Nimeamini CCM itaendelea kutawala hii nchi mpaka itakapoamua kupumzika

Nimeamini CCM itaendelea kutawala hii nchi mpaka itakapoamua kupumzika

Vichekesho

Member
Joined
Jun 20, 2024
Posts
66
Reaction score
3,277
Mambo mawili niliyo amini baada ya taarifa ya utumbuzi wa Nape Nnauye na wengine ni

1. CCM itaendelea kuitawala hii nchi miaka tele ijayo.
2. Yanga itaendelea kutawala soka la hii nchi

Kwanini?
Watu wamesahau kuwa uteuzi na utenguzi ni maigizo ya CCM miongo na miongo, Nape huyu na January huyu, waliteuliwa awamu iliyopita na kutumbuliwa na watu wakashangilia sana.

Awamu hii wakateuliwa na January akashindwa waziwazi kutatua changamoto za wizara ya nishati, akahamishwa, watu wakashangilia sana.

Juzi nape kazungumza hadharani ile tabia yao ya wizi wa kura, jana ametumbuliwa watu wameshangilia sana.

Hivi karibuni Luhaga Mpina atateuliwa kuchukua nafasi ya Bashe, watu watashangilia sana.

CCM ni ile ile, oooh ni ile ileee x2
 
Hujakoseaa hata kidogo mkuu ,CCM inacheza na akili za watanzania haswaaaa. Hyo yanga ss na hyo cmba pita mtaanii redio zote na vijana wt ndio mada zao za Kila cku.
 
Mambo mawili niliyo amini baada ya taarifa ya utumbuzi wa Nape Nnauye na wengine ni
1. CCM itaendelea kuitawala hii nchi miaka tele ijayo.
2. Yanga itaendelea kutawala soka la hii nchi

Kwanini?
Watu wamesahau kuwa uteuzi na utenguzi ni maigizo ya CCM miongo na miongo, Nape huyu na January huyu, waliteuliwa awamu iliyopita na kutumbuliwa na watu wakashangilia sana.

Awamu hii wakateuliwa na January akashindwa waziwazi kutatua changamoto za wizara ya nishati, akahamishwa, watu wakashangilia sana.

Juzi nape kazungumza hadharani ile tabia yao ya wizi wa kura, jana ametumbuliwa watu wameshangilia sana.

Hivi karibuni Luhaga Mpina atateuliwa kuchukua nafasi ya Bashe, watu watashangilia sana.

CCM ni ile ile, oooh ni ile ileee x2
Hyo no 2 ya YANGA - umenikosha mkuu!!naunga mguu hoja
 
Watanzania wamejikatia tamaa.
Wakisikia habari za vifo, ajali au kutumbuliwa mtu ndio hupata faraja.
 
Bingwa wako mara 30, Yanga ndio walioleta uhuru wa nchi hii. CCM ni Yanga.
Punguza utoto dogo. Ccm watatawala milele kwasababu ya watu kujadili Nape na January kutolewa kwenye nafasi zao ama? Huu ndio mjadala wa leo, tatizo liko wapi watu wakijadili?
 
CCM itatawala milele iwapo katiba haitabadilika, vyombo vya dola vitaendelea kuumiza watu kwa niaba ya chama na Tume ya uchaguzi isiyo huru na sii vinginevyo. Hatuwezi sema ccm haijafanya vitu vizuri hapana wamefanya ila sera zake na mstakabali wa Taifa na kwa jinsi na kasi ya mabadiliko hakiwezi tena kwenda kwa kasi hii na generation ya sasa. Change must come kwa njia zozote ziwe nzuri au mbaya ili kutoa mwanya kwa mawazo mapya ili nchi iendelee. Nchi imebadilika na kuanza kutukuza mtu na sii sera, tumeanza kidogo kidoko kuegemea kwenye udini navyo ni viashiria vibaya sana kwa mstakabali wa Taifa hili. Aina ya utawala wa kikumunisti juu ya uchumi (centralised economy) na centralised management (we need provincial governance kuwapa watu mwanya wa kujitawala kutokana na mazingira yao) nao umepitwa na wakati na kutudidimiza kwenye umaskini zaidi. We need to change drastically.
 
Back
Top Bottom