Ndugu wapendwa wa MMU, Nimeona niahirishe kuoa baada ya kukutana na wapenzi 2 humu jf tukakubaliana na suala zima la ndoa lakini mwisho wake wananitosa. Mmoja tulifikia hatua ya kwenda kutambulisha dakika za mwisho akaingia mitini. Wa pili tulifikia hatua ya kuonana tufahamiane baada ya kuafikiana kila kitu kwenye mawasiliano nae akazamia kusikojulikana. Haikuishia hapo, mwingine nikakutana nae kanisani tukaweka mambo sawa mwezi sasa umepita kakata mawasiliano. Anadai suala la kuolewa halipo tena kwenye akili yake. Kwangu mimi umri unasogea lakini nimeona tu bora niahirishe kuoa niendelee na maisha ya peke yangu kama kawaida kuliko kuendelea kudanganywa na hawa wanawake. Kama kuna ushauri nipeni waungwana.