Nimeajiriwa secta binafsi, nahitaji kukopa benki (CRDB)

yaasary

Senior Member
Joined
Mar 26, 2011
Posts
110
Reaction score
59
habari zenu wakuu, nimeajiriwa katika secta binafsi na ninamwaka mmoja sasa katika ajira hii, nimekuwa nikifuatilia habari za upatikanaji wa mikopo( hasa humu JF) na kwa taarifa ninazoziona ni kuwa mikopo inahitaji dhamana ya mali mfano nyumba, viwanja au gari vitu ambavyo mimi siko navyo. sasa nilikuwa nahitaji msaada kwa wale wenye ujuzi/uelewa wa hitaji langu,naomba mnijuze yafuatayo;
1) je ninaweza kupata mkopo benki( hasa CRDB) kwa kutumia hii ajira yangu
2) kama ni ndio, je nifuate taratibu zipi au vitu gani vinahitajika
3)nimetazamia kukopa kiasi cha 2M, basic salary yangu ni laki tano(500000 tsh) je inawezekana, marejesho yake inakuwaje(muda, riba), or minumum and maximum amount ambayo naweza kukopeshwa ni kiasi gani
N.B
nimweka benki ya CRDB kwa sababu ya kwamba ndiko mshahara wangu unapowekwa na mwajiri wangu
unaweza nipa maelezo au ushauri wowote kuhusiana na mada yangu kwa sababu lengo kuu ni kupata mkopo kulinga na hali yangu niliyoieleza hapo juu,
Akhasante
 
Taratibu za benki nyingi ni kutoa mikopo kwa wafanyakazi wa waajiri ambao wana akaunti nao

Kwa mfano wewe mwajiri wako ana akaunti na CRDB na ndipo anapokulipia mishahara yako

Mfuate afisa wa Rasilimali Watu hapo ofisini kwako...Muulize kama Kampuni yenu inawadhamini wafanyakazi kwenda kukopa benki

Baada ya hapo...tembelea tawi lolote la CRDB utapata maelekezo mazuri zaidi
 
Sijaona sababu ya wewe kuja hapa Jf na kuuliza suala kama hilo,ndio maana karibia benki zote wameweka "Customer Enquiry"isitoshe ni mdau wa CRDB.
 

nashukuru kwa ushauri wako, inamaana kuwa kampuni zina option za kudhamini au kutokudhamin wafanyakazi wake kukopa benki,
asante
 
Sijaona sababu ya wewe kuja hapa Jf na kuuliza suala kama hilo,ndio maana karibia benki zote wameweka "Customer Enquiry"isitoshe ni mdau wa CRDB.
hujaona sababu na ndio maana hujauliza wewe ,
 
nakushauri nenda kwa afisa mikopo benki husika kapate muongozo.. over..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…