Jinamizi, ni neno linalotumika kwa waginjwa au watu fulani kutaka kueleza jinsi anavyo "kabwa" wakati akilala usiku!!
Neno la kiingereza huitwa Breathlessness na lile la kitaalamu huitwa "Paroxysmal Nocturnal Dyspnea" (PND)
Hii hutokea pale kunapokuwa hakuna uwiano sawa kati ya damu inayozunguka mwili hasa itokayo na kwenda katika mapafu( Pulmonary Circulation) na Upumuaji wa hewa ya Oxygen..
Mkandamizo/Shinikizo(Pressure/Tension) unapokuwa mkubwa katika uwiano huu hasa kwa watu wenye magonjwa mengine tayari mfano moyo, mapafu, ini, figo pia uzee, n.k husababisha damu kurudi katika mapafu badala ya kuendelea na mzunguko wake wa kawaida...na kwa vile mapafu hutumika kwa kupumulia(Breathing), maji au damu yanapokuwa yakijaa husababisha mtu kushindwa kupumua vizuri, na wagonjwa/watu wengi husema "NIMEKABWA NA JINI ila baada ya kufungua madirisha liliondoka"...
Watu wengi husema hivyo kwa sababu mtu ukisimama mkandamizo ni mkubwa na hivyo kulazimisha kutoka katika mapafu kwenda katika moyo, na ile damu kidogo inayobaki due to gravity haileti madhara..lakini pale mtu anapolala tena, mzunguko ule ule hutokea na hivyo kufanya mtu kushindwa kulala, ..kutumia mito(pillows) husaidia katika hali hii, lakini ikumbukwe kwamba the more the pillows the worse the condition.
MUHIMU: Hali hii PND, "Kukabwa na jinamizi" hutokea na dalili nyingine kama kuchoka haraka,(katika kupanda ngazi, kutembea mwendo mfupi), mapigo ya moyo kwenda kasi, kusikia kizunguzungu n.k ila watu wengi hupuuzia kwani huona ni jambo la kawaida hadi pale hali inapokuwa mbaya kwa kushindwa kulala na hivyo kwenda hospitali..
Ushauri: Ni vema kuwahi HOSPITALI hali hii inapojitokeza.