokupa bado unakuja lalamika jukwaani ahahaa
natania jamni, namuona Lizzy kawaka kweli sijui aliwahi kufanya kazi lugalo
nihivi hawa wote ni wazinzi, na dalili huyo dada kaisha onyesha ubaya wake kutoka nje bila kujali usalama wako na afiya kwakuwa sas maradhi yametapakaa na kutojaribu kutafuta ufumbuzi wa tatizo lenu mana tumesoma kuwa na hapo nyuma uliwahi kuomba msaada ukashauriwa lakini hujatuweka wazi kuwa uliyatumia vipi mawazo ya jamii kumficha kijana ni hatari sana huyo kijana angehatarisha maisha yake na pia umeisha muumiza sana ki saikolojia atwachukulia wanawake wote kuwa ndo hiyohiyo sina lakushauri ukivunja ndoa utakuwa kwenye ndowano akili mkichwa
 
haya yote ni ubatili nimekosa la kukwambia mpenzi wangu
 
Hebu jamani kila mtu humu anashutumu wanaumetu je huyu dada nae mbona hasemi nayeye sika katoka nje ya ndoa au hahesabiwi matusi yote kwa wanaume sio vizuri wajemeni tunayo wafanyia mengi na uvumilivu wetu ni mkubwa sana hebukuweni na usawa haki
 
Lizzy nakubali kwa asilimia miamoja japokuwa umetoa hukum kali sana kweli kama mwanaume humpendi siuachike, huwa nainjoi sana ushauri wako hakuna siasa, nikama Bwana Bushi alivyokuwa madarakani
 
Hebu jamani kila mtu humu anashutumu wanaumetu je huyu dada nae mbona hasemi nayeye sika katoka nje ya ndoa au hahesabiwi matusi yote kwa wanaume sio vizuri wajemeni tunayo wafanyia mengi na uvumilivu wetu ni mkubwa sana hebukuweni na usawa haki

Wote wabaya bwana.
Ila dada anashangaza kutaka kula kipande cha keki na kukiweka kwa wakati mmoja!Unachotakiwa kufanya ni kilinganisha faida na hasara na kubaki/kuondoka kisha uchague kile chenye faida zaidi kwako.Maana mume umeshasema humpendi tena ila hutaki kumwacha kwaajili ya mtoto na wakati huo huo unataka uwe na kijana wako wa chuo kwasababu unampenda sijui mnapendana....ukiendelea hivi utakua huwatendei haki hao wanaume au hata mwanao.Kaa chini ufanye maamuzi magumu na uwe tayari kuishi nayo!!

Kila la kheri...Mungu akutangulie!!
 
Lizzy nakubali kwa asilimia miamoja japokuwa umetoa hukum kali sana kweli kama mwanaume humpendi siuachike, huwa nainjoi sana ushauri wako hakuna siasa, nikama Bwana Bushi alivyokuwa madarakani

Hahahhahha Kasopa mbona unanichekesha kwenye thread ya masikitiko ndugu yangu!!?Mi nadhani achague tu kipi ni muhimu zaidi kwake atulie nacho....huwezi kupata joto na baridi kwa wakati mmoja bila usanii!
 
Kinga mtu kawaka hivi, hapo ni nyama kwa nyama thats why amekolea msichana
 
Mimi mdada nakushauri tu utafute njia ya kusolve issue na mumeo kwakuwa watu tumeona watu wakiumbuka sana, wanatoka kwa waume zao wakidhani wamepata happiness kumbe ni hila tu wanafanyiwa, huyo mwanafunzi kakupenda sababu uko kwa mumeo toka uone kama atakutupia hata jicho, hata kama hakujua una mume kwa kifupi mumeo ndio kakutunza umekuwa hivo ulivyo na yyeye kakuona, mie nazimia sana wanaotetea ndoa zao, kwa maslahi ya family....na haswa uliposema kabadilika ndio kabisa nora usiondoke , mie nahisi wewe pia ni tatizo humo ndoani badilika utafaidi matunda yake
 
Atakula MBIVU Lizzy, umekosea Mamii!!
Well akivumilia kwa muda MBICHI zitakua MBIVU....sasa asipozila kwa muda muafaka na kuendelea kuvumilia atakuja kuambulia MBIVU zake zilishakua MBOVU zamaniiiiii!
 
Kuna madhara ya kuolewa utotoni.sijui circumstance zilizokufanya uolewe mapema ila naona uliwahi sana.mfikirie mwanao na ufikirie maisha yako ndugu yangu, kama ndoa imekuwa chungu ebu ivunje kihalali kwanza kabla hujaanzisha mengine.
 
Its hard when sisi wanawake tunapotegemea yoote kwa mume na hivyo tunaogopa kujitoa kwani waume zetu ndio wanatuweka mjini, na pia kwavile tunamatumaini mfu kuwa 'atajirudi tu'

Nadhani una uwezo wa kufikiria kwa makini sana kwanini uko naye mpaka leo, je kuna tarajio lolote ?

Yawezekana kuwa na huyo kijana ni kufullfill 'lust' na sio penzi na ni upweke unaokusumbua na kutafuta appreciation..

Kwakuwa yote yametendeka na amerudi kwenye mstari, pima mwenyewe kama unataka muendelee, ama la anza kufikiri ufanye nini na maisha yako, wewe kwangu ni mdogo sana na bado una muda wa kusoma na ninaamini ukianza shule itakukeep busy kidogo utasahau mambo ya mapenzi ama utapata penzi jipya

Kama Dr Phil anavyosema 'tell it like it is' wewe mwenyewe una uwezo wa kuamua usuke ama unyoe, na madhara ya option zote mbili sambamba na faida zake pia unazo

Nakutakia wakati mzuri ukifikiri juu ya haya yote!
 
ni kweli naunga mkono hoja.
 
Mbona ilo ni tatizo dogo sana, anachotakiwa ni kuwaita wazee wake na wa mumewe, wakae pamoja na kuyazungumza. Vilevile kama wao ni wakristo ni kuwaona viongozi wa kanisa lenu ili waje kuyazungumza na kuwasuluisha. Haya mambo ya kuachana mara nyingi yana madhara yake kifamilia.

Na kama ikishindikana yote hayo basi ndio mfikirie hayo mambo ya kuachana....! Kwenye ukristo si kwamba taraka haziruhusiwi ila kinachopelekea taraka ni pale sababu za msingi za kuvunjika kwa ndoa, na kama zipo hakuna budi kuwepo utaratibu unaozungumzia suala hili la talaka.

Suhala ambalo limezungumziwa kwenye agano jipya ili kupelekea watu kuachana ni Uasherati, kama imethibitika kwamba Mume/Mke ni muasherati basi taraka inawezwa kuombwa na mmoja wa wahusika. Na kutokana na maelezo yaliyoko hapo juu, inaonyesha kwamba kila mmoja ni Muasherati.

Nami nawaambia ninyi, Kila mtu atakayemwacha mkewe, isipokuwa ni kwa sababu ya uasherati, akaoa mwingine, azini; naye amwoaye yule aliyeachwa azini.

(Biblia ya kiswahili Union version: Mathayo 19:9 pia Mathayo 5:32)
 
Kuna madhara ya kuolewa utotoni.sijui circumstance zilizokufanya uolewe mapema ila naona uliwahi sana.mfikirie mwanao na ufikirie maisha yako ndugu yangu, kama ndoa imekuwa chungu ebu ivunje kihalali kwanza kabla hujaanzisha mengine.
Kweli kabisa tatizo huwa tunajifikiria sie tu
 
Ungefanyaje sasa na mwenye mali keshagundua?

it depends na ni mwanamke anataka....
unaweza mshauri adai talaka mliendeleze libeneke kwa uhuru

au kumuacha aendelee na mumewe.....

hapo mwanamke ndo anatakiwa atoe maamuzi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…