Nimeamua Kulima kwa mara ya Pili kilimo cha mahindi

Lasway.Jr .... naomba ushauri wa kilimo cha mahindi madogo ya njano yajulikanayo kama mahindi ya bisi (Popcorn) ... hali ya hewa, upatikanaji wa mbegu bora na mavuno .... hii iwe ni kutumia uzoefu wa hapa nchini kwetu
 
Katika hatua muhimu za kilimo cha ahindi ni palizi. Palizi huwa linahitajika ili kuondosha ushindani wa mahindi na magugu kwa nutriets na mwanga. Bila palizi kiasi kikubwa cha mazoa hupungua kwani mmea hushindwa kukua vizuri.

Magugu yanaweza kusababisha kupungua kwa mavuno hadi asilimia 90 yasipodhibitiwa. Wataalamu wanabinisha kuwa kipindi muhimu kabisa cha kuzuia magugu katika zao la mahindi ni wiki ya kwanza mpaka ya nane toka kuota.

Zipo namna nne ambazo zinaweza kutumika kuzuia magugu. Moja wapo ni hii maarufu ya kupalilia kwa jembe. Palizi hili huwa likifanyika usahihi linasaidia sana mmea lakini linahitaji nguvu kazi kubwa na linachukua muda mrefu. Kipindi cha palizi vibarua wengi wanakuwa mashambani mwao na changamoto ya kuwapata huwa ni kubwa.

Ili kurahisha palizi kuna njia nyepesi ambayo ni ya kutumia kemikali (herbicides Viuagugu) za kuua magugu. Nitaeleza faida na hasara za hizi viuagugu
 
Asante kwa darasa zuri sisi wakulima tumekuelewa. Mimi niko Tanga mbegu niliyotumia ni seed. co vp unaweza kunisaidia sifa ya hii mbegu?

Mkuu unalima Tanga sehemu gani naona sehemu nyingi bado mvua hazijaanza hapo Tanga. Mbegu nyingine ambazo waweza otesha zikafanya vizuri ni DK8031,Pannar 4m -19, na hizi Seedco 403 au 513.
 
Ingia hapa
Kilimo cha Mahindi
 
Majibu yako hapa

Kilimo cha Mahindi
 
Mkuu BabM

Kwa Dar es Salaam ni mbegu gani ya mahindi inafaa kulima?

Asante.
 
Mkuu BabM

Kwa Dar es Salaam ni mbegu gani ya mahindi inafaa kulima?

Asante.

Kwa Dar mbegu ambazo zinakomaa kwa muda mfupi zinafaa zaidi na ambazo ni za ukanda wa chini. Mbegu ambazo zinakomaa kati ya siku 90 na 120 kama zilivyoanishwa hapo juu. Mbegu nyingine ambazo waweza otesha zikafanya vizuri ni DK8031,Pannar 4m -19, na hizi Seedco 403 au 513.
 
somo zuri sana mkuu. naomba basi uje na somo la Maharage pia
 
Hakika, hii ni elimu kamambe.

Kupitia elimu kama hii tunaweza kuondokana na umasikini kwa kupata taarifa sahihi na mahususi juu ya teknolojia za Kilimo na kuzifanyia kazi ipasavyo.

Asante sana mkuu, bila shaka wewe ni mtu unaye husika na mbegu bora za Kilimo.

Kama ni ndivyo ningependa kujua upo taasisi gani au duka gani la pembejeo za Kilimo ili kuweza kupata ushauri wa karibu zaidi?

Asante.
 
Mkuu unalima Tanga sehemu gani naona sehemu nyingi bado mvua hazijaanza hapo Tanga. Mbegu nyingine ambazo waweza otesha zikafanya vizuri ni DK8031,Pannar 4m -19, na hizi Seedco 403 au 513.
Mkuu mimi nalima muheza na kwa sasa niko kwenye palizi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…