Lizzy, ni ushauri mzuri, lakini huyu dada yupo kwenye ndoa, na sio vizuri ku-solve tatizo kwa kukimbia, kwani hadi wanaoana alikuwa hajui kuwa anampenda?
Hapo kwenye RED ndio ukweli..
Dada, Mama K, asante kwa kutuomba na sisi tukushauri ufanye nini...
Kikubwa ninachokiona mapenzi na huyo mwanafunzi yajengwa katika misingi ya ngono..na mara nyingi ngono ya uwizi inaonekana ni tamu, lakini madhara yake ni makubwa.
Tayari umefanya vyema kumshauri huyo kijana atafute maisha mengine; na sioni sababu ya wewe kuendelea kuwa naye wakati umeshajua nini kinaendelea.
Nakushauri utafute muda ukae na mumeo muongee yanayowasibu..Kama umekuwa na ushahidi wa kutosha kwa mumeo kuwa anatoka nje ya ndoa, kwanini usiyapeleke kwa wazazi au washenga wenu?
Hapa unasema;
Umefanya kosa, ndo maana hata moyo wako unakusuta..na huwezi kulipiza baya juu ya baya, na ikanonekana ulifanya haki. Kosa ni kosa tu.
Mie ninaona wewe bado ni msichana mdogo, 24, na maamuzi unayoyafanya ni ya kitoto. Angalia sana, usije ukapoteza ndoa yako kwa sababu tu ya huyo mwanafunzi. Hapa unasema mume wako yuko busy,ni mtu wa safari, una hakika gani kwamba amekuwa ni mtu kutoka nje??..
Hakuna ndoa iliyokamilika dada, zote zina shida kuliko..na unayofurahia mapenzi ya huyo kijana kwa sababu tu hakuna majukumu mengine mazito kama huyo kijana kutafuta chakula, kulea mtoto, yaani kwa kifupi, kinachowakutanisha nyie ni ngono tu..
Sasa kama unataka kuona maisha machungu, achana na huyo mume wako, na ukaishi na huyo kijana, halafu ndo utajua nini maana ya majukumu.. Inaonesha wewe ni mama ya nyumbani, sidhani kama mumeo hakupi matunzo mengine. Sina mengi, ila achana na huyo kijana kama ulivyoamua na uanze kujenga ndoa yako upya. Simama mwanamke..simamia ndoa yako.