Nimeambiwa Simba SC wakitumia Low Block na Counter Attack Wydad Casablanca FC anatupeleka Semi Finals CAFCL

Wahakikishe yule jezi namba Tano(5) wa WAC hafanyi chochote cha maana, itakuwa ngumu ila naamini Simba ina wachezaji wanaojitambua, yule asije akafanikiwa kupiga pasi za maana mbele karibu na boksi yatakuja maafa makubwa tena nyumbani kwao hiiiiii, rafu za uzembe na zile za karibu na boksi ni hatari wachezaji waambiwe hili, tshabalala kama atakuwepo awe makini sana ule upande wake tena naamini deadly passes zitatoka kati zitamiminika sana upande wake, ni suala la kujitoa zaidi uwanjani na kufia huko ndani na cha mwisho nadhani mazingira ya uwanja wanayafahamu au washaambiwa tayari jinsi vagi la uwanjani (mashabiki), wasiwaogope "ultras winners" kwani wao ni kawaida kushangilia mwanzo mwisho, ni suala la kujitambua na kujituma kwani inawezekana hiyo siku hata sauti au maelekezo ya kocha kwenye mechi wasiyasikie kutokana na sauti za ultras wao kuwa juu Hadi majengo ya lodge au hoteli zilizo karibu na uwanja kutikisika vibaya mno...
 
Tulicheza semi 1974, hatutaki utopolo hapa. Heshima kwanza!
 
 
Mkuu hao WYDAD huo mfumo hawaufahamu au sio?
 
Kaka tz Kuna timu inayoabudu uchawi kama Simba?? Kutoka mbezi hadi temeke kinyumenyume ni uchawi bado ukaunguza uwanja wa watu ugenini na ukapigwa ya mbavu
 
Huyo jini mwambieni akafie mbele huko manina,hapo kwenye 4 1 41 ndo penyewe hapo,huo mfumo unaweza ukachanganyikiwa ukicheza nao,alipigika sana horoya na huo mfumo asee..[emoji109]
Usifananishe Waydad na vitu vya kijinga..!! Waydad anafungwaga ugenini halafu kwao anakutia nusu kaputi na kukutwanga kuanzia 4 kwenda mbele
 
Mfumo huo mzuri ila inahitaji pumzi ya maana maana kuruhusu counter attack ni rahisi zaidi. Ushauri wangu timu ijaze viungo kwaajili ya kuharibu movement za adui. Lakini pia kama kocha ataona inafaa Mzamiru, Kibu D na Putin kanute wacheze nyuma kidogo kuwasaidia mabeki huku wakifanya mashambulizi ya kushitukiza nasema hivyo ili mipira yote inapigwa na mabeki wakitingwa iokolewe haraka.
 
Ni mfumo mzur sana sanaaa.....wajuzi tusaidiane Kwa hii Simba yetu hatuwezi kucheza Kwa kuwakamia Hawa raja yaani tucheze man to man....
Tucheze Kwa kukamia ila Kwa akili sana maana waarabu Kwa kujiangusha........

Nimemkumbuka
Gennaro Gattuso
 
Mkuu huwa unanifurahishaga sana comments zako, eti wooote mizigo[emoji3]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…