Wapi Huko kwenye fursa Mkuu!Wanajamii mko fresh eee...
Ebwana haya maisha ni noma sana, mambo yanachanganya na mengine yanachosha moyo.
Baada ya kujitafuta sana kwa miaka mitano kwenye harakati mbalimbali, hatimaye leo nmeamua kubadili mwelekeo wa mambo.
Nilianza na kupanga chumba kimoja, baada ya mwaka nikaona nina uwezo wa kumudu nafasi kubwa zaidi... nikahamia chumba na sebule. Harakati hazikupoa, nikaona nioe.
Huko nikaishia kupigwa za uso na nikamfukuza mke. Maisha yakawa bomba sana kwa kiasi chake. Nikafanikiwa kununua viwanja vitatu, boda 2 na kuongeza msuli wa kazi.
Mwezi wa pili nilikaa nikaitafakari kazi + mazingira ninayoishi nikajiona ni kama mda wote sikuwa kwenye mstari ninaoutaka.
Niliamua kuuza kila kitu, viwanja vyote, boda zote na mzigo wa kazi nilokuwa naifanya hadi kila kitu cha ndani.
Nilikamata milioni 16 huku nikiwa sina hata pa kulala, japo chumba nilibaki nacho. Nilisepa nikaenda mkoa ambao sikuwahi hata kuufikiria, nikasoma upepo nikaona kuna fursa.
Nilinunua mashine 2 za kukamua alizeti pamoja na mashine 1 ya kuparata mkonge then nikaingia sokoni.
Niliajiri vijana 9 nikaanza kukimbizana na fungu la kupata au kukosa.
Kwa sasa maisha yameanza na ukurasa mpya. Hadi sasa nimesev milioni 7 tu kwa miez 2.... japo ka moyo kanadunda kwa maamuzi nilochukua.
Ila fresh... nimejilipua.
viwanja 3, boda 2, mzigo wa biashara, vitu vyote vya ndani.....16M?? hii chai. Nikafanikiwa kununua viwanja vitatu, boda 2 na kuongeza msuli wa kazi.
Niliamua kuuza kila kitu, viwanja vyote, boda zote na mzigo wa kazi nilokuwa naifanya hadi kila kitu cha ndani.
Nilikamata milioni 16 huku nikiwa sina hata pa kulala, japo chumba nilibaki nacho.
Michepuko inakufilisi!Hongera mkuu ila umetake risk kweli kweli kimjini mjini umiliki hivyo vitu vyote unakua ushamaliza maisha ni kuongeza tu michepuko.
Je kama vilikuwa viwanja vya mil mbili mbili huko vikindu?viwanja 3, boda 2, mzigo wa biashara, vitu vyote vya ndani.....16M?? hii chai
Chai kivipi labda kila kiwanja ameuza million 3 na boda ameuza 2..5viwanja 3, boda 2, mzigo wa biashara, vitu vyote vya ndani.....16M?? hii chai
Mimi nimejenga kwa vile sina mke mpaka wenzangu wanashangaa bila ya mikopo.Kuna kipindi nilikaa bila mwanamke kwa miezi 6 nilisave 21M.
Wanawake ni financial vampire,lakini ndio hivyo huwezi kuishi bila wao ni sehemu ya maisha yetu.
Hakika michepuko n hatariMichepuko inakufilisi!
Wewe ni bank hadi ujue hicho kiasi Kwa account yake?Utafika mbali sana,ongeza bidii na punguza matumizi.kuna mdada namjua naye ana hizo machine za kukamua alizeti anapiga pesa sana,kwenye account yake ana 90M just za faida inayotokana na hiyo biashara.